Kwa kinachoendelea Mahakamani kwenye kesi ya Mbowe, imedhihirika CHADEMA walikuwa sahihi kutokwenda Mahakamani baada ya uchaguzi Mkuu wa 2020

Ijumaa_kariim%F0%9F%95%8B.jpg
 
Kuna watu wengi waliituhumu CHADEMA kwa kutokwenda mahakamani baada ya kuporwa uchaguzi Mkuu wa 2020. Cdm walisema baadhi ya taasisi za umma zilizoingiziwa uozo wa siasa chafu za ccm, ni pamoja na mahakama.

Kwa sasa kwenye kesi hii ya Mbowe ushahidi unazidi kukaa wazi, na bado kesi haijafika mwisho, lakini tayari majaji wawili wameshatoka, na huyu wa sasa amejaa maamuzi ya utata, na sidhani kama atafika mwisho wa kesi.

Kubwa kuliko yote ni mahakama kutumika kuvujisha nyaraka kwa mashahidi wa jamuhuri kinyume kabisa cha sheria, na utawala wa mahakama uko kimya kuhusu hilo! Iwapo mahakamani ndio sehemu tunaambiwa ni ya kupatia haki, na inatakiwa tuiamini kuwa itatenda haki, wanashirikiana na watu waliobambikizia kesi, ni taasisi ipi tena ya umma inaweza kuaminika?

Kwa hapa tulipofikia ni kwa jinsi gani tunaweza kukwepa katiba mpya, wakati hadi mahakama imekubali kutumikia siasa chafu za CCM?
WALIOJIINGIZA KWENYE TAALUMA SIO WATU SAHIHI KWA SASA.....WAMEINGIZWA KUHARIBU TASWIRA YA SHERIA NA HAKI......WAMEKUWA WALA NJAMA.....SHERIA HAIKO HIVYO NYIE MAJAJI PANDIKIZI....TOKA ENZI ZA MABABU HAIKUWA NAMNA HIYO......WASTAAFU MAJAJI....MSIKAE KIMYA.....HALI HII IKIDUMISHWA NA WATU WAKIKATA TAMAA NI HATARI
 
Kuna watu wengi waliituhumu CHADEMA kwa kutokwenda mahakamani baada ya kuporwa uchaguzi Mkuu wa 2020. Cdm walisema baadhi ya taasisi za umma zilizoingiziwa uozo wa siasa chafu za ccm, ni pamoja na mahakama.

Kwa sasa kwenye kesi hii ya Mbowe ushahidi unazidi kukaa wazi, na bado kesi haijafika mwisho, lakini tayari majaji wawili wameshatoka, na huyu wa sasa amejaa maamuzi ya utata, na sidhani kama atafika mwisho wa kesi.

Kubwa kuliko yote ni mahakama kutumika kuvujisha nyaraka kwa mashahidi wa jamuhuri kinyume kabisa cha sheria, na utawala wa mahakama uko kimya kuhusu hilo! Iwapo mahakamani ndio sehemu tunaambiwa ni ya kupatia haki, na inatakiwa tuiamini kuwa itatenda haki, wanashirikiana na watu waliobambikizia kesi, ni taasisi ipi tena ya umma inaweza kuaminika?

Kwa hapa tulipofikia ni kwa jinsi gani tunaweza kukwepa katiba mpya, wakati hadi mahakama imekubali kutumikia siasa chafu za CCM?
Tumekwama
 
Tumeshawazoea nyinyi nyumbu! Alipofungwa Sabaya mkasema Mahakama imetenda haki ila kwa huyu Gaidi mkubwa mnabwabwaja tuuu. Tulie dawa iwaingie sawasawa ili mpone ugonjwa wenu wa kinyumbu!!
Hujui kwamba Sabaya anafungwa kwa kuwatukana na kuwadharau baadhi ya vigogo wa jeshi la polisi na hata mawaziri na aliyekuwa makamu wa rais wakati huo pamoja na waziri mkuu? Kosa lake hakujua kwamba JPM angekufa sikumoja na ndio maana alilia kama mtoto. Vinginevyo Sabaya angelikuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wakati huu.
 
Tumeshawazoea nyinyi nyumbu! Alipofungwa Sabaya mkasema Mahakama imetenda haki ila kwa huyu Gaidi mkubwa mnabwabwaja tuuu. Tulie dawa iwaingie sawasawa ili mpone ugonjwa wenu wa kinyumbu!!
Ikitenda haki mahakama moja, haimaanishi na nyingine zimetenda haki kwa hii moja kufanya hivyo..!!! Kila mahakama inajitegemea kwenye utendaji na maamuzi.. Maamuzi ya kesi moja yanaweza yasifanane na nyingine..!! Na ndiyo maana wengine huwa wanahukumiwa hivi, lakini wakikata rufaa hukumu hubadirika..
 
Tumeshawazoea nyinyi nyumbu! Alipofungwa Sabaya mkasema Mahakama imetenda haki ila kwa huyu Gaidi mkubwa mnabwabwaja tuuu. Tulie dawa iwaingie sawasawa ili mpone ugonjwa wenu wa kinyumbu!!
Twambieni nani aliingia kwenye stoo/masijala ya Mahakama na kuiba ile nyaraka na kuwapelekea washitaki wa Mbowe? Funguo za hicho chumba walipata wapi? Kila mahakama ina mkubwa wake. Awajibike kwa kosa hilo la wizi wa Nyaraka na kuwapelekea polisi wanaomshitaki Mbowe, eti alitaka kumdhuru Sabaya
 
Back
Top Bottom