Kwa kilichotokea na kuendelea pale Rocky City Mall ni hujuma dhidi ya Rais Samia lakini CCM mmechokwa

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,500
2,000
Kama Mada inavyojieleza juzi tu hapa machinga wamefurumshwa mjini kati, Jana wakaandamana, Leo usiku huu rocky City mall inaungua hasa sehemu ya kuchezea watoto

CCM hamjawahi kushinda uchaguzi, halafu mwenda zake aliwakingia kifua machinga nchi nzima wakafanya biashara wanapotaka Leo hii wanatimuliwa

Kinachoendelea Mwanza ni hujuma dhidi ya Rais na CCM yake .
 
Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
6,732
2,000
Mafisadi papa wamenunua mahakama, bunge, nk ila kamwe hamtaweza kununua nguvu ya umma! Buhongwa dampo ndio sehemu ya kuweka machinga, kweli?

Hata lile wazo la kwamba angalau baadhi ya barabara katikati ya mji ziwe zinafungwa angalau kuanzia saa kumi jioni ili kuwapa nafasi hawa akina mama wauze tembele na dagaa zao mkaona halifai kisa ni JPM alisema,
Endeleeni kuwasikiliza akina Vick Kamata tuone mtafika wapi!
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,901
2,000
Hapana.

Mada haijielezi, na jinsi unavyoiweka wewe ni dhahiri hamuwezi kufika mbali kwa namna hii.

Kupiga kiberiti Rock City Mall hakumhujumu Rais Samia, kitendo hicho ni kuwahujumu wananchi wote wa Mwanza.

Unaposema "...mwenda zake aliwakingia kifua machinga nchi nzima, wakafanya biashara wanapotaka." Wewe unadhani njia hiyo ndiyo sahihi ya kuondoa matatizo, siyo ya machinga pekee bali ya jamii kwa ujumla?

Uliwahi kuona wapi, nchi gani inayofanya shughuli zake kwa vurugu namna hiyo, nje ya taratibu!

Juzi juzi hapa ulikuja na mada ya vitisho kama hii humu humu JF, tukakukemea, bado hujifunzi jinsi ya kutetea hoja zenu ziweze kuwavuta hata wasiokuwa upande wenu?

Haya unayodhani ndiyo njia ya kuwapeleka mbele, ni kinyume kabisa. Husaidii agenda ya Machinga wa Mwanza, bali unaibomoa.

Sasa hapa usidhani nawatetea CCM au viongozi wake walioshindwa kutafuta njia bora za kuwasaidia wananchi wake kama hawa Machinga. Ninachokataa ni namna shughuli hiyo inavyoendeshwa, na nina hakika kuna njia bora zaidi za kuwasaidia Machinga kuliko inavyofanyika sasa.

Lakini sikubaliani kabisa na mwelekeo wa mawazo yako.
 
Townchild

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
7,545
2,000
Kama Mada inavyojieleza juzi tu hapa machinga wamefurumshwa mjini kati,Jana wakaandamana,Leo usiku huu rocky City mall inaungua hasa sehemu ya kuchezea watoto

CCM hamjawahi kushinda uchaguzi,halafu mwenda zake aliwakingia kifua machinga nchi nzima wakafanya biashara wanapotaka Leo hii wanatimuliwa

Kinachoendelea Mwanza ni hujuma dhidi ya rais na CCm yake .
Nyikani Kuna mambo mengi sana, fisi kumhujumu fisi hakuna fisi wa kumhoji mwenzie zaidi naye atashiriki au akiwa ameshiba atakaa pembeni kama hajaona na haoni kitu. 🐆🐅 .
 
christeve88

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
1,375
2,000
Nawaonea huruma sna wale wamama wauza mbogamboga na mahindi ambao wteja wao wakubwa tulikuwa ni sisi wpita njia. Sasa leo humpeleke mtu Buhongwa itakuwa vip? yaani mimi nifunge safiri kwenda Buhongwa kununua muhindi wa kuchoma. Naona ugumu wa maisha ukiwazidia hawa wa mama ambao wengi wao wana mikopo.
 
Waonee hurhma kanunue mahindi ya kuchoma hukohuko Buhongwa.
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
5,213
2,000
Kama Mada inavyojieleza juzi tu hapa machinga wamefurumshwa mjini kati,Jana wakaandamana,Leo usiku huu rocky City mall inaungua hasa sehemu ya kuchezea watoto

CCM hamjawahi kushinda uchaguzi,halafu mwenda zake aliwakingia kifua machinga nchi nzima wakafanya biashara wanapotaka Leo hii wanatimuliwa

Kinachoendelea Mwanza ni hujuma dhidi ya rais na CCm yake .

E9822DCA-38F1-40A7-9060-4E97EDBFA359.jpeg
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
9,038
2,000
Kama Mada inavyojieleza juzi tu hapa machinga wamefurumshwa mjini kati,Jana wakaandamana,Leo usiku huu rocky City mall inaungua hasa sehemu ya kuchezea watoto

CCM hamjawahi kushinda uchaguzi,halafu mwenda zake aliwakingia kifua machinga nchi nzima wakafanya biashara wanapotaka Leo hii wanatimuliwa

Kinachoendelea Mwanza ni hujuma dhidi ya rais na CCm yake .
Kanda ya ziwa tumemkataa Samia na serikali yake, wanayofanya sio haki kwa watanzania. Tutainyanyua CHADEMA mpaka ccm wajute.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom