Kwa Kijana yeyote mwenye uhitaji wa kazi hii tafadhali nicheki

King Loto

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
1,573
1,344
Okay Kwema Wakuu Mi ninacho amini hali zetu haziko sawa katika haya maisha na wapo tuliotoka familia duni au tunaishi kwa rafiki au hata ndugu kwa masimango na manyanyaso makubwa.

Mbali zaidi wapo wanaotakwa Kingono ili wapewe kazi kwa hawa kina dada zetu na kina kaka siku hizi japo kwa uchache mtu sawa na mama yako anaweza kukutaka umridhishe haja yake, .........hii hutokea kwa house boy, wachoma chipsi mtaani, na wafanya usafi wa bustani. (Mambo yote haya hayapendezi na hayana heri) japo mara chache unaeza bahatika kupata mwajiri au kiongozi muelewa uwapo kazini kwako.

Wanajukwaa nisiandike sana wacha nilenge kilichonileta hapa.

Mimi ninatafuta kijana wa kazi ya kuuza vinywaji aina ya vilevi na visivyo vilevi yaani ( Bar/ Grocery attendant), nafasi moja (1)
eneo la kazi ni Moshi Kilimanjaro.

Sifa zake
1. jinsia yoyote ilimradi awe tayari kukubali mazingira ya kazi.

2. Umri wake awe na angalau miaka 18+ na asizidi miaka 40.( Awe kijana).

3. Ningependelea awe mkaaji wa Moshi, Boma Ng'ombe, Arusha, Tanga, Babati, Karatu, Singida, Same, na Mwanga.

4. Awe wazi kueleza aliwahi kuwajibika na kazi zipi huko nyuma kabla ya kupatiwa hii hapa.

5.Malazi (sehemu pakulala) nitampa mimi pamoja na Chakula.

6. Asiwe mtumiaji wa Kilevi cha aina yoyote au awe mnywaji lakini asiyekunywa kupindukia kiasi.

7. Awe ni mtu wa Kauli kwa kila mteja.

8. Awe mvumilivu na asiyejibizana na wateja (awe msikivu).

Nipo tayari kumsaidia yeyote bila kuangalia jinsia kama ni kijana wakiume tutafanya kazi vizuri tu, kama ni wakike vile vile maana hapa kuna harakati nyingi na kazi zitaongezeka kila siku zinavyo kuja.

Malipo ya Kazi.
Malipo huwa tunalipana kwa kamisheni (Jinsi mauzo yatavyo kuwa yamefanyika). Sitakuwa na mshahara wa mwezi.

Kwenye PM yako nitaomba kama unaweza kuniandikia vitu hivi, basi andika
1. Majina yako.
2. Unaishi wapi kwa sasa.
3. Umri wako pamoja na jinsia yako.
4. Kazi yako kwa sasa kama huna sema sina.
6. Una wazazi au huna.
7. Unataka mshahara wa kiasi gani?(siyo lazima useme).
8.Andika wewe ni mwenyeji wa wapi?
Taarifa hizi ukinipatia zinanisaidia mimi nisiulize maswali mengi kuhusu wewe unayeomba kazi.

Karibu PM kama una huhitaji wa kufanya kazi hii, If interested PM King Loto
 
Yaani bar maid unaweka masharti kama bonge la ofisi vile kuliko hata TRA ,
😅😅😅 Yaani nimecheka kwanza maana vitu vinavyo kosa misingi ndiyo hivi vinafanyika kwa mazoea kila siku na maisha yanakuwa haya haya ya buku jero tu mkuu. Sasa mkuu hata hii kazi lazima ipewe misingi vile vile na ikipewa nafasi lazima wateja waje na wakae attention.

Mtu anatoa pesa yake ajue na kesho anakuja tena siyo mtu anatoa pesa afu zero services hapa ndiyo wabongo tunafeligi hata hawa watalii tunawapotezaga hivi hivi kesho wanaenda south africa na Egypt ambako wako serious kwa kila kitu.
 
Okay Kwema Wakuu Mi ninacho amini hali zetu haziko sawa katika haya maisha na wapo tuliotoka familia duni au tunaishi kwa rafiki au hata ndugu kwa masimango na manyanyaso makubwa...
Nimekupata ni kweli kuna tatizo la ajira nchini ila ni zile rasmi,mtu akiamua kuwa house girl kesho tu anapata kazi,mtu akiamua kuwa bar maid kesho tu anaanza, soko lao ni kubwa na nyeti ukimuwekea masharti anakimbia, hawakosagi kazi hao
 
Nimekupata,ni kweli kuna tatizo la ajira nchini ila ni zile rasmi,mtu akiamua kuwa house girl kesho tu anapata kazi,mtu akiamua kuwa bar maid kesho tu anaanza,soko lao ni kubwa na nyeti ukimuwekea masharti anakimbia,hawakosagi kazi hao
Kama unaijua hii kazi ya bar sio rahisi kama unavyodhani, kupata wafanyakazi wa bar wachapakazi nawaaminifu ni kazi sana.

Tatizo asilia mubwa ya wanaofanya kazi hii wametoka iadha mazingira magumu ya kifamilia au wameshindwa kuishi maisha ya malezi ya kifamilia so kudilinao no kazi kubwa sana.
 
Kama unaijua hii kazi ya bar sio rahisi kama unavyodhani, kupata wafanyakazi wa bar wachapakazi nawaaminifu ni kazi sana.

Tatizo asilia mubwa ya wanaofanya kazi hii wametoka iadha mazingira magumu ya kifamilia au wameshindwa kuishi maisha ya malezi ya kifamilia so kudilinao no kazi kubwa sana.
Nashukuru kwa kumwelewesha jamaa...
 
Mkuu punguza masharti
Mkuu walevi hatutakagi hivyo vigezo vyote awe mwenye t.ako, sura hata mbuzi anayo. Nakuhakikishia Bar yako itapata jina by default.
 
Naitaka hiyo kazi hata sasa ....Niko dar hapa nataka kuelekea mwanza nikaanze maisha sina kazi wala makaazi so am willing nishirikiane na ww ...illa ningependelea kufanyia kazi like Moshi au mwanza
 
Naitaka hiyo kazi hata sasa ....Niko dar hapa nataka kuelekea mwanza nikaanze maisha sina kazi wala makaazi so am willing nishirikiane na ww ...illa ningependelea kufanyia kazi like Moshi au mwanza
Fuata maelekezo kaka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom