Kwa kigezo cha umri huu naweza kujiunga JKT?

wewe ni Mbwa mzee hautaweza kushika mafunzo.

Hivo vigezo hapo vinakwaje?
Masharti ya kijana wa kujitolea kwa ajili ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa

1.Awe raia wa Tanzania

2.Awe na Umri kati ya miaka 18-23

3.Awe amemaliza darasa la saba na kuendelea

4.Asiwe ameoa au kuolewa na asiwe na mtu yeyote anayemtegemea

5.Awe tayari kufuata sheria zote za kijeshi zitazokuwa juu yake wakati akiwa jeshini(kutoroka,wizi,ulevi,uvutaji bangi, madawa ya kulevya na upatikanaji wa mimba n.k) Jeshini ni makosa makubwa na utaweza kushtakiwa na kufutiwa mkataba na JKT

6.Awe tayari kurudi nyumbani baada ya kumaliza mkataba wake na Jeshi la Kujenga Taifa

7.Awe na tabia na mwenendo mzuri

Masharti ya kijana wa mujibu wa sheria kwa ajili ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa

1.Awe raia wa Tanzania

2.Awe na Umri kati ya miaka 18-35

3.Awe amemaliza kidato cha sita na kuendelea

4.Awe tayari kufuata sheria zote za kijeshi zitazokuwa juu yake wakati akiwa jeshini(Uvutaji bang, madawa ya kulevya na upatikanaji wa mimba atashitakiwa na kufutiwa mkataba na JKT

5.Utoro haukubaliki na kosa la utoro mkataba utasogezwa mbele

6.Awe na tabia na mwenendo mzuri
 
Kuna kigezo hicho cha namba mbili miaka 18-23
Halafu kigezo hicho kingine cha namba mbili pia 18-35!
Fafanueni
 
5.Utoro haukubaliki na kosa la utoro mkataba utasogezwa mbele.
Yaani mkataba kusogezwa mbele ni kama adhabu? au kiaje hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom