Kwa kidato cha nne mtakaofanya mtihani Oktoba, ukienda diploma za ufundi umeumia

Lambert Mende

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
210
43
Napenda kuwashauri tena na tena vijana walioko kidato cha nne na ambao wanategemea kufanya mtihani wa kidato cha nne mwezi Oktoba, wakati wa kuchagua nafasi za kuendelea na masomo yao, wawe makini sana, kwenda kidato cha sita ndio njia rahisi ya kuweza kusoma elimu ya juu.

Kama una ufaulu mzuri kabisa wa kidato cha nne,nenda kasome kidato cha tano na sita, kupata daraja la pili kwa kozi za uhandisi kwa level ya diploma ni ngumu kidogo,pambaneni mpate nafasi za kidato cha tano, wenzenu wanalalamika sana kutokana na mabadiliko yaliyotokea mwaka huu.
 
Those who can't do something, should not interrupt those who can do those things.

Kama hawakiwezi wao, haimaanishi na wengine watakishindwa kukiweza!

Usikatishe vijana tamaa! Je ikitokea wakishindwa kwenye F5 unataka wakajiunge na vikundi vya kucheza SINGELI?
Mkuu @liliwayne
Tunawasaidia vijana,elimu ndio kila kitu, huku kimeshabana na uwezekano wa kupata hayo madaraja ni Mdgo sana,njia sahihi ni huko kidato cha tano.
 
Wakikosa huko wafanyeje? Wakae tu Nyumbani.

Nadhani unajua kabisa kuwa huko ndiko kuliko kimbilia la Vijana wengi washindwao kwenda F5.
 
Napenda kuwashauri tena na tena vijana walioko kidato cha nne na ambao wanategemea kufanya mtihani wa kidato cha nne mwezi oktoba,wakati wa kuchagua nafasi za kuendelea na masomo yao,wawe makini sana,kwenda kidato cha sita ndio njia pekee ya kuweza kusoma elimu ya juu,ukitaka kuzika ndoto zako za kusoma elimu ya juu nenda kasome vyuo vya ufundi,kupata daraja la pili kwa kozi za uhandisi kwa level ya diploma ni ngumu sana,pambaneni mpate nafasi za kidato cha tano,wenzenu wanalia vibaya sana na hawajui nani atawasaidia.
Dah... hii ni kweli kabisa, ila mfumo huu siyo mzuri diploma miaka 3 wakati high school ni 2 tu.. halafu wote mnakutana chuo...:(:(
 
NACTE wanasimama wapi?au ndio wanakufa kimya kimya?maana wao ndio waliokuwa wasimamizi wakubwa wa vyuo vya ufundi,sasa kwa mtafaruku huu sijui nini kinaendelea.
 
Dah... mie nadhani wangekomaa kwa kuwatofautisha kwamba wale wanaopitia diploma basi wapewe B Eng na wale wa vidato wapewe B Sc na wasichanganywe kwenye masomo ili wale wanaopitia diploma wafaidike..
 
Tatizo ni serikali kutowajali maEngineer na Matechnician wenye diploma na vyeti. Kishahara yao ni midogo wakati hawa ndio watendaji wakuu kwenye kazi za kivitendo.
Hata kwenye ajira za serikali hawapewi sana kipao mbele au motisha. Matokeo yake kila mtu anakimbilia digrii hata kama hana uwezo wa kusoma sana elimu ya nadharia.
 
Napenda kuwashauri tena na tena vijana walioko kidato cha nne na ambao wanategemea kufanya mtihani wa kidato cha nne mwezi Oktoba, wakati wa kuchagua nafasi za kuendelea na masomo yao, wawe makini sana, kwenda kidato cha sita ndio njia pekee ya kuweza kusoma elimu ya juu.

Ukitaka kuzika ndoto zako za kusoma elimu ya juu nenda kasome vyuo vya ufundi, kupata daraja la pili kwa kozi za uhandisi kwa level ya diploma ni ngumu sana, pambaneni mpate nafasi za kidato cha tano, wenzenu wanalia vibaya sana na hawajui nani atawasaidia.
Bora waende uko rafiki yangu, ebu angalia Guide book 2016/2017 kwa watu wa science. Bila shaka utaona namna palivyo banwa. Lkn uko tyr mtu unakuwa professional sio vyeti tu bila skills.
 
Mkuu @liliwayne
Tunawasaidia vijana,elimu ndio kila kitu, huku kimeshabana na uwezekano wa kupata hayo madaraja ni Mdgo sana,njia sahihi ni huko kidato cha tano.
Kaiangalie Guide book 2016/2017 kwanza. Alaf ndo uje uongee ayo.
 
Napenda kuwashauri tena na tena vijana walioko kidato cha nne na ambao wanategemea kufanya mtihani wa kidato cha nne mwezi Oktoba, wakati wa kuchagua nafasi za kuendelea na masomo yao, wawe makini sana, kwenda kidato cha sita ndio njia rahisi ya kuweza kusoma elimu ya juu.

Kama una ufaulu mzuri kabisa wa kidato cha nne,nenda kasome kidato cha tano na sita, kupata daraja la pili kwa kozi za uhandisi kwa level ya diploma ni ngumu kidogo,pambaneni mpate nafasi za kidato cha tano, wenzenu wanalalamika sana kutokana na mabadiliko yaliyotokea mwaka huu.
unachosema ndugu kuna ukweli lkn mtu yeyote akitaka kupata GPA above 3.5 kwa diploma za engineering inawezekana vizuri tuu lkn kama ni arusha tech kwa civil wanabaniwa sana
 
Napenda kuwashauri tena na tena vijana walioko kidato cha nne na ambao wanategemea kufanya mtihani wa kidato cha nne mwezi Oktoba, wakati wa kuchagua nafasi za kuendelea na masomo yao, wawe makini sana, kwenda kidato cha sita ndio njia rahisi ya kuweza kusoma elimu ya juu.

Kama una ufaulu mzuri kabisa wa kidato cha nne,nenda kasome kidato cha tano na sita, kupata daraja la pili kwa kozi za uhandisi kwa level ya diploma ni ngumu kidogo,pambaneni mpate nafasi za kidato cha tano, wenzenu wanalalamika sana kutokana na mabadiliko yaliyotokea mwaka huu.
Mkuu hiyo mitihani inanzaa tarehe gani october?
 
Usiwatishe madogo,tech kawaida tu kuna watu hatujawah kukosa first class
 
Dah... ila kwa uchunguzi wangu mainjinia walipitia diploma huwa wanatisha sana kwenye fani :):)
 
Back
Top Bottom