Kwa Kibao hiki cha 'WAAH' chake Mwana Simba Mwenzangu Diamond akimshirikisha Koffi nasema 'Shikamoo' mno tu Kwake

Mzee wangu wewe lingala unaijua vyema kabisa, naamini viunga vyote umekanyaga tena na uhakika kuanzia beni, niania, mambasa , bangedaido, mavivi hadi kisangani kote umefika sasa mimi nilieishia fasi ya uvira tena kwa dakika moja nitaweza kweli kutafsiri?
 
Na nauhakika maniema yote umefika sasa unaleta utata wako tu, hapo ni sawa na unieleze sombe na makako wanaandaa vipi wakati sijui.
 
Huu Wimbo wa 'WAAH' ukiwa unapigwa au hata unausikiliza tu popote pale halafu huamki ama Kucheza tu au Kutikisika basi utakuwa na matatizo Kichwani au utakuwa ni mwana Yanga SC mwenye Roho Mbaya au utakuwa kati ya Team Kiba au Yule aliyetaka Kufa kwa Kuanguka kutoka katika Paa la Uwanja wa Mkapa Team Harmonize.

Leo natangaza rasmi kuwa Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinumz a.k.a Dangote na Koffi Olomide kampa a.k.a nyingine kwa kumuita Le Generale Dangote ni Habari nyingine kwa Kuimba vyema na kwa Ustadi wote kabisa hapa Afrika Mashariki, Afrika nzima, Duniani na pengine hata huko Mbinguni Kwake Maulana / Mola.

Huwezi Kumshirikisha Fundi na Gwiji la Muziki wa Dansi Afrika Koffi Charles Antoine Olomide a.k.a Le Grand Mopao a.k.a Boss ( Mokonzi ) ya Mboka halafu Nyimbo yako isiwe nzuri na tamu Kuisikiliza. Kupitia tu Video ya Wimbo huu mtamu wa 'WAAH' nimegundua kuwa Diamond ( Dangote ) ana Vipaji vingi na uwezo mkubwa wa Kucheza vyema na Sauti yake.

Namtakia Mafanikio mema zaidi katika Kazi yake ya Muziki Diamond Platinumz ( Chibu Dangote ) na popote alipo ajue GENTAMYCINE ninamkubali.
Umejaliwa kipaji cha kusifia
Yaani et mondi anaimba zaid ya walioko mbinguni
Kazi kweli kweli
 
Umejaliwa kipaji cha kusifia
Yaani et mondi anaimba zaid ya walioko mbinguni
Kazi kweli kweli

Kionjo cha WAAH , ni sebene laini ambayo kwa mpenda muziki lazima asifie, kama kionjo hichohicho alikisifu Franco toka miaka ya hiyo japo mwasisi wa kionjo hicho ni Henri Bowane wewe ni nani hadi upinge? Au haya basi tunasifia lake matadi ina maji meusi ili uridhike.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom