Kwa Kibao hiki cha 'WAAH' chake Mwana Simba Mwenzangu Diamond akimshirikisha Koffi nasema 'Shikamoo' mno tu Kwake

Poisonous

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,477
2,000
Huu Wimbo wa 'WAAH' ukiwa unapigwa au hata unausikiliza tu popote pale halafu huamki ama Kucheza tu au Kutikisika basi utakuwa na matatizo Kichwani au utakuwa ni mwana Yanga SC mwenye Roho Mbaya au utakuwa kati ya Team Kiba au Yule aliyetaka Kufa kwa Kuanguka kutoka katika Paa la Uwanja wa Mkapa Team Harmonize.

Leo natangaza rasmi kuwa Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinumz a.k.a Dangote na Koffi Olomide kampa a.k.a nyingine kwa kumuita Le Generale Dangote ni Habari nyingine kwa Kuimba vyema na kwa Ustadi wote kabisa hapa Afrika Mashariki, Afrika nzima, Duniani na pengine hata huko Mbinguni Kwake Maulana / Mola.

Huwezi Kumshirikisha Fundi na Gwiji la Muziki wa Dansi Afrika Koffi Charles Antoine Olomide a.k.a Le Grand Mopao a.k.a Boss ( Mokonzi ) ya Mboka halafu Nyimbo yako isiwe nzuri na tamu Kuisikiliza. Kupitia tu Video ya Wimbo huu mtamu wa 'WAAH' nimegundua kuwa Diamond ( Dangote ) ana Vipaji vingi na uwezo mkubwa wa Kucheza vyema na Sauti yake.

Namtakia Mafanikio mema zaidi katika Kazi yake ya Muziki Diamond Platinumz ( Chibu Dangote ) na popote alipo ajue GENTAMYCINE ninamkubali.
 

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
5,247
2,000
Mboka inamaanisha nini?

MBOKA ina maana ya Nchi ina maana ukisema Boss ya Mboka ni kama tajiri wa nchi.
MOKONZI ina maana ya kiongozi au mtu muzito
MOPAO ina maana ya Mwenyeji au mzaliwa
Na maneno yote hayo ni maneno ya kujipa sifa hasa watu wanaohesabhia makuta ya mingi
 

Poisonous

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,477
2,000
MBOKA ina maana ya Nchi ina maana ukisema Boss ya Mboka ni kama tajiri wa nchi.
MOKONZI ina maana ya kiongozi au mtu muzito
MOPAO ina maana ya Mwenyeji au mzaliwa
Na maneno yote hayo ni maneno ya kujipa sifa hasa watu wanaohesabhia makuta ya mingi
Nitaomba pia na maana ya maneno haya yafuatayo tafadhali....

Mareshale Mukulu
Papa Cherie
Lonkia Milo Dan Koko
Souverain Premier
De La Patria
Mukulu ya Bamukulu
Mokonzi ya Fikin
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom