Kwa kesi hii ya ugaidi ya akina Mbowe: Je, Kitengo cha propaganda ndani ya Serikali wamefaulu au wamefeli?

Kumbe kazi ya TISS ni kufanya Propaganda? Yawezekana basi hata CIA nao kazi yao Kubwa huko Marekani ni Kufanya tu Propaganda.

Kazi kweli kweli.....!!
Kumbe hujui kazi ya CIA, umesahau propaganda za Sadamu kumiliki WMD zilienezwa na nani.
 
Binafsi hakuna propaganda ninazoziogopa kama zinazoweza kuleta madhara kwa umma siku za mbelen
Mfano propaganda ya #Babu wa Loliondo,ilifumwa ili kuinusuru serikali ya wakati huo kwenye makashfa ya Richmond na EPA yaliyokuwa yametanda anga zima la siasa za Tanzania.

Lakini matokea tuliyaona,serikali ilifanikiwa kuhamisha goli lakini mamia ya wananchi wakapoteza uhai kwa kuamini dawa isiyokuwa na uthibisho wa kikemia na kuacha matibabu yao!!!!.
Kumbe hii nayo ilikuwa propaganda??
 
mi nasemaga Raisi pekee aliyeweza kumudu siasa za ushindani ni JK hawa wengine wanachojua ni kutumia dola sasa tatizo nyakati zinabadilika saahivi kuna mtandao watu wanapata na kutoa taarifa kwa haraka na kwa wepesi sana, matokeo take ndio hivi kuvuliwa shungi mbele ya mkweo
 
Lowasa anakuja chadema ni asset au liability ....hapo ndipo aliamua kusimamia analolijua Hadi Leo kwakweli mhuuuu
Ukweli mchungu ni kwamba kwa wagombea urais from opposition tokea mfumo wa vyama vingi uanze kuna aliyewahi kupata kura nyingi na wabunge wengi kumzidi Lowasa??
 
Ndugu wana jukwaa, kwenye kichwa cha habari hilo ni swali, hivyo katika kutoa hoja naomba kwanza tutangulize kwanza kujibu na baadae ndio zifuatie hoja za uchambuzi.

Katika maswala mazima ya mifumo ya kiutawala katika nchi za Kiafrika, hili neno la propanda linapewa kipaumbele kikubwa pindi inapojitokeza mihemko ya jamii ya watawaliwa, na idara maalum zinazohusika na mipango hii ya propaganda hukaa chini na kuibua jambo litakalokuwa midomoni mwa wananchi na kwenye vyombo vyote vya habari kwa wakati huo, dhamira kuu ni kuiacha serikali ipumue dhidi ya masimango na maneno kutoka kwenye jamii kwa wakati huo!

Nije kwenye kiini cha mada,kwa mtazamo wangu mimi, hili swala la serikali kumtia nguvuni mwenyekiti wa Chadema Bw. Mbowe na kumpandisha kizimbani na watuhumiwa wengine katika makosa ya ugaidi, serikali kwa ujumla imejaribu kuhamisha goli ili wanaoshambulia wakose muelekeo.

Sote tunajua, baada ya kukamata usukani wa madaraka Rais Samia, kipaumbele chake chake cha kwanza mkononi kilikua ni kuirudisha Tanzania kwenye nafasi yake katika ramani ya Kidemokrasia ulimwenguni.Na matamshi yake akauthibitishia ulimwengu kwamba yale mambo yote yasiyokuwa ya kiungwana katika utawala wake hayatakuwepo.

Hapa sasa,kiujumla hadi mwenda zake anatangulia mbele ya haki, uwanja wa demokrasia nchini ulishajaa tope na vyama vya upinzani vilikua hoi bin taabani.Miongoni mwetu watanzania wa kawaida hakuna asie fahamu hilo.

Hivyo basi upinzani upinzani ukajaribu kusuka ajenda kuu itayowapa kick ili kutembelea nyota ya Samia na kurudisha umaruufu wao uliopokonywa kwa mabavu, na katika kuzichanga karata zao wakaona ajenda namba moja ni katiba mpya.

Wakaanza kuliamsha dude nchi nzima tena kwa spidi kubwa huku wakijaribu kuwatumia hadi watu mbalimbali wenye ushawishi kwa jamii ili kupata attention. Na serikali kadri ilivyojaribu kutumia maneno ya hekima na busara ili waachane na jambo hilo,ndio kwanza wakazidi kupata kick.

Hapo ndio serikali ikaamua kuwakabidhi jukumu watu wa kitengo ili kuhamisha goli la mjadala huo waliokuwa nao wapinzani.

Na watu wakainama, wakainuka na wakaamua kufukua makaburi kwa kuirudisha tena ubaoni kesi ya ugaidi ambayo kwa maneno ya ndani inasemekana, walishaichumbua na kujiridhisha kwamba haina ukweli.

Na baada ya Bw. Mbowe kupandishwa kizimbani hatimaye lengo lao limetimia kwani upande wote wa upinzani umeshatawanyika na wanahaha na kesi ya mwenyekiti.
Hoja ya bandiko lako ni nini? Bandiko hili halieleweki unachotaka tukijadili, andika upya labda utapatia.
 
Kesi ya Mbowe ipo toka mwaka jana. Leta mada nyingine.
 
Propaganda zingine humaliza na kuwaabisha wapishi wake kama hii dhidi ya mbowe
 
Kumbe kazi ya TISS ni kufanya Propaganda? Yawezekana basi hata CIA nao kazi yao Kubwa huko Marekani ni Kufanya tu Propaganda.

Kazi kweli kweli.....!!
Kiongozi GENTAMYCINE,kwa nchi za kiafrika idara za usalama ndio nguzo kuu za watawala,kwa yale mema na hata mabaya.Je unafahamu kwamba nyuma ya pazia wengi waliopangwa kusimamia kesi hii kuanzia mahakamani hadi upande wa mashtaka ni watu wa kitengo?.
 
Kumbe hii nayo ilikuwa propaganda??
Ndio kiongozi,watu wa ndani kabisa wa serikali walikua wanafahamu kwamba kikombe cha babu hakina nguvu wala uwezo wowote wa kuponya maradhi sugu ya wananchi.Lakini kwa kuwa ulikuwa mpango mkakati basi ndio kwanza waliongoza misafara kwenda Loliondo!!.Lakini matokeo tuliyaona.
 
Nifikiriavyo mimi ameamua kumfedhehesha mbowe kwa inferiority aliyonayo ktk uchaguzi ujao, imagine hata jaji anashindwa kuficha mahaba yake juu ya upande wa mashtaka.

Chief hangaya ana roho mbaya sana ugaidi wa kufadhiliwa na laki na nusu, mara laki mbili! Na bastola moja yenye risasi tatu! Bastola ambayo mama mbege anaielezea kuifahamh vizuri utafikiri anaimiliki!
Propaganda hazijawahi kufanikiwa zaidi ya kuivuruga Taifa. Ndicho kina chotokea katika kesi hii ya hovyo kuwahi kutokea Tanzania. Ni aibu, ni aibu na ni aibu sana kwa Mama Samia na Serikali yake.
 
Back
Top Bottom