Kwa kauli za huyu Mbunge wa Upinzani nakiomba sasa chama chake kianze kujiandaa kisaikolojia kwa Maumivu!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,848
2,000
Ni Mbunge ambaye kwa Wiki hii ya Pili sasa amekuwa akionyesha ' Ukomavu ' wake Kisiasa lakini ' Ucha Mungu ' mkubwa uliojawa na Hekima hadi Busara kwa upande Watendaji wa Chama Tawala ( sasa Wastaafu ) Lakini kama hiyo haitoshi kwa Kauli zake za Leo Bungeni ni kama ameshajua hatorejea tena Bungeni ila kwa anavyopendwa huko kama akihamia CCM ataendelea kuwa Mbunge.

Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwamba kwa takribani miezi Miwili nimeweza kutembelea Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kama ya Mbeya, Katavi, Iringa, Rukwa na Njombe ila GENTAMYCINE sijawahi kuvutiwa na Mji mzuri kama wa Iringa Mjini ambao kiukweli umejengeka vyema kabisa kuliko hiyo Miji mingine. Nikipata tena Nauli ni lazima tu nitarejea tena hapo Iringa Mjini nimepapenda.

Niliwahi Kukutana na Mwanasaikolojia Mmoja ' Mahiri ' sana ambapo katika Mazungumzo yetu nakumbuka aliwahi Kuniambia GENTAMYCINE kuwa Siku zote hata kama ukiwa na Uadui na Familia fulani lakini kama hiyo Familia imeoa Kwenu au mmeoa Kwao hapo inakuwa ni Kiini Macho tu na kwamba muda wowote ' Uhusiano ' huo utakuja Kuwaunganisha na mtakuwa pamoja tu daima.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
1,135
2,000
Sasa hapo atajiunga kwasababu ya mapenzi yake kwa chama kipya, au atajiunga kwasababu kaoa huko?!

Halafu ikitokea hivyo, itaonekana dhahiri ni shinikizo tu toka sehemu fulani, lilianza wakati ule walipokuwa lupango na wenzake, maana alichangiwa yeye atoke lupango, wenzie wakaachwa.
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,603
2,000
Ni Msigwa! By the way Msigwa, Kubenea wataenda ccm hao wanajulikana!

Waende waunge juhudi ila watakao baki upinzani ndio wanaume, mwanaume halisi huwezi kupewa ahadi na kutongozwa kama demu ni upumbavu!

Hata kama sehemu ina matatizo unatakiwa ujiuzulu kabisa na kusitaafu siasa watu tutakuelewa ila kulia na kuomba cheo cha kufagia kwenye chama cha kihuni kama ccm ni upumbavu.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
1,135
2,000
Ni Msigwa! By the way Msigwa, Kubenea wataenda ccm hao wanajulikana!

Waende waunge juhudi ila watakao baki upinzani ndio wanaume, mwanaume halisi huwezi kupewa ahadi na kutongozwa kama demu ni upumbavu!

hata kama sehemu ina matatizo unatakiwa ujiuzulu kabisa na kusitaafu siasa watu tutakuelewa ila kulia na kuomba cheo cha kufagia kwenye chama cha kihuni kama ccm ni upumbavu.
Akifanya hivyo nitamshangaa sana, hasa nikikumbuka ule msimamo wake siku kamkimbia Polepole kule Segerea...
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,028
2,000
Mkuu Genta, umerahisisha sana zoezi la utambuzi la huyu kamanda. Ni vyema wao waonao na kusikia kwa umakini wajiandae kwa lolote lile linaloweza kutokea.
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
3,621
2,000
Wewe unashindwa kuelewa kiswahili, Halafu unaanzisha uzi wa vita za kiuchumi

Kwa umbumbu huo na ujinga huo Hakika wewe ni mpiga tarumbeta

Soma vizuri au mpigie simu mwalimu wako wa Fasihi atakueleza
Sina muda wakubisha na vibinti vya ngomani mimi,humu mambo huwekwa wazi mambo ya mmu haya ya codes
 

lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,753
2,000
Hii mada haina tofauti na kubeba matikiti, mipotopoto na mawese kwenda kupima koona
 

mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
7,218
2,000
Ni Msigwa! By the way Msigwa, Kubenea wataenda ccm hao wanajulikana!

Waende waunge juhudi ila watakao baki upinzani ndio wanaume, mwanaume halisi huwezi kupewa ahadi na kutongozwa kama demu ni upumbavu!

Hata kama sehemu ina matatizo unatakiwa ujiuzulu kabisa na kusitaafu siasa watu tutakuelewa ila kulia na kuomba cheo cha kufagia kwenye chama cha kihuni kama ccm ni upumbavu.
Labda hawa wataondoka kistaarabu hawatamtukana mbowe na chadema
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom