Kwa Kauli za Chuki za Mbunge Tarimba Abbas (CCM) dhidi ya Simba SC na TFF naiomba Simba SC iachane rasmi na SpotiPesa yake

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,350
2,000
"TFF ni Simba SC na Simba SC ni TFF na tumeshaona jinsi Simba SC inavyobebwa na TFF kiasi cha wengine Kuchoshwa na Upuuzi huu ", Mbunge wa Kinondoni Tarimba Abbas Tarimba.

Chanzo: Sports Court Wasafi FM leo.

Simba SC nadhani tumeshauvumilia huu unafiki uliopitiliza wa Mbunge wa Kinondoni Tarimba Abbas.

Tarimba Abbas (Mbunge wa Kinondoni) amesahau kuwa ni Simba SC pekee kwa hapa Tanzania na Afrika Mashariki ndiyo inaipa Mileage ya kutosha Kampuni yake ya Spoti Pesa na siyo Klabu yake inayochechemea ya Yanga.

Mimi kama GENTAMYCINE (Msaga Kunguni Mkuu na Mzee wa Nongwa JamiiForums nzima) nauomba upesi sana Uongozi wa Simba SC utafakari hili la huyu Mbunge Tarimba Abbas kwa Kina ila Simba SC ikisitisha Mkataba rasmi na Spoti Pesa ndiyo itakuwa Furaha yangu na atatia Adabu.

Kampuni za Kuidhamini Simba SC ni nyingi na tena Kubwa na zenye Financial Stability na Muscles kuliko hiyo Spoti Pesa yake. Kama Mbunge Tarimba Abbas anavyoichukia Simba SC na Mimi GENTAMYCINE simpendi vile vile. Ubaya Ubayani tu Kudadadeki.

Wallace Karia miaka Minne ( 4 ) tena kwani amefanya mengi na makubwa halafu anatosha vile vile. Tena napendekeza Wallace Karia atawale (aiongoze) TFF hii daima milele Amina au mpaka pale atakapochoka Yeye.
 

Chomo

Senior Member
Mar 29, 2017
157
500
unashaur waachane na udhamini wao,wewe unaweza kudhamini au kutafuta wengne..labda ukadhamini icho kichongeo chako hapo chini
 

Joo Wane

JF-Expert Member
Mar 14, 2007
736
1,000
Ni kweli kayatamka hayo maneno? Iwapo ni kweli kayatamka hayo maneno basi anapaswa aiombe radhi klabu ya Simba ili kuonyesha uungwana wake. Na uongozi wa Simba nitawashangaa sana kama watalikalia kimya suala hili. Na kwa maneno hayo tu hapaswi hata kugombea kwa sababu tayari ameshaonyesha chuki wazi wazi kwa Simba kitu ambacho sio sahihi. Maana yake yeye anataka kwenda kuwa raisi wa TFF ili aikomoe Simba basi hatufai.

Kwa sasa watu wanapambana ili Karia aondoke kwa sababu anaonekana ana upande halafu yeye tena anaanza kuonyesha upande wake hata kabla hajapitishwa. Ili mpira uendelee nchi hii na kuondoa manung'uniko TFF inatakiwa impate kiongozi makini kama alivyokuwa Leonard Tenga ambaye aliongoza mpira wa nchi hii bila kupendelea klabu yake anayoipend Yanga. Kwa kweli Tarimba yeye abaki huko huko bungeni huku kwenye mpira tunataka kiongozi safi asiyependelea upande anaoshabikia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom