Kinuju
JF-Expert Member
- Mar 20, 2021
- 2,390
- 5,310
Tangu aape kuwa Rais wa sita wa Tanzania ni kama hajui kuwa ilani ya CCM inataka Tanzania iwe ya viwanda mpaka kufikia mwaka 2025 ili kuongeza ajira na uzalishaji nchini.
Kwa sasa umeme unasuasua na kuongeza gharama za uzalishaji je nani ataanzisha kiwanda?
Ameruhusu ungizwaji wa bidhaa holela bila kulipiwa kodi, wafanyabiashara wakwepa kodi waliokuwa wanapitishia bidhaa zao bandari ya Zanzibar sasa hivi wamekimbilia bandari ya Dar es Salaam kwa sababu swala la kodi halitiliwi mkazo tena.
Bandari ya Zanzibar sasa hivi chini ya rais Mwinyi huwezi kupitisha bidhaa bila kulipa kodi ndiyo maana wamekimbilia huku bara.
Kauli ya Rais Samia kwamba Tanzania imefunguliwa na bidhaa mbalimbali ziingie tu kutoka kokote hailindi viwanda vya ndani na ni mwiba mchungu kwa waliojenga viwanda.
Ikumbukwe viwanda vilivyoachwa na Nyerere vilikufa baada ya Rais Mwinyi kusema sasa Tanzania ni ruksa kwa kila kitu.
Je, Rais Samia anafuata falsafa za mr ruksa?