Kwa kauli ya nassari inabidi chadema wasitishe kwanza sera yao ya majimbo otherwise itatucost.

nimetafakari kwa kina bado sijaona tatizo kwa kauli ya nassari, ikiwa kauli aliyotoa alikua kwy jukwaa ambapo munkari wake ukiwa juu we achaaaaaaaaaa tu.
 
Usitetee uozo hapa.Mtu kakosea lazima arekebishwe.Sasa wewe unatofauti gani na wanaccm wasiopenda kukosoana kwa maslahi yao.Ni wakati wa chadema kujitofautisha na ccm na wala sio kutetea utumbo.
nimetafakari kwa kina bado sijaona tatizo kwa kauli ya nassari, ikiwa kauli aliyotoa alikua kwy jukwaa ambapo munkari wake ukiwa juu we achaaaaaaaaaa tu.
 
Baada maelezo ya Nassari kupelekwa kwa (DPP) Nassari kaanza kuweweseka kwa kauli yake, anasema kasikitishwa sana na tafsiri potofu kuhusu kauli yake.

Anasema kauli yake kamwe haikulenga kuigawa nchi wala kumzuia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kikwete kufika Arusha.
 
Ndugu WanaJF,

swala la nasari kwa maono yangu nayachukulia ni mtaji wa Chadema tena mzuri tu.

1. PUBLICITY

katika hali ya kawaida CCM ilitakiwa iwaonyeshe watanzania kuwa chama chao kupitia serikali iliyopo madarakani kinawasikiliza wananchi ndio maana sasa wamebadilisha wawaziri(hata kama hoja ilianzishwa na wapinzani ni watanzania pia kwahiyo mesemo wa serikali sikivu ungekuwa wa kuweka ushawishi) na kuteua wakuu wa wilaya. jamabo la ajabu midomoni mwa makada wa CCM yanatoka maneno sita neno chadema manne yanaendelea kuilezea chadema.

Kwangu Nape anyokazi kubwa.

2. KUIMARISHA NGUVU YA UMA

Wakati CCM inaendelea na mtindo ulele ule wakushawishi dola ichukue hatua dhidi ya Chadema kwa kuonyesha imefanya jambo baya sana lisilokubalika, Chadema wao wanapita kwa wananchi na kuwaeleza shida wanazopata zinasababishwa na CCM na kuwapa matumaini ya kuwa wao ni mbadala hata kwa kukamatwa na kuwekwa rumande na ya kuwa wako tayari kwa hilo katika kutetea haki zao na sio kufumbia macho ufisadi.

Kwa stahili hii CCM haitawakonga moyo wananchi bali itazidi kuwasha moto.


3. HOJA NZURI KATIKA WAKATI USIO MWAFAKA

kutokana na ukweli kwamba asilimia kubwa ya watendaji wa serikali ni MAKADA WA CCM, watakapoendelea na makati huu wa kusimamia hoja isiyo na mashiko wala tija kwa taifa ni wazi makada hawa nao watalazimika kusimamia kauli za viongozi wao. hali hii itasababisha utendaji kuzorota na matokeo yake ni maisha kuendelea kuwa magumu na kwa hali hii mwananchi hatahitaji lolote kutoka kwa kada wa serikali iliyopo madarakani zaidi ya wanatatuaje matatizo yanayoendelea kuwakabili.

Wana CCM wakati umefika wa kuchagua viongozi wenu wanaojua siasa za ulimwengu wa leo.


nawakilisha, kupinga kwa hoja ni sawa.

Hapa hakuna wa kupinga maana ukweli ndio huo, CDM kazeni uzi endelea kutujuza yale yaliyofichwa na CCM
 
Nassari amepata publicity ya hali ya juu na CCM wasichokijua ni kwamba wanampaisha huyu jamaa kwenye anga za kisiasa vibaya mno kauli yake imeshazubgumzwa na wanasiasa na wananchi wengi kwa nyakati tofauti kutoka maeneo tofauti nimeshasema mara nyingi Strategist party wa CCM mukichwa hamna kitu haoni hii nguvu inayowekwa na CCM kumnanga Nassari ndio inafanya watu wengi watake kumfahamu na chama chake
 
nimetafakari kwa kina bado sijaona tatizo kwa kauli ya nassari, ikiwa kauli aliyotoa alikua kwy jukwaa ambapo munkari wake ukiwa juu we achaaaaaaaaaa tu.
shule ya vidudu hujamaliza unakimbilia mijadala ya kaka zako waliomaliza vyuo vikuu kwa degree kibao..!
Ona sasa ulivo weak na brain yako mbumbumbu..!
 
Nassari amepata publicity ya hali ya juu na CCM wasichokijua ni kwamba wanampaisha huyu jamaa kwenye anga za kisiasa vibaya mno kauli yake imeshazubgumzwa na wanasiasa na wananchi wengi kwa nyakati tofauti kutoka maeneo tofauti nimeshasema mara nyingi Strategist party wa CCM mukichwa hamna kitu haoni hii nguvu inayowekwa na CCM kumnanga Nassari ndio inafanya watu wengi watake kumfahamu na chama chake
Mkuu Froida umesema kitu ambacho huwa nakisema kila wakati, ma strategist wa CCM huwa wanaenda na matukio hawaangalii impact ya muda mrefu. Mfano mdogo ni tarehe ya hukumu ya Lema ambayo ilipangwa makusudi haikupangwa kwa bahati mbaya lengo lilikuwa ku neutralize sherehe za ushindi wa AR lakini sasa wanajuta.

Leo wanahangaika na Nassari the event which they didn't plan before, wanampandisha chart kuishusha itakuwa kazi kama wanavyohangaika kuishusha ya Zitto na Lema. Wanaandamana kuitangaza CDM. Wakati wao wakihangaika na Nassari CDM wao wanafanya mikutano ya kuimarisha chama, can't you see the difference.

Another thing angalia hata humu JF, basically kuna makundi makubwa mawili hayajifichi pro CCM na pro CDM. Mara nyingi Pro CDM huwa wanaleta matukio ya chama chao kama mikutano, picha nk, wakati huo pro CCM kazi yao ni ku play down habari za CDM bila wao kuleta habari za CCM. Kinachotokea ni kuzidi kuitangaza CDM humu JF. Ukienda kwenye mitandao ya Kenya ya siasa utafurahi, kama FORD-Kenya wakileta picha, FORD-Asili nao wanaleta za kwao, KANU nao wanaleta za kwao na wanaenda hivyo kwa matukio yote. Hapa ni different pro CCM wao wanasubiri pro-CDM waseme madiwani watano wamehama CCM ndipo pro CCM wajitokeze kupinga hakuna kitu kama hicho.
 
Baada ya bunge la bajeti tutasuka tena upya baraza la mawaziti tuangalie mwelekeo wa upepo, Pengine tutawavuta watu kwetu.
 
Nakubaliana na mtoa mada. Kumsema mtu sana kunasababisha watu watake kumjua zaidi hali inayomjengea umaarufu
 
Froida, & @ Feedback, mlchokisema kina nguvu na maana kubwa sana ktk ilee mbunge mstaaf wa ccm alichoita "siasa uchwara"
 
Last edited by a moderator:
Jana kwnye media nmemwona Ndgu Shigela akihangaika kulaani kauli ya Nasar.sijui huyu katibu Uvccm wa kundi lipi kati ya mafisadi au watanzania maskini wanao kula mlo mmoja? Kauli ya Joshua ina uhusiano gani na kupanda kwa gharama za maisha,umaskini,huduma mbovu za elimu/afya/barabara, wizi wa rasilimali za taifa,ufisadi na dhuruma inayofanywa na vyombo vya dola. Hili jazi ndo limezama, ccm imebaki ofsini kwenye vitabu tu watu hawapo, . Kwa taarifa ccm ipo I.C.U au mortuary tayari kwa kuzikwa.
 
Ngumu kusahaulika kwa sababu inatenganisha umoja wetu ???

Hebu tujikumbushe kauli hii amabyo ndio kauli ya ukweli katika kutenganisha umoja wetu !!!

“Ninyi wanawake wenzangu ambao waume zenu wapo katika vyama pinzani na mnajua wazi kuwa hawawapi ushirikiano wowote katika siasa ya CCM wanyimeni ‘nonino’, muone kama hawatarejea katika chama tawala, nonino nikiwa na maana ya tendo la ndoa,”

alisema Sophia Simba (MB), huku akishangiliwa na wanawake wote kuonyesha kuwa alilolisema limewagusa.

Hii ilikuwa tarehe 20th June 2010.

Hapo Vipi ???? { Hii "Hapo Vipi" - ni kwa hisani ya Edward Lowassa}

Mkuu ongezea na hii.

UVCCM MKOA Wa PWANI; “…Rais wa 2015, Kamwe hawezi kutokea Kanda ya Kaskazini na anayemjua Rais wa 2015, ni Rais Jakaya M. Kikwete…”
 
Mkuu pamoja na hayo yote, Kuna ,a,mo yamepikwa sana, Nasari hakuzungumzia mikoa ya kaskazini pekee alitamka MIKOA YA MWANZA, SHINYANGA, MARA, KILIMANJARO, MANYARA, ARUSHA NA TANGA NA AKASEMA TUTAKUWA NA MADINI, MBUGA ZA WANYAMA,BANDARI NA KAZALIKA SASA IMEGEUZWA NA KUWA NI MIKOA YA KASKAZINI TU, MIMI NAZANI ILI KUKATA MZIZI WA FITINA ILETWE ILE RECODED, MSIKIE ALICHO SEMA,
 
Imepitwa na wakati sasA hivi tunachoangalia na kuzungumza ni VUA GAMBA VAA GWANDA NA M4C
 
Mkuu pamoja na hayo yote, Kuna ,a,mo yamepikwa sana, Nasari hakuzungumzia mikoa ya kaskazini pekee alitamka MIKOA YA MWANZA, SHINYANGA, MARA, KILIMANJARO, MANYARA, ARUSHA NA TANGA NA AKASEMA TUTAKUWA NA MADINI, MBUGA ZA WANYAMA,BANDARI NA KAZALIKA SASA IMEGEUZWA NA KUWA NI MIKOA YA KASKAZINI TU, MIMI NAZANI ILI KUKATA MZIZI WA FITINA ILETWE ILE RECODED, MSIKIE ALICHO SEMA,

Naunga mkono hoja%100.
 
Back
Top Bottom