Kwa kauli ya nassari inabidi chadema wasitishe kwanza sera yao ya majimbo otherwise itatucost. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa kauli ya nassari inabidi chadema wasitishe kwanza sera yao ya majimbo otherwise itatucost.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msolid1990, May 9, 2012.

 1. Msolid1990

  Msolid1990 Senior Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa mtazamo wangu naona ile sera ya majimbo itabebewa bango sana na ccm na kuihusisha na kauli ya nassari kwa kusema ni mpango wa kaskaz kujitenga.
   
 2. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  hivi huoni hata aibu kurudia vitu na kujadili vitu vilivyosahaulika?
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mtu mjinga utamjua tu
   
 4. M

  Makupa JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  mungu ni mkubwa.2015.tumeshapata silaha ya maangamizi
   
 5. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Msipoangalia itawaangamiza wenyewe.
   
 6. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bomu halichagui ndugu, Labda yale yaliotumiwa south afrika yakiandalia ngozi ya mtu.
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu kauli kama hiyo ya kutenganisha umoja wetu ni ngumu kusahulika.
   
 8. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  CDM tuna msimamo na sera ya majimbo ndio kila kitu na hatuwezi kubadili sera yenye maslahi ya Taifa kwa ajili ya kuogopa propaganda chafu za wakina wassira. Alafu Nassary alichosema wengi mmepotosha 2 pia sisi kama chadema hatuwezi kuogopa propaganda ya kipuuzi kama hii kwani zilikuwa nyingi sana kama hzi kama za udini, ukabila lakini zote zilishindwa, Majibu zaidi mtayapata 2015 na ndipo mtaijua nguvu ya peoples.........
  Ngome yetu ni Mungu tu na sio kingine.
   
 9. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Hivi lazima uandike? Endelea kusoma, huna sera.
   
 10. M

  Makupa JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Sio siri cdm imepata umaarufu siku za hivi karibuni na hata kuanza kuonekana kuleta changamoto kwa chama tawala, ninachowaomba cdm kama wanataka kufuata mkumbo wa iliyokuwa Nccr waendelee ni hii dhana ya utawala wa majimbo ambayo kinadharia ni nzuri ila ni rahisi sana kutumiwa na upande mwingine kuwa nia na madhumuni ya utawala wa majimbo ni kuwagawa watanzania
   
 11. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  we mdosi punguza unafiki.sera ya majimbo imeelezwa vizuri sana na cdm,itafute uisome.
   
 12. M

  Makupa JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu sikatai , ni watanzania wangapi wanasoma ,na usisahau kwamba asilimia zaidi ya sabini ya watanzania huwa wanaamini wanachoambiwa chukulia mfano Babu wa samunge
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Jumatano, Mei 09, 2012 06:11 Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam


  [​IMG]Joshua Nassari

  [​IMG]
  Freeman Mbowe


  *Baada ya Nassari kutoa kauli nzito
  *Asema ni kauli ya kitoto, haina maana
  *Alitaka mikoa ya kaskazini iwe ‘Jamhuri'


  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amefanikiwa kuzima jaribio la Mbunge wa Arumeru Mashariki wa chama hicho, Joshua Nassari, kuhusu suala la kujitenga.
  Mbunge huyo, aliyechaguliwa hivi karibuni, alitoa kauli nzito wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Arusha.

  Alisema umefika wakati ukanda wa kaskazini mwa Tanzania, kujitenga na kuunda taifa lake huru.

  Lakini katika mkutano huo, Mbowe akionekana kutofurahishwa na kauli hiyo, alisimama na kumpinga hadharani Nassari kwa kumponda kuwa hilo ni wazo la kitoto.

  Mkutano huo wa hadhara ulifanyika kwenye viwanja vya Unga Limited, uliokuwa na lengo la kupokea wanachama 3,000 waliokihama Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Maofisa wengi wa chama hicho, walihutubia mkutano huo vizuri na ilipofika zamu ya Nassari kuzungumza, alisema chama kinafikiria wazo la kuunda taifa huru linalohusisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

  "Tuna utajiri wa madini, maeneo mazuri ya utalii na ardhi ya kutosha kuunda nchi yetu wenyewe. Tunapaswa kutafuta uhuru wetu wenyewe, badala ya kuruhusu wengine ambao hawafurahishwi na mabadiliko kuendelea kutuchelewesha," Nassari alisema, huku akishangiliwa na umati.

  Mbowe, ambaye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alikuwa na mwitikio tofauti, akisema madai ya Nassari ni mawazo yake mwenyewe, wala hayawakilishi sera rasmi ya chama.

  "Si sera ya Chadema kuhamasisha kujitenga kwa ukanda wa kaskazini, chama chetu kinahitaji watu kutoka maeneo mengine kushirikiana pamoja kuondoa siasa mbaya za CCM," alisema.

  Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, chama kinaongoza ‘vuguvugu la mabadiliko', ambayo alidai yanafanikiwa, akitolea mfano utendaji wa wabunge wao vijana.

  Aliwataka wabunge hao vijana kuwa pamoja na aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Nassari, akisema wanafanya kazi kubwa katika kuhamasisha mabadiliko nchini.

  Wakati wa mkutano huo, Chadema ilivuna wanachama wapya kutoka wilaya za Monduli, Simanjiro na Ngorongoro, wote wakiapa kuwa watiifu kwa chama chao kipya.

  Katika hatua nyingine, Nassari, aliyekuwa akitafutwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha, jana amejisalimisha mwenyewe.

  Joshua alijisalimisha jana saa 4 asubuhi Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Arusha, ambapo alishindwa kuhojiwa na kuruhusiwa kuondoka, baada ya Kamanda wa Polisi, Thobias Andengenye na Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi, Isaya Mungulu kutokuwapo kituoni hapo.

  Akizungumza na MTANZANIA, Nassari alisema hakuwa na taarifa ya kuitwa na polisi kwa ajili ya mahojiano, zaidi ya kupata taarifa hizo kupitia vyombo vya habari.

  "Mimi sikuwa na taarifa yoyote ya kuitwa polisi, binafsi nimeshangaa kuona jana usiku kwenye televisheni, Kamishina Mungulu akizungumza na waandishi juu yangu kwamba natafutwa, ndiyo maana asubuhi nimefika kituoni, lakini bahati mbaya sikuwapata wote na nimeruhusiwa kuondoka na kutakiwa kurudi baadaye.

  "Sijajua hasa wanachotaka kunihoji, lakini kwa mujibu wa maelezo ya Mungulu, alidai nilitoa lugha za uchochezi katika moja ya mikutano yangu, ninachosema sijawahi kutamka maneno ya uchochezi, tusubiri kwa kuwa nimeambiwa nirudi tutaelezana baadaye," alisema.

  Juzi Jeshi la Polisi, lilifanya mkutano na waandishi na kudai kwamba linawasaka wanachama watatu wa Chadema, akiwamo Nassari, kutokana na kutoa kauli za uchochezi katika mkutano wao maarufu vua gamba na vaa gwanda.

  Mungulu alisema baadhi ya maneno yaliyotamkwa na watuhumiwa ni kwamba ikiwa Jeshi la Polisi halitawakamata waliohusika na mauaji ya Mwenyekiti wa Chadema wa Tawi la Usa River, Msafiri Mbwambo, basi watajitangazia uhuru wa eneo la Meru pamoja na mikoa ya Kaskazini kwa kushirikiana na mikoa ya kanda ya Ziwa.

  Watuhumiwa wengine waliokuwa wakihojiwa na polisi ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), John Heche, Alphonce Mawazo, Emmanuel Kombe na Ally Bananga.

  Akizungumza na MTANZANIA jana, Heche alisema juzi aliitwa polisi na kuhojiwa zaidi ya saa tatu juu ya kauli kadhaa za uchochezi anazodaiwa kuzitoa kwenye mkutano wa hadhara na baadaye kuachiwa.

  Alisema katika mahojiano na polisi, wanamlazimisha kueleza kilichosemwa na Nassari pamoja na viongozi wengine katika mkutano wao hadhara.

  Watuhumiwa hao walifika kituo cha polisi jana wakiongozana na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

  Akizungumza na MTANZANIA, Lema alisema kitendo cha polisi kuwahoji wabunge, viongozi na wanachama wa Chadema ni mbinu zao za kutaka kudhoofisha chama na kuongeza kwamba watapambana hadi mwisho.

  "Huu ni uonevu na dhuluma inayofanywa na Jeshi la Polisi kutaka kudhoofisha nguvu za chama chetu, lakini ninachosema ukanda huu hawauwezi hata kidogo, wapo wanachama wanaohojiwa hata kwenye mkutano hawakuongea kitu chochote, lakini nao wanahojiwa.
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Wow Nassari anafikiria nini?
   
 15. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kauli ya Nassari haina uzito huo inaopewa!
  Wanasiasa uchwara kama Nape wanachukulia hii kama uchochoro wa kutokea mbele za watu!
   
 16. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkuu ivi aliyetajwa hapo juu ni nape !
   
 17. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mod mtu akileta thread Kama hizi tena ambazo zinafikia kumi kwa sasa mpige ban ya mwaka anza na huyu
   
 18. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Imewauma sana inaelekea ndugu yangu Precise!

  Hawa mkiwapiga ban mnawaonea, apigwe ban huyo mtoto asiyechunga kauli zake.
   
 19. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Waandishi wa habari mufilisi....

  Mawazo kwenye pesa, wauze gazeti kwa habari za fasta fasta na uzushi wa kuunda-unda!!
   
 20. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Mkuu tufafanulie , maana wengine hatukuwepo kwenye kusanyiko hilo Arusha
   
Loading...