Kwa kauli hizi unaweza kuitofautisha CCM na Boer (Mkaburu) huu ubaguzi nini hatma ya taifa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Unafungua vyombo vya habari,unaenda mtandaoni unakutana na kauli zifuatazo kutoka kwa viongozi.

1."Kama mnataka msiendelee kubomolewa mchagueni mgombea wetu"unaanza kujiuliza kwa hiyo mkichagua mpinzani,mnapigwa bomoa bomoa?.

2."Unakutana na kauli nyingine,mimi kwenye mkoa wangu diwani wa upinzani siwezi hata kupokea simu yake na hata kumuona sitaki kabisa na wewe mkuu wa wilaya nitakaye kuona unaongea na diwani wa upinzani jiandae kujieleza",unajiuliza ndiyo tumefika huku?

3."Wewe kama ni mtumishi wa umma na unapingana na chama tawala,jiandae kuondoka" unajiuliza mpaka watumishi wa umma nao?

4."Sisi kule bungeni huwa kuna vikao vya vyama,sisi kikao chetu huwa kinaongozwa na waziri mkuu,huko huwa tunagawana kwanza sisi halafu tunaenda bungeni kupitisha ukiwa upinzani hutapata mgao wa miradi ya maendeleo" unajiuliza hii ndiyo maana ya bunge?

Naomba haya iwe ni kutekeza kwa ulimi na si kuwa ndiyo dhamira ya siasa za sasa!.

Hapa ndipo huwa nafikia hatua nasema,wacha nijifunze zaidi hiki kinachoitwa sayansi ya siasa!.Ndiyo hiki wanachosoma watu chuo kikuu mpaka ngazi ya udaktari?
 
Wanajisahau mnooo madaraka yamewapa kibri kikubwa hata hao watetezi wao watakuja choka tuu!
 
Watanzania wamekwisha batizwa wanyonge na masikini so ili mabadiliko ya kweli yatokee ni lazima huo ubatizo wa "unyonge" utoke
 
Back
Top Bottom