Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,863
- 5,694
Kwa kauli aliyoitoa Mh. Mwigulu kuwa kuuawa Kwa wafuasi Wa CCM sio ugaidi Bali ni mauaji ya kisiasa amepotoka na atasababisha mtafaruku zaidi Kwa maoni yangu.
Hapa atahamisha hisia kuwa kuna mauaji yanafanywa na kundi fulani la watu na kusababisha eidha kundi jingine kulipiza kisasi au kujihami ni jambo baya sana Kwa usalama.
Alipaswa kabla hajatoa taarifa hiyo aeleze wazi wahusika ni akina nani na sio kutoa maoni ya kuhisi wakati kama huu mgumu ambao hatujui nani muhusika na watu wanaangamia.
Kwa nilivyo muelewa Mwigulu anatuaminisha kuwa ugaidi hauwezi Lenga kundi la watu fulani tuu, ni lazima lilenge watu wote ndio tuite ugaidi huo sio mtazamo sahihi.
Magaidi walilipua ubalozi wa Marekani hapa nchini na Kenya Kwa wakati mmoja mbona balozi zingine hazikulipuliwa na tulikubali kuwa hilo lilikuwa tukio la kigaidi?
Ukiacha hilo Bomu lililipuka ktk mkuta wa CHADEMA na kuua watu watatu katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani pale Arusha lakini ktk mikutano mingine iliyofanyika siku ile ile hapakulipuka mabomu mbona hatukuambiwa yalikuwa mauaji ya kisiasa? Na wahusika hawajakamatwa mpaka Leo.
Mimi sipingi kuwa nani anahusika au nani hahusiki, nachoeleza ni kuwa ktk hali tuliyo nayo Kwa sasa tujizuie kuongea sana badala yake tutafute Ukweli kwanza tusije tukaingia mtego mbaya zaidi Wa sisi Kwa sisi halafu tukawaacha maadui wakapita katikati yetu salama.