Kwa kauli hizi hawa wamejiandaa kukataa matokeo hata wakishindwa

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Nimesikia mara kadhaa wagombea wa ACT na wa CDM wakidai hawatakubali kushindwa kwa kuibiwa kura. Hii ina maana gani? Ni nani atakayeamua kura zimeibwa au hazikuibwa? Wao? Kama wataamua wao nani atakayepima wanachosema ni kweli au ni uongo? Nani kisheria ndiye anatangaza mshindi?

Kwa kauli hizi hawa wamejiandaa kukataa matokeo hata wakishindwa. Tayari wameshajiandaa kutenda uhalifu. Nia sio uchaguzi! Hawa wametumwa kuleta machafuko nchini. Iwe isiwe hawatakubali matokeo mpaka watangazwe wameshinda hata kama wameshindwa.

Ni kwa nini jeshi la polisi haliwahoji wenye kutoa kauli kuwa wakishindwa wataongoza watu barabarani? Leo mmoja anadai hata jeshi linamuunga mkono! Kweli JWTZ inapanga naye kuingiza watu barabarani?!!
Kinga ni bora kuliko tiba. Tusiache watu watamke uhaini kwa kisingizio cha kampeni. Ni muda sasa wa kumhoji anayedai jeshi letu limejiandaa kufanya vurugu oktoba! Hizi sio kauli nyepesi! Wajinga wakiona zinaachwa wataamini kuwa kweli JWTZ itaingana nao mitaani.
Ndiooo, mtawapiga hata kuwaua lakini kwa nini tuache ifike huko?.
Waiteni muwahoji hawa! Walau basi waonyeni wasiendelee kutoa hizi kauli za kihaini.
Nashangaa KM wa CCM haoni haya anaona mambo ya Yanga na Simba! Yeye ndiye angewaomba polisi wawahoji watu hawa na kauli zao! Angezikemea kauli hizi za kuvunja amani ya Taifa. Angehoji ni nani huyo atakayeamua kura zimeibwa au la? Madaraka hayo atayatoa wapi? Kauli ya KM wa chama tawala ingeweza kuweka uzito kuhusu uhaini huu wa waziwazi.
 
Back
Top Bottom