Kwa kauli hizi hakika uamsho wanaitaka Zanzibar yao. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa kauli hizi hakika uamsho wanaitaka Zanzibar yao.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohamedi Mtoi, Jun 23, 2012.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa wameweka wazi wanachokitaka na hakuna shaka kuwa uamsho ni taasisi ya kidini inayofanya siasa za kuikomboa Zanzibar.

  Haya yako kwenye aya ya mwisho ya taarifa yao kwa vyombo vya habari waliyoitoa leo. inayosema...

  "Jumuiya na Taasisi
  za Kiislamu zinapenda
  ifahamike kwamba,
  inatoa na kupaza sauti ya
  ukombozi wa Zanzibar kwa
  njia za amani bila
  ya kutumia nguvu za silaha
  bali kwa kutumia nguvu za
  hoja na
  inaendesha harakati zake hizo za ukombozi juu ya
  misingi ya sheria za
  nchi na katiba.

  Hivyo basi, wananchi wa Zanzibar kudai uhuru wakujiamulia mambo yetu ni haki yetu ya msingi, na
  kwa hilo HATUNA MJADALA (MPAKA
  TUTAKAPOIPATA NCHI YETU INSHA-ALLAH), tutaendelea
  kudai haki zetu kwa
  kila hali bila ya kuvunja sheria za nchi. Tunasisitiza kuendelea na
  kuidai Zanzibar yetu huru ingawa tunaelewa
  gharama ya kufanya hivyo ni kubwa ikiwemo
  kupoteza roho zetu na mali zetu.

  Na tunatamka wazi
  yakwamba tumechoka na
  ukoloni wa watanganyika
  wachache wasioitakia
  mema Tanganyika na
  Zanzibar.
  Tutaidai nchi yetu kwa gharama yoyote mpaka kuipata Zanzibar yetu
  huru."
   
 2. Ukoo Flani

  Ukoo Flani Senior Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sasa wanamdai nani hiyo nchi yao ilhali wana viongozi wao waliopo kwenye serikali ya Muungano? Wakiwa kitu kimoja na Serikali yao wenyewe ya Umoja wa Kitaifa watatoka kwenye Muungano hata kesho. THE BALL IS ON THEIR SIDE, waache kuuzunguka mbuyu na kutukashifu sisi kwa uroho wa viongozi wao. Ifike mahali Wazanzibari waelewe kuwa Watanganyika wengi hatufaidiki kwa vyovyote vile na uwepo wao kwenye Muungano. Wametuulia nchi yetu tumenyamaza, wameitawala Tanganyika kwa MIAKA KUMI (uongozi wa awamu ya Pili) tulinyamaza. Leo wanatutukana kana kwamba tunafaidika sana na huu Muungano. Shime Wazanzibari unganeni na viongozi wenu mjitoe hata kesho. Kama mlifikiri tunatolea macho uto tumafuta twenu hata kwetu yapo, na mkitaka tuwapunguzia kama tulivyofanya kwenye Umeme. For the records, Tanganyika is the land of Abundances. We are the last country to fight for Natural Resources whatsoever. I hope one day UAMSHO will get these hard facts. Enough is Enough, Let Zanzibar GO!
   
 3. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,195
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  Janjaweed vs uamsho! Patachimbika! Tg yetu macho maana mtoto akililia wembe mpe!
   
 4. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  kazi kweli kweli.
   
 5. hodogo

  hodogo JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 239
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Elimu ni pamoja na upeo wa kuangalia mambo! Namna wewe unavyoangalia mambo hata NECTA wakikupa A+ utapwaya! Ndo maana waswahili wanausemi kuwa KICHWA CHA KUKU HAKISTAHIMILI KILEMBA! Hamuwezi kuanzisha shule, sasa Mkapa kawapa bure chuo msome hamtaki, mnahamia NECTA! Kazi kwelikweli ! Mafisadi ni itikadi ya kisiasa, haina uhusiano na dini!
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  DHAIFU style
   
 7. B

  Bubona JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi Mtanganyika nishaanza kushangaa: Wenzetu wanaondoka!!!!!!
   
 8. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hivi habari ya kudai muungano na ukristo vinahusiana vipi? Zanzibar inatawaliwa na Mwislamu, na mawaziri wake waandamizi wote ni waislamu, Tanganyika inatawaliwa na Mwislamu, makamu wake mwislamu, na waziri wa muungano mwislamu. Sasa Mkristo ameingiaje kwenye hizi habari za muungano uislamu wenu? Na anahusika vipi na matatizo ya waislamu na wazanzibari? Uwe unajaribu kutumia hata damu kufikiria kama ikitokea ubongo wako umeshindwa kabisa. Maana hapa hata tungempa panzi kutafakari jambo hili angalifanya kwa maarifa mengi zaidi kuliko wewe.
   
 9. Ukoo Flani

  Ukoo Flani Senior Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Watu DHAIFU wa fikra wanajua kutoa dismissive claims. Ukristo na Muungano wapi na wapi? Ni bahati mbaya sana baadhi ya waislamu wako obsessed na wakristo. Wanaamini kila tatizo lao linasababishwa na wakristo. Mambo ya kitaifa wao wanalazimisha kucheza kete za udini. Ndio maana walihamaki kusikia wakristo ni 52% ya Watanzania (Tanganyika + Zanzibar).
   
 10. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Jambo usilolijua usiku wa kiza.
   
 11. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,880
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  hivi hilo kanisa ni lipi linalolalamikiwa kila kukicha? Mbna mnakuwa na akili finyu ya kugeneralize mambo
   
 12. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hapo hoja ni udini! Hakuna kingine! Iwapo hoja ni muungano, kazi ni ndogo: Wana rais wao, wamuulize: "kwa nini unang'anga'nia muungano!!!" Asipowajibu basi waichome moto ikulu yao tuone! Kelele za nini!!?
   
 13. The Mockingjay

  The Mockingjay JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tuacheni na chogo zetu. Mkishaondoka hamtafika popote. Mtatwangana tu na kubakana kama Homs na Dafur. Sehemu ya ubongo wa kufikiri iliathirika pale mlipo saga visogo vyenu uchangani.
   
 14. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nina mashaka wazazi wenu walifanya kazi ya kufagia kanisani kwa miaka na miaka halafu kwa sababu nisizozijua, hawakulipwa ujira wao. Na hii ndio sababu hata mkipata jipu leo basi shutuma ni kwa kanisa. Chuki ni dalili ya udhaifu na kushindwa kukabili mambo.

  Hapa umezungumziwa Muungano ambao si sehemu ya UKRISTO wala kanisa, lkn low minds tayari wamesharukia kanisani kujaribu kushusha lawama ya kukosa kwao elimu na ufahamu.

  Labda mniambie kwa ufahamu wenu, Rais wa Zanzibar na Makamu wake wawili na Rais wa Jamhuri na makamu wake mmoja (na wake zake wawili) = hawa watu wanasali kanisa gani kati ya Anglican na RC?

  Labda mtasema wao ni vilaza, haya basi Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na wa Jamhuri nao wanasali wapi kati ya Baptist Mission na Lutheran?

  Huyu bonivilwa inaonesha ameharibika kwa kupenda kukaa na dada zake muda mwingi. Kushinda jikoni ndio madhara yake sasa mtoto wa kiume unabana pua kuongea mipasho. Na ngoja waje hao waarabu, michezo yao si tunaijua, sisi yetu macho na kuwajengea clinic za kujifungulia watoto machotara mnaowataka
   
 15. B

  Bob G JF Bronze Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hivi znz ikijitenga kipi cha msingi Tanganyika itapata hasara? kwanini kulaqzimisha kitu?
   
 16. The Mockingjay

  The Mockingjay JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hoja sio udini bali ni chuki kubwa dhidhi ya wabara. Ingekuwa udini, wasingeita waislamu wa bara chogo. Wanadanganywa na wao sababu ni majuha hawalioni hili kwa sasa.
  Jussa wao hana tofauti na Bashir wa Sudan.
  Bashir aliwarubuni waislamu weusi wa Dafur kuungana na warabu kuwapiga makafir wa kusini.
  Vita ilivyoisha na kuundwa kwa serikali ya mseto ya kusini na north, Bashir hakuweka mtu hata mmoja toka Dafur kwenye govt ya north ya kiislamu. Ndipo Dafur wakajua walidanganywa. Walipojaribu kuleta chokochoko, Bashir akaachia Janjaweed kuwashikisha adabu hao waislamu weusi wa Dafur.
  Hali ya sasa ni mbaya sana. Waislamu safi wa Dafur wanaishi kama wakimbizi kwenye ardhi yao. Wanaume hawadiriki kutoka nje ya kambi kutafuta chakula, wanauliwa. Wanawake ndio wanatoka kutafuta kuni, wanabakwa na baibui zao masikini. Wale wenye mimba wanauliwa sababu wamebeba mtoto mbaya wa adui.

  Ndio maana Bashir anatafutwa na kina Ocampo. Si kwa kutesa na kuuwa makafir, bali kwa mashitaka dhidhi ya matendo anayowafanyia waislamu wa Dafur.

  Na Dafur nao wanajuta sana, wangeshirikiana na wenzao wa kusini, yasingewakuta.

  Kwa hiyo hii ya UAMSHO wanatumia dini tu bali wana agenda za kimaslahi
   
 17. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakuna anayewalazimisha kama ambavyo hakuna anayedai kujitenga. Hawa wana yao tu. Ingekuwa suala ni Muungano sidhani kama kuchoma kanisa lilikuwa jambo sahihi
   
 18. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tatizo lako wewe unafikiri kila mtu ana akili, ngoja nikuambie kitu kwa herufi kubwa.

  KILA UBONGO UPO NDANI YA KICHWA, LKN SI KWELI KWAMBA NDANI YA KILA KICHWA KUNA UBONGO.

  Hayo uliyoyaandika hapo yataeleweka miongoni mwao baada ya miaka 15
   
 19. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #19
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hivi nyinyi Watumbatu, eeeei! Sinawaita nyie mbona hamuitiki? Hivi uhuru mnamdai nani? Rais si mnaye, serikali si mnayo? Wawakilishi na mawaziri wote si mnao? Toeni tamko moja tu kuwa, muungano marufuku. Tangazeni kuwa hamumtambui rais wa jamhuri na wabunge wa jamhuri wapigeni pini wasije tena huku...baaasi!
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Uamsho hawakuchoma kanisa??? wewe wamechoma askari kutoka Tanganyika??

  Uamsho wamewaambia polisi wawashike wote ambao wanafikiri wamechoma kimyaaaa..
   
Loading...