Kwa kauli hii ya Rais Samia, ni wazi kwamba watu wanamdharau (wanamchukulia poa)

nyboma

JF-Expert Member
Aug 29, 2021
2,199
6,890
Kauli ya Mama yetu Raisi Samiah Suluhu Hassan wakati akishuhudia utiaji saini wa awamu ya tatu ya reli ya SGR

"..Ubora wa vifaa vinavyonunuliwa uendane na reli inayojengwa kwa sababu miezi michache niliyokaa serikali, nimeona mambo mengi sana ambayo huko nyuma yalikuwa hayafanyiki lakini sasa yanataka kufanyika, sitakubaki yafanyike”

Kwa upande wangu ningependa kumshauri Mtukufu Mama na Rais wetu Samiah Suluhu Hassani kwamba

“Itakuwa vyema kwa yeye kukaa pembeni mwaka 2025 ili kuepuka kutoa malalamiko kama haya katika hotuba zake pindi ahutubiapo Taifa”

Mpaka Sasa najiulizia Mama yetu Samiah hajatambua nguvu aliyonayo hadi kushauriwa mambo ambayo anaona kabisa yanampotezea credit kwa wananchi na hii inanipa picha ya kwamba kuna watendaji wa ngazi za juu kabisa wanamdharau Mama yetu huyu.

Nihitimishe kwa kusema awe makini na washauri wake maana wamegundua mama ni mpole na ni mgumu wa kuchukua maamuzi.
 
Huwenda haamini kawa Raisi maana kila siku anasema kuna mambo yanaendelea chinichini na hatumuoni akichukua hatua yoyote…

Watoto wa mjini washamzidi kete..
Kama kiongozi huo ni zaidi ya udhaifu mkubwa sana
 
Sio Kumdharau . watu washazoea kupelekeshwa na kupelekwa pelekwa Kama magari mabovu. Wafokewe fokewe wadhalilishwe na kutukanwa majukwaani ndio akili inawakaa sawa.
Yani washamiss tumbua tumbua.

Sasa mama hapo itabidi aige Magufuli style. Tumbua tumbua ianze.

Kikwete nae alikua mpole na diplomasia nyingi yaliyofanyika ndio Kama vile.

Kumbe ndio maana Magufuli alikuwa ana act ubabe na udikteta ili mambo yaende.
Hebu oneni jamani mijitu yenyewe ndio hii. Mizembe kuwaza upigaji tu mfyuuuuuu
 
Aanze na mshauri wake anayemdanganya kusafiri nje kwa kigezo cha kufungua nchi kumbe anampoteza, akimalizana na huyo ndio aje kwa vijana wa mjini maana ndio wanamtia nuksi katika uongozi wake…
Kikwete alisafiri na alifanya makubwa sana, ikiwemo uwekezaji na ajira nje nje, so mwacheni azurule huko nje kuliko kujifungia ndani ka kuku anayeatamia
 
Sio Kumdharau . watu washazoea kupelekeshwa na kupelekwa pelekwa Kama magari mabovu. Wafokewe fokewe fokewe wadhalilishwe majukwaani ndio akili inawakaa sawa.
Yani washamiss tumbua tumbua.

Sasa mama hapo itabidi aige Magufuli style. Tumbua tumbua ianze.

Kumbe ndio maana Magufuli alikuwa ana act ubabe na udikteta kumbe mijitu yenyewe ndio hii. Mizembe kuwaza upigaji tu mfyuuuu
Keshasema yeye ni mama ana staili yake mpya ya kuongoza ila kama staili yenyewe ndio hii ameshafeli muda mrefu abadirike akitaka kuimudu vyema hiyo nafasi..

Kwa kipindi chake ndio nimesikia kauli tofouti tofouti tata zikimlenga moja kwa moja, na hii inaonesha moja kwa moja kwamba watu wanampuuza maana wanajua ni dhaifu..
 
"2025 mtaamua wenyewe muwalete walioleta matozo au muwatoe"

Unapata picha gani kwa kauli hii, Mama keshachokwa na hapa ni miezi tisa tu.
Unapata picha gani kwan wao wana guarantee ya kukaa madarakani kama hawawez ndio watoke
 
Anajistukia tu ukijulisha na namna ambavyo anaongoza nchi bado hajiamini. Ila sio kauli ngeni, nimekua nikiona kwa wnawake wengi wanapopewa dhamana kuna kua na ile dhana kwamba wananichukulia poa. Yan awe mwalimu, mkurugenzi au waziri na sasa tunaona kwa Raisi bado anaona watu wanamdharau.
 
Kauli ya Mama yetu Raisi Samiah Suluhu Hassan wakati akishuhudia utiaji saini wa awamu ya tatu ya reli ya SGR

"..Ubora wa vifaa vinavyonunuliwa uendane na reli inayojengwa kwa sababu miezi michache niliyokaa serikali, nimeona mambo mengi sana ambayo huko nyuma yalikuwa hayafanyiki lakini sasa yanataka kufanyika, sitakubaki yafanyike”

Kwa upande wangu ningependa kumshauri Mtukufu Mama na Rais wetu Samiah Suluhu Hassani kwamba

“Itakuwa vyema kwa yeye kukaa pembeni mwaka 2025 ili kuepuka kutoa malalamiko kama haya katika hotuba zake pindi ahutubiapo Taifa”

Mpaka Sasa najiulizia Mama yetu Samiah hajatambua nguvu aliyonayo hadi kushauriwa mambo ambayo anaona kabisa yanampotezea credit kwa wananchi na hii inanipa picha ya kwamba kuna watendaji wa ngazi za juu kabisa wanamdharau Mama yetu huyu.

Nihitimishe kwa kusema awe makini na washauri wake maana wamegundua mama ni mpole na ni mgumu wa kuchukua maamuzi.
Anamuonea tu MBOWE mijizi inajichotea tu na hana cha kuifanya
 
Back
Top Bottom