Kwa kauli hii ya Mwenyekiti wa CCM kuhusu kura za maoni, Mwita Waitara amekurupuka kutangaza nia muda bado

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,761
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Magufuli amewataka wanachama wa chama chake kuacha kugombana kwa tamaa ya kugombea madaraka na hasa ubunge na udiwani.

Rais Magufuli amewataka wana CCM kufuata taratibu na kanuni za chama kuhusiana na kura za maoni na kwamba waepuke tabia za "kukurupuka"

Rais Magufuli amewataka wana CCM kusubiri ratiba ya chama kuhusu muda wa kutangaza NIA na utaratibu wa kampeni za kura ya maoni.

Source: Star Tv

My take: Naibu Waziri Mwita Waitara ameshatangaza nia kupitia Star Tv kwamba atagombea Ubunge Tarime Bijijini, Je amekurupuka?
 
Mwenyekiti mwenyewe ni mfuata utaratibu? Kama yeye na genge lake wana majina yao mfukoni, anategemea nini?
Kuna wakati watu hujifunza na kubadilika. Japo mimi siyo mfuasi wa CCM, lakini Rais Magufuli ametoa hotuba/maneno mazuri kwenye kikao cha viongozi wa CCM juu ya taratibu zitakazotumika kuwapata wagombea. Lakini pia alieleza kuwa uchaguzi utakuwa wa haki.

Kilichobakia ni kusubiria na kuona kama Rais Magufuli atatembea juu ya maneno yake. Karibu awamu zote, marais wamekuwa hawafanyi vizuri kwenye miaka 5 ya mwanzo. Hujirekebisha wakati wa kipindi cha pili. Hata Magufuli anaweza kufanya vizuri kipindi cha pili. Wengine watashangaa kwa nini nazungumzia kipindi cha pili wakati hajachaguliwa. Ukweli ni kuwa napenda Rais Magufuli apate challenge ya uchaguzi wa ushindani wa haki lakini siamini kama anaweza kushindwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa mwaka huu hata kama kukiwa na Tume huru.
 
Mkuu uko sahihi sana kwa maelezo yako, lakini Magufuli ninayemjua mimi huwa anafuata taratibu anazozitaka yeye, na yale anayotaka yeye hata kama yanapingana na sheria atayafanya bila kujali sheria/aratibu zinataka nini. Nilichojifunza kwake anachokisema hasa kwenye utii wa demokrasia ni tofauti na anachofanya, hivyo sitegemei jipya kwenye uchaguzi huu. Rejea alipokuwa mbunge ni mara ngapi alishinda kwa box la kura, na fuatilia baada ya kuwasili rais chaguzi haba nchini zimefanyika kwa mwenendo gani.

Uko sahihi sana unaposema hata kukiwa na tume huru hawezi kushindwa. Kwanza kimsingi tume huru si kwaajili ya Magufuli kushindwa au ccm, bali ni kwa ajili ya kutangaza mshindi wa halali. Ni mjinga tu ndio anaamini tume huru ni kwa ajili ya Magufuli au ccm kushindwa. Iwapo kutakuwa na tume huru ya kweli, Magufuli anaweza kushinda, hilo sina tatizo nalo, lakini hakuna uwezekano wa yeye kushinda kwa zaidi ya 50%+, jambo ambalo hayuko tayari yeye binafsi na chama chake. Pia mtazame vizuri sio mtu anayeweza siasa za ushindani, na hayuko tayari hasa yeye binafsi na chama chake kushiriki kwenye uchaguzi wa ushindani wa kweli.
 
Back
Top Bottom