Kwa kauli hii tu waTZ wangekuwa makini kikwete asingefaa kuwa hata M/kiti wa kijiji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa kauli hii tu waTZ wangekuwa makini kikwete asingefaa kuwa hata M/kiti wa kijiji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Feb 28, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Mnakumbuka ile kauli maarufu ya jk kwamba hafahamu kwa nini nchi yake ni maskini?!? Kwa mawazo yangu watanzania tungekuwa makini angalau kidogo, kauli hii ingem-disqualify kikwete kiasi cha kutofaa kuwa hata M'kiti wa serikali kijiji.
   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Tatizo letu sisi ni waoga sna!!!
  Asante Chadema mapinduzi daimaa
   
 3. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  NGUVU YA UMMA ITALETA MAgeuzi ya Kweli na si hiyo kauli mbiu za Kifisadi kupindua haki za raia wake
   
 4. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Ooohhh yes, kiongozi gani wa nchi asiyejua hata sababu ya nchi kuwa maskini!!!!!! Sasa yupo ikulu kufanya nini kama siyo kupoteza muda tu!!!!! Angegombea uenyekiti wa mtaa wetu wala asingepata.
   
 5. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Ukiwa kiongozi unatakiwa uwe na falsafa yako na maono yako.

  Kama kiongozi hajui matatizo ya anaowaongoza basi pasi shaka kila njia inafaa kwake.

  Nyerere aliazimia kujenga umoja wa kitaifa na kwa sehemu alifanikiwa.
  Mwinyi aliazimia kufungua milango ya uchumi na alifanikiwa ingawa hata mainzi yaliingia. Serikali ikawa maskini ingawa wananchi wanaweka pesa kwenye soksi.
  Mkapa aliazimia kukuza uchumi mkuu na serikali kweli ikawa na mapesa kibao hata ya kununua rada, jet, epa, meremeta, reserve ya kufa mtu n.k. Hapa serikali tajiri wananchi wanalia Ukapa.

  Our very own presidaa akaambiwa na kina EL aje na kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania. Miaka mitano down the road, maisha yangu hayajabadilika. Serikali haina pesa na wananchi hatuna pesa cha msingi BORA MAISHA.

  Mkuu wa nchi anasema anataka tumkumbuke kwamba alitutoa hapa mpaka hapa. A very general statement as usual.

  Uzuri/Ubaya ni kwamba iwe tulimchagua ama hatukumchagua anabaki kuwa Presidaa wetu, tutakoma!
   
Loading...