Kwa Kauli hii tata na iliyojaa Mafumbo Mbunge Nape Nnauye amemaanisha nini na kamlenga nani Tanzania?

Watu wa Dar bwana! Yaani siku ya jana walikuwa busy kupigana vikumbo eti kwenda kushuhudia tamthiliya yao pendwa ya Sultani ikifikia tamati! Haya ni maajabu ya dunia! Na Nape naye kumbe alikuwepo!

Eti walitakiwa wavae Kisultani na Kihurem nani sijui vile na wakavaa kweli! Muda huo wazee wa mikoani tulitingwa na mechi ya Afcon kati ya Burundi dhidi ya Nigeria! Aisee wacha tu mjengewe flyovers! Maana mnastahili.
 
Anamaanisha: Yeye pamoja na wote waliokatwa mikia watarejea kuidai haki yao dhidi ya Bwana Yule
 
..shambulizi dhidi ya Mh.Tundu Lissu.
Ya Tundu ndo imemuuma kuliko ya wale waliomwaga damu hadi kufa kule Arusha kwa kurushiwa bomu kwenye mkutano na mtu "asiyejulikana" wakati wao wakikata mitaa na Kinana?
Anyways, no problem.
Siku hizi akina Nape, Membe, Nyalandu ndo mashujaa wetu makamanda.
 
Anaweza kuwa anasema ukweli. Ila changamoto ni hii busara inayoibuka baada ya kutumbuliwa.
 
Halengi damu ya mtu kweli, bali damu ya mtu kwenye tamthilia.

Nape alikuwa ni shujaa enzi zile akisema ”kinyago uchonge mwenyewe, hakiwezi kukutisha" lakini tangu alipotishwa na hiki kinyago alichokichonga mwenyewe, sasa Nape ni kwisha kabisa habari yake, hadi akiona kivuli tuu, anatishika.
P.
 
Mwisho
Umesema amekaa kimamamama, lakini na wewe umemalizia kwa fumbo "Unafiki una mwisho wake" Fafanua kidogo.
Mwisho Wa unafiki ni pale inapojulikana kuwa wewe ni mnafiki.
Hakuna mtu atakutilia maanani zaidi ya wanafiki wenzio
Tena wahanga wa unafiki wako wanaweza kukushughulikia hata kwa kusutwa
Hili sio fumbo
 
Ya Tundu ndo imemuuma kuliko ya wale waliomwaga damu hadi kufa kule Arusha kwa kurushiwa bomu kwenye mkutano na mtu "asiyejulikana" wakati wao wakikata mitaa na Kinana?
Anyways, no problem.
Siku hizi akina Nape, Membe, Nyalandu ndo mashujaa wetu makamanda.

..Lissu ni mbunge mwenzake.

..pia wana utani wa kuitana mjomba.

..Makamanda wana sympathize na Nape kwasababu ya mkasa uliomkuta wa kutaka kuuwawa kwa bastola na mtu aliyeonekana lakini "asiyejulikana."
 
Halengi damu ya mtu kweli, bali damu ya mtu kwenye tamthilia.

Nape alikuwa ni shujaa enzi zile akisema ”kinyago uchonge mwenyewe, hakiwezi kukutisha" lakini tangu alipotishwa na hiki kinyago alichokichonga mwenyewe, sasa Nape ni kwisha kabisa habari yake, hadi akiona kivuli tuu, anatishika.
P.
Pascal ukitaka kuingia kwenye siasa kwa stahili yako hautafika mbali. Pili huna uwezo wa kututafsilia sisi maana.
 
Halengi damu ya mtu kweli, bali damu ya mtu kwenye tamthilia.

Nape alikuwa ni shujaa enzi zile akisema ”kinyago uchonge mwenyewe, hakiwezi kukutisha" lakini tangu alipotishwa na hiki kinyago alichokichonga mwenyewe, sasa Nape ni kwisha kabisa habari yake, hadi akiona kivuli tuu, anatishika.
P.
Ni kama Pascal toka alipoitwa na kuhojiwa na Bunge kawa kama Mbwa mzee...kubweka saaana kuuma hawezi tena
 
Katika Mahojiano yake na Azam Tv dhidi ya Tamthilia maarufu ya Sultan Mbunge Nape Nnauye alisikika akisema kuwa Damu ya Mtu Inadai na hata wakati anaisema hii Kauli Usoni mwake alionekana ni Mtu aliye serious kabisa kana kwamba kuna Jambo linamuumiza au limetokea na limemuumiza.

Kwa wale mliobobea katika Mafumbo kwa Kauli hii ya Nape kuwa Damu ya Mtu Inadai analenga nini?

Tujadili.
TL
 
Halengi damu ya mtu kweli, bali damu ya mtu kwenye tamthilia.

Nape alikuwa ni shujaa enzi zile akisema ”kinyago uchonge mwenyewe, hakiwezi kukutisha" lakini tangu alipotishwa na hiki kinyago alichokichonga mwenyewe, sasa Nape ni kwisha kabisa habari yake, hadi akiona kivuli tuu, anatishika.
P.

Ni wazi alikuwa hajajua ile hadithi ya ‘The Frankenstein Monster’!
 
Sikatai kwamba ktk serikali hii yapo mapungufu kadhaa lkn hii haimpi uharali wowote mtu km Nape leo kujifanya mkosoaji mkuu kwangu mm kumbukumbu za mambo ya hovyo yaliyofanywa na hawa kina Nape zibaki mbichi miaka zaidi ya miambili.
 
..msikilizeni Mh.Nape kwenye video hapo chini.

..gari iliyokuwa ikimfuatilia Mh.Lissu ilikuwa ikimfuatilia Nape na wabunge wengine.

..Na Nape anasema wabunge walilalamika na kutoa taarifa.

..hili suala lina ukakasi. Haiwezekani kuwe na watu wanawafuatilia wabunge halafu Polisi wasichukue hatua.

..utetezi wa IGP Sirro kwamba TL hakwenda kituoni kutoa taarifa ni utetezi dhaifu.

Back
Top Bottom