Kwa Kauli hii Seif kweli si UAMSHO? au kuna nini nyuma ya kauli hii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Kauli hii Seif kweli si UAMSHO? au kuna nini nyuma ya kauli hii?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Jun 18, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Jana makamu wa kwanza wa rais Zanzibar Seif kasema na nilimsikia kwamba Wazanzibar wanayo katiba Yao kwa hiyo machakato wa Katiba hauwahusu ila tu waseme maoni Yao kuhusu Muungano.

  Wadau hapa Utamtofautishaje na UAMSHO?
   
 2. P

  PakavuNateleza JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 957
  Likes Received: 513
  Trophy Points: 180
  There is neither connection nor correlation between what you are saying and what maalim is saying kwa sababu Zanzibar ni kweli wanakatiba yao.So where is UAMSHO coming in?
   
 3. n

  nsekangaye.kagabo Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KAMA WANA KATIBA YAO KWENYE TUME WATAKWENDA KUFANYA NINI? KWA NINI HAWAKUKATAA? AU WACHUMIA TUMBO?:thinking:
   
 4. M

  Makupa JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  asilimia tisini wa wana cuf wanaunga mkono uamsho
   
 5. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  BWANA YESU ANAOKOA, KWA NINI MNAUMIZA AKILI HIVI?KWA NINI MNASONONEKA?KWA NINI MNAHANGAIKA NA HII DUNIA? MPE BWANA YESU MAISHA YAKO NA KUHAKIKISHIA HUTA JUTA,roho ya hasira,chuki na mambo mabaya yataondoka nawe utakuwa mwenye furaha muda wote.KARIBU KANISA LOLOTE LILILOKARIBU NAWE LINALOAMINI WOKOVU.
  AU TUWASILIANE KWA EMAIL :johnhella2007@yahoo.com hiyo email naitumia hata facebook ukisearch kwa email hiyo utanipata
   
 6. D

  Deofm JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kama kweli wanataka kuvunja muungano, wabunge wa zanzibar wagome kuja bungeni, na makamu wa rais pamoja na mawaziri wa jamhuri ya muungano wanaotokea zanzibar warudi kwao ndipo waanze kudai hiyo kura ya maoni na marekebisho mengini, huwezi kukata tawi ulilokalia, utaumia mwenyewe.
   
 7. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Muungano ulale mahali pema peponi
   
 8. A

  Albimany JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
   
 9. B

  Bob G JF Bronze Member

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mbona hilo liko wazi na si yeye hata walioungana nao lao moja si mmemsikia Raza kwenye baraza la wawakilishi ni walewale kikundi cha KIGAIDI UAMSHO
   
 10. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Kwani una wivu gani Seif Kuwa Uamsho? Uamsho ni Wazanzibar kindaki ndaki na ni kundi la wana wa zanzibar lililo sajiliwa kisheria kwa katiba ya Serekali ya Mapinduzi ya watu wa Zanzibar 1984, na seif si Mtanganyika ni Mzanzibar sasa wewe kinachokuma nini ?.

  Huu Muungano na nyiyi imekuwa tabu tena kutaka kujuwa mambo hata ya wazanzibar wenyewe yasio wahusu nyiyi, jee kuna zambi gani Seif kuwa Uamsho ?.

  Nyiyi mwisho tena imekuwa kama machambenga vile munaumwa hata kuona wazanzibar kwa wazanzibar wana kaa pamoja nyiyi wivu, ni yale yale ya Wazanzibar kuda Serekali yao ya pamoja nyiyi mukaumwa na kupiticha choko choko.

  Kwani nani kawakataza na nyiyi kufanya hivyo Watanganyika?, mbona mumekuwa vigwagwadu nyiyi kwa mambo yasio wahusu kuwa na wivu nayo?
   
 11. R

  RMA JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Basi Wazanzibari walioteuliwa kwenye tume ya katiba waondolewe!!!
   
 12. Zux de

  Zux de JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
   
 13. Zux de

  Zux de JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  duu we msomali nn?
   
 14. M

  Mzenji73 JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hata wana CCM zanzibar na wananchi wengine wakio wengi wa zanzibar pia tunaiunga mkono uamsho. so what?

   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwani Sefu au Mwingine yeyote kuwaunga mkono Uamsho ni haramu?
   
 16. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hivi kuna tofauti kati ya cuf na uamsho!?
   
 17. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  JUMATATU, JUNI 25, 2012 05:20

  NA BENJAMIN MASESE, DAR ES SALAAM

  Gazeti La MTANZANIA

  ALIYEKUWA Mlinzi wa Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad, anadaiwa kuwa miongoni mwa wafuasi wa kikundi cha Uamsho visiwani humo.

  Taarifa zilizopatikana kutoka Mjini Zanzibar zinasema kuwa, mlinzi huyo wa zamani wa Maalim Seif, Rashid Ally Nyange, alionekana akiwa katika msafara wa kiongozi wa Shura ya Maimamu Zanzibar, Farid Hadi Ahmed, wakati akitoka kuswali katika Msikiti wa Mbuyuni Unguja hivi karibuni.

  Mmoja wa wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema:

  "Mlinzi huyo wa Maalim Seif ni mmoja kati ya walinzi watatu wa karibu wa kiongozi huyo wa dini, anayeongoza kikundi cha jumuiya ya Uamsho.

  "Sisi wananchi tumesikitishwa sana tulipoona picha ya kiongozi wa Shura ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid katika gazeti moja la kila siku akilindwa na aliyekuwa mlinzi wa Maalim Seif.

  "Sisi kama wanachama wa CUF tunahoji sababu za mlinzi huyo wa Maalim Seif kumlinda kiongozi huyu wa dini na aliajiriwa lini au ameagizwa na Katibu Mkuu wetu Seif kumlinda kiongozi huyo wa dini," alihoji mtoa taarifa huyo.

  Akizungumza na MTANZANIA mwishoni mwa wiki iliyopita Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro, alisema baada ya Maalim Seif kuwa, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, waliokuwa walinzi wake wa karibu waliachishwa kazi kwa barua rasmi.

  Mtatiro alikiri kwamba, Nyange ni mmoja kati ya waliokuwa walinzi wa karibu wa Maalim Seif na kuongeza kwamba, hivi sasa siyo mlinzi tena na hawajui anafanya kazi gani.

  "Hivi sasa Maalim Seif analindwa na walinzi wa Serikali na wale walinzi wake wa awali, waliachishwa kazi kwa barua na hatujui walipo sasa na pia hao walinzi hawazuiwi kuajiriwa sehemu nyingine kwa sababu wana uzoefu wa ulinzi.

  "Kwa sasa Maalim wakati wote analindwa na walinzi wa Serikali, hata anapokuja hapa walinzi wake hutangulia na mbwa kuja kunusanusa.

  "Katika hili, sijawahi kuwaona walinzi wake wa awali, pia jambo la kusema Maalim Seif anajihusisha na kikundi cha Uamsho ni uongo na uzushi, kwani katika hotuba zake zote alizozitoa baada ya kutokea vurugu hizo, alikemea sana, sasa iweje ajihusishe?

  "Maalim Seif hapingi Muungano uliopo sasa, hata siku moja hajawahi kusema, lakini mara nyingi amekuwa akiunga mkono uwepo wa Serikali tatu, yaani Serikali ya Zanzibar, Tanganyika na Serikali ya Shirikisho na hili siyo geni, kwani hata Katiba yetu inaeleza hivyo," alisema Mtatiro.

  Nyange alipozungumza na MTANZANIA kwa simu mwishoni mwa wiki, hakutaka kukubali wala kukataa juu ya kujihusisha na kikundi hicho.

  Katika mazungumzo yake na mwandishi wetu, Nyange alisikiliza kila alichokuwa akiulizwa, kisha akasema asante na kukata simu.

  Juzi, Mwanasheria wa SMZ, Othman Masoud, aliitaka jumuiya hiyo kuacha kuwapotosha wananchi kuhusu Muungano.

  Pia Masoud alionya kuwa jumuiya hiyo wanachofanya ni kuwapeleka wananchi porini, baada ya kuacha njia safi iliyonyooka ambayo ni kusubiri kutoa maoni katika tume ya kukusanya maoni ya kurekebisha Katiba.

  Awali, Waziri asiyekuwa na wizara maalumu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mansour Yusuf Himid, alitangaza kuvutiwa na msimamo wa jumuiya hiyo kuhusu Muungano, huku akisisitiza kwamba lengo la jumuiya hiyo ni kutetea maslahi ya watu wa Zanzibar katika Muungano na kuitaka Serikali kuwaacha wananchi wawe huru.

   
 18. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wow Hatari Kweli... Ni kama ilivyokuwa Rwanda mtu unayemjua fika anakujia na Panga anakuambia Samahani

  Nimeambiwa nikate kichwa chako, nisipofanya hivyo watakikata changu.
   
 19. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Kila mzanzibar ni uamsho.. kila mwenye kupenda maendeleo ya Zanzibar kimbilio pekee lililobaki ni kwa ma shekh wetu kwani wanasiasa wanatupotezea... Mungu awape maisha marefu ma shekh wetu mpaka Zanzibar iwe huru...
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona maneno yako hayana uhusiano na Uamsho nadhani huijui Zanzibar, Zanzibar nzima ni Uamsho.
   
Loading...