KWA KAULI hii MUUNGANO UVUNJIKE TU!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KWA KAULI hii MUUNGANO UVUNJIKE TU!!!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mizambwa, Jul 19, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  BOFYA HAPA: 250 wazama Zanzibar

  Naanza kwa kuwapa pole wananchi wote walipoteza ndugu zao na wale walionusurika katika ajali ya kuzama kwa meli hapo jana 18/07/2012.

  RIP Marehemu wote.

  Maneno aliyosema Mh. Spika na tabia ya uendeshaji wa Bunge la Muungano inaonyesha kuna ubaguzi mkubwa ambapo hakuna sababu ya kuendelea kuwa na Muungano kama pande za Muungano hazina umoja na Mshikamanao wa kweli.

  Na pia kauli ya Raisi Kikwete eti anatuma salamu za Rambirambi kwa Raisi wa ZNZ, ina maana hizi ni nchi mbili kwani tulitegemea kama ni salamu za Rambirambi zitoke nje ya JMT na siyo kutoka kwa Rais wa JMT.

  Waliopatwa na maafa katika tukio la kuzama meli hapo jana siyo WAZNZ peke yao bali ile meli ilikuwa inatoka DSM kwenda ZNZ hivyo bila shaka pia kuna Watu wa huko Tanzania bara walikuwmo pia.

  Sas Raisi Kikwete aliwaona wa Wananchi wa tanzania Visiwani tu, hakujua kuwa tukiwa kama nchi kuna wananchi wengi toka Bara wamo na wananch wengi wa ZNZ wamo katika ile meli.

  Binafsi sioni sababu za kuendelea na muungano kwani viongozi wa mihimili ya juu wamejionyesha kuwa tupo tofauti.  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 2. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  We ulikuwa hujui kuwa muungano no lazima uvunjike ili kila mtu awe na adabu?
   
 3. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hivi pale JK anapotuma rambi rambi kwa mkuu wa mkoa ajali au kitu kinapotokea hua inakuwaje?
   
 4. koo

  koo JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwahiyo unamfananisha rais wa zenji na mkuu wa mkoa?

  Ila kimsingi sioni kosa kutuma salam kwa rais wa zanziba kwani ndiye anaeshughulikia swala hilo kwa karibu kwa niaba yake hivyo anastahili kupewa salam hizo.

  Kuvunjika kwa muungano hakutokani na sababu ulizotaja mtoa hoja bali nikukosekana kwa mantiki ya mfumo wa muungano na kuchoshwa na kelele za wazenji zisizoisha na ulafi wa vijirasilimali vya mafuta nakujiona mmemaliza matatizo kumbe ndio yanaanza.
   
 5. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Kila mtu bora muungano uvunjike bila kusema utafunjikaje?Toka kwenye keyboard nenda nje anza maandamo ndiyo ujue utafunjika ama lah.
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Naona kuna utata mwingi hapo. Pia spika alisema kuwa labda ajali ingetokea maeneo ya chamwino...
   
 7. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,950
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  Shein ni kama mkuu wa mkoa!
   
 8. K

  Kakubilo Kasota Senior Member

  #8
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani mkuu ulikua hufahamu kuwa Zanzibar na rais wao ni kama mkoa na mkuu wa mkoa tu, bisha nikupe ushahidi, bajeti zao zote source of income moja wapo huwa tutapokea kiasi fulani toka Tanzania bara na nyingine kwenye vyanzo vyao, kwani bajeti za mikoa hasa majiji huwa zinakuaje? si ni hivyo hivyo tu.

  Muheshimia Shein akienda nje ya nchi huwa anatambuliwa kama nani? maana'ke huwa wanasema ametoka Tanzania na sio Zanzibar, rais wa Tanzania nje ya nchi jamani si anaeleweka? Labda kimsingi tunaweza kumpa nafasi sawa na Waziri, kwani kwenye baraza la mawaziri yeye na Dr Hussein Mwinyi, tofauti zao huwa ni nini pale kikaoni? Bisheni sasa, kwanza hata hela za kuwalipa polisi wenu huwa mnatoa huku!
   
 9. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ndo maana unaambiwa rais wetu ni dhaifu!
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Jamani Ndio Nyinyi Wenyewe Mliomba hayo; Mnakumbuka Rais Wa Zanzibar alikuwa automatically Makamu wa

  Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania? Rais Mwinyi alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano bado

  Mlikuwa Mnalalamika; AZIMIO LA ZANZIBAR Ndio likatenganisha hayo Madaraka; Rais wa Zanzibar akawa HURU

  NA JAMHURI YA MUUNGANO; UNAKUMBUKA KIKWETE ALIMUAPISHA RAIS WA SASA WA ZANZIBAR RAIS Dr.

  SHEIN ili awe anashiriki Mikutano ya Baraza la Mawaziri la Muungano ambalo haji kushiriki lakini kiti chake

  kinawekwa na kinakuwa wazi. Kwahiyo Sasa kikwete anapaswa kutuma RAMBIRAMBI kwa RAIS wa ZANZIBAR

  kama Nchi ndani ya NCHI unajua kuna BENDERA ya Zanzibar baada ya AZIMIO LA ZANZIBAR... ZANZIBAR is

  80% INDEPENDENT COUNTRY...
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwa nchi za wenzetu, inapotokea swala kama hili basi bunge hubadilisha hata agenda zake na kujadili haraka swala lilojitokeza na sio kuvunja bunge kwa sababu ya msiba ambao bado unahitaji nguvu kubwa ya kiutendaji kuokoa maisha ya watu. kuna maswali menmgi yalitakiwa kuulizwa na pengine kupata majibu haraka jambo ambalo halikufanyika kwa sababu tulivunja bunge bila kufikiria..

  Tatizo la Tanzania siku zote tunafanya vitu kinyume nyume, harusi na misiba ndio sehemu za matumizi makubwa ya fedha japokuwa tumekatazwa ktk imani za dini. Na kuhusu swala la rambi rambi ni muhimu sana kwa rais kuelekeza rambirambi zake kwa wafiwa japokuwa yeye mwenyewe ni mfiwa. Hata mzazi wako akifariki leo maadam haupo msibani utawapa pole dada, kaka na ndugu zako wote ambao pia watakupa pole wewe vile vile. Huwezi kutoa pole za hewani yaani hazina mwenyewe au kujipa pole wewe mwenyewe..Hii sii mila na desturi zetu hivyo Rais hajakosea.
   
 12. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  JK na Makinda walistahili kui-regard ajali as ni ya Zanzibar.

  Siku ya kwanza kabisa, mmiliki wa meli hiyo alisema inakuwa vigumu kwa vikosi vya uokoaji vya Bara kwenda kuokoa wahanga kwa kuwa eneo ilipotokea ajali ni 'maji ya bahari ya Zanzibar' !!

  Hapo hapo nilipata picha fulani inayoonyesha kuwa wanaovuka huku na kule between Bara na Zanzibar huwa wana.face mambo fulani ya kimipaka!
   
 13. M

  Mkangawalo New Member

  #13
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 7, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muungano uvunjike kwani tuna faida gani na muungano?
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Katika kichwa cha habari inasema "kwa kauli hii" katika utumbo wa habari hujaleta kauli yoyote bali ni kauli zako tu. Vipi?
   
 15. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Angalia haya maneno ya Spika:
  =====================================================================================================
  Hata hivyo Spika Makinda alikataa kuahirisha shughuli za Bunge akisema kanuni hiyo inatumika vibaya, kwani ilitakiwa jambo hilo liwe limetokea eneo lililo karibu na Bunge.

  Alisema watahitajika wabunge wawahi kutoa damu au msaada wowote wa haraka lakini kwakuwa limetokea Zanzibar, wabunge hawawezi kutoa msaada wowote kwa haraka, zaidi ya kupiga simu kujua kilichotokea.

  "Nimeshawasiliana na waziri anayehusika na majanga na wamekubaliana kuwa awasiliane na wahusika waliopo kwenye eneo la tukio na kisha tutajua tutakavyojipanga," alisema Makinda.

  =========================================================================================

  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,225
  Trophy Points: 280
  undugu wa kujuana kwenye majanga tu.....

  hali ikiwa shwari wanawaita wabara "chogo"

  kazi ipo......

  kidumu chama cha mapinduzi
   
 17. Mtanzanika

  Mtanzanika JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 2,209
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, na kuna Kiongozi wa Zanzibar....sioni kama kuna tatizo Kiongozi wa eneo husika kupewa salaam za rambirambi...ni kama hivyo usemavyo mkuu kuhusu kiongozi wa Mkoa!!!
   
 18. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanzania nchi 1 na Serikali 1 ndio suluhu ya kweli
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hatuhitaji ajali ya meli ili kuvunja Muungano. Katiba ya JMT ipo Zanzibar? Inafanya kazi? Kuna walioapa kuilinda na kuitetea kule? Wanafanya hivo?
   
 20. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,147
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  hawa wazanzibari ni kama mkoa mmoja tu nashangaa hizi mbwembwe zinatoka wapi..
   
Loading...