Kwa Katiba yetu ya sasa, tunajiliwaza kusema 'Zanzibar ni nchi'

President Elect

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
693
212
Mazungumzo yaliyomalizika bungeni hivi karibuni, yalipelekea wawakilishi wa Z'bar kukanusha kwamba, kamwe hawawezi kuwa koloni la Tanganyika!

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar ni 'sehemu' ya nchi ya Tanzania, ambapo visiwa vya Unguja na Pemba vinachangia mikoa mitano ndani ya serikali ya JMT.

Kwa vile katiba yetu pia haitambui kuwepo kwa nchi ya Tanganyika, ni kweli kuwa kamwe Z'bar haiwezi kuwa koloni la Tanganyika. Je, kwa vile iko chini ya Tanzania ndio tuseme kwamba Z'bar ni koloni la Tanzania?

Wazanzibari wana haki ya kudai utaifa wao. Ni vyema watumie mabadiliko ya katiba kuthibitisha hilo.

Na waende mbali zaidi, wadai kiti chao UN! Hapo muungano utakuwa wa maana kwao, kati ya nchi ya Z'bar na Tanganyika.
 
Zanzibar SI nchi ndani ya Tanzania,
Itakuwa nchi kama watajitoa kwenye Muungano,
Kama ni kutaka kujiridhisha na kuwafurahisha, ni sawa, ni NCHI ili wafurahi!
 
Zanzibar inatamani sana kuwa 'a sovereign state' ndani ya muungano. Katiba ya Jamhuri ikibadilishwa, hilo linawezekana.
 
Watu wa visiwani wanayomatatizo makubwa kuliko uzanzibar wanaouzungumzia,waliotakiwa kupiga kelelel ni watanganyika'wadanganyika'lakini ajabu ni kuwa wazanzibar ndo wanoongoza kulalamika kama 'Boko harammmm'vile
 
Back
Top Bottom