Kwa kasi hii ya Saashisha Mafuwe, hakuna wa kumtoa Jimbo la Hai

Jul 19, 2020
39
128
Ni Mbunge Imara na Mwenye Maono Mapana ya Jimbo lake

Anaandika Madam Rose Matemu

Mhe. Saashisha Elinikyo Mafuwe, katika kipindi chake cha Uongozi, ameweza kuonyesha njia kwa kuwa msimamizi mzuri, msemaji, mfuatiliaji na mhamasishaji wa shughuli za Maendeleo katika jimbo letu la Hai. Mbali na kuwa Kiongozi wa watu lakini ameweza kujenga ukaribu mkubwa na Wananchi wa Jimbo lake la hai kwa kuwasikiliza, kutatua ama kuwasilisha changamoto zao kwa Mamlaka husika ama kupitia jukwaa la Kibunge.

Mbunge huyu ameweza kusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika muda wake mfupi tu wa Uongozi;

Miradi ya Maji: Ameweza kuibua miradi mbalimbali ya maji kwa kushawishi Mamlaka kutimiza wajibu wake kama ilivyo katika ilani ya Chama cha Mapinduzi. Mbunge wetu ameonekana mara kadhaa bungeni akipigania miradi hii ikamilike kwa uharaka, hivi majuzi amefanikiwa kuwasha kukamilika kwa mradi wa Kikafu na sasa tunapata maji jambo lililokuwa limeshindikana kwa zaidi ya miaka 20 ya watangulizi wake. Hii ni kutoka na ufuatiliaji wake wa mara kwa mara wa Mbunge wetu.

Leo hii katika Jimbo la hai, changamoto ya huduma ya maji safi na salama kwa Wanachi imepungua kwa kiasi kikubwa sana. Zaidi ya Kata zote katika jimbo la Hai huduma hii ya ni ya uhakika, na bado anaendelea kupambana kuhakikisha changamoto hii ya maji inakuwa historia katika Jimbo la Hai. *Hakika ni Kiongozi mwenye kuacha Alama.

Miundo Mbinu ya Barabara: Hali ya miundombinu ya barabara imeimarika katika jimbo la hai. Maeneo mengi ndani ya jimbo na kata zetu kwa sasa yanafikika kiurahisi kutoka na matengenezo ya mara kwa mara ya barabara zetu katika kiwango cha lami na changarawe. Hivi ni nani asiyeona hili katika Jimbo letu?

Huduma za Afya: Leo hii katika jimbo la hai, kupitia Mbunge wetu, ameweza kusemea, kuhamasisha na hatimaye kufanikiwa katika ujenzi/upanuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Hai, Vituo vya afya na Zahanati. Kwa sasa Wananchi wanapata huduma ya afya bila changamoto yoyote na kwa ukaribu zaidi. Haya yote yasingewezekana bila jitihada za Mbunge. Haya ni matunda ya uongozi makini na ufatiliaji wa kina unaofanywa na Mbunge wetu Mhe. Saashisha Mafuwe.

Elimu: Kila Mwanajimbo wa hai anaweza kuelezea hili, shule nyingi zimejengwa katika ngazi ya kata hivyo kuwezesha watoto wetu kupata elimu karibu na maeneo yao. Idadi kubwa ya watoto wanaojiunga na masomo katika shule zetu za awali na sekondari ni matokeo chanya ya Serikali, Chama Cha Mapinduzi na Jitihada Binafsi za Mheshimiwa Mbunge. Haya yote sio rahisi kufanyika pasipokuwa na Msemaji wala Mfuatiliaji.

Uchumi: Kwa wasiofahamu, sisi wakazi wa hai kwa asilimia kubwa tunaishi kwa kutegemea kilimo na viwanda japokuwa vingi ni vile vidogo vidogo. Kwa kuzingatia umuhimu wa Wananchi kujikwamua kiuchumi, Mbunge wetu ameweza kuvalia njuga hali ya Uchumi ya Wananchi wa Hai kwa kuhakisha shughuli za Kilimo na Viwanda ndizo zinakuwa msingi wa kunyanyua kipato cha Mwananchi mmoja mmoja wa Jimbo la Hai.

Leo hii, sote tunaona Kiwanda cha Machine Tools zaidi ya miaka mingi kilikufa na je hao walio pita Katika nafasi zao hawakuona umuhimu wa uwepo wa kufufuliwa kiwanda hicho??

Ø Mashine Tools: Tayari mashine mpya na vifaa vipya vimefungwa na kuanza kazi rasmi. Kiwanda hiki ni muhimu sana kwa wana Hai katika kuibua ajira na kukuza uchumi wa jimbo letu la hai.

🪞Kiwanda cha kuchakata zao la parachichi kinaenda kujengwa hapa hai.

Ø Mashamba ya Vyama vya Ushirika: Kwenye hili, hakuna mwanajimbo asiyetambua ni kwa kiasi gani kuyumba kwa mashamba haya kulifanya uchumi wa Wanahai kudidimia. Jitihada za Mbunge katika kusimamia ufufuaji wa mashamba ya ushirika, umeleta msukumo mkubwa wa kunyanyua uchumi wa Wanahai.

Ø Kilimo cha Umwagiliaji: Sote tulishuhudia usimamizi hafifu wa ulinzi na usalama wa Mifereji mikuu ya maji hivyo kudumaza shughuli za kilimo katika jimbo letu. Leo hii kupitia jitihada za Mbunge, skimu mbalimbali za umwagiliaji zimeibuliwa kupitia usimamizi madhubuti wa mifereji hii. Mbunge anashinda mitaani kufanya kazi hiyo ili walau kilimo cha umwagiliaji kiendelee na kuleta ukombozi kwenye uchumi wetu. Hivi tunataka nini Wanahai????????

Ø Mazao ya Mkakati: Wote ni mashuhuda mazao tegemezi kama kahawa yalikosa usimamizi kabisa lakini kupitia Mbunge wetu Ndugu Saashisha Mafuwe, tumeanza kuona akiingia vijijini kuhamasisha wakulima warejee shambani huku akisaidia katika utafutaji wa masoko. TaCRI pamoja na Shirika la Red Cross ni mifano hai katika uwekezaji kwenye mashamba ya ukanda wa tambarare wakifanya kilimo cha mazao ya kimkakati.

*Kwa hatua hizi chache na muhimu, Wanahai tunapaswa kukiri na kuamini kuwa Saashisha Mafuwe ni mpambanaji wa kweli na anayejua changamoto za Wanahai. Na bado tutamuhitaji leo, kesho na kesho kutwa kwa matokeo chanya ya Wilaya na Taifa kwa ujumla.

Rai yangu kwetu sisi sote tutambue, tuthamini mazuri haya yanayo fanywa na Serikali yetu katika Jimbo letu kupitia jitihada za Mbunge wetu Mhe. Saashisha Mafuwe. Ni ukweli usiopingika kuwa bila yeye kusema shida za jimbo letu tusinge pata mengi mazuri ndani ya Jimbo hili. Ni wakati sasa wa kuweka kando hisia na mahaba binafsi ya kisiasa ili kupata maendeleo halisi yanayogusa maisha yetu ya kila siku. Tuachane na harakati za makundi ya kisiasa, usengenyaji, wivu na zaidi upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu wasiolitakia mema jimbo letu la hai. Tumpe moyo Mbunge wetu na tumsaidie katika kuhamasisha shughuli za maendeleo katika jimbo letu. Hai ni muhimu zaidi kuliko maslahi ya kisiasa ya baadhi ya watu.

Sisi wananchi wa Hai tunapenda kuona tunapata huduma bora katika tasnia ya Maji, Elimu, Afya, Barabara na shughuli zote za kiuchumi zinazogusa Kilimo, Masoko, Viwanda ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira pamoja na uinuaji wa Uchumi wa mtu mmoja mmoja kwa wakazi wote wa Jimbo la Hai. Hatupendi si kuwa sehemu ya wachache wanaokaa na kuangalia udhaifu wa mtu usiokuwa na maslahi mapana ya Wanajimbo.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Wilaya yetu ya Hai,
Mungu Mbariki Mbunge wetu, tunakuomba uumpe nguvu na moyo thabiti wa kuendelea kulipambania Jimbo letu kwa matokeo chanya ya ustawi wa Wanahai.

Bariki Viongozi wetu wa Wilaya ya HAI wakiongozwa na Mkuu wetu wa Wilaya Ndugu Juma Irando pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya Ndugu Upendo Wela na Viongozi wote wanaohudumia wanahai katika ofisi mbalimbali.Mungu wabariki mno.
 
Hakuna shida sanduku la kura litaamua 2025. Naona ameanza kampeni mapema sana
 
Wewe ni mbunge wa viti maalumu,aliyewspitisha hayupo,2025 hata ukichukua fomu jina lako litakatwa na wajumbe.

Hata wewe unashangaa kuwa mbunge.
 
Ni Mbunge Imara na Mwenye Maono Mapana ya Jimbo lake

Anaandika Madam Rose Matemu

Mhe. Saashisha Elinikyo Mafuwe, katika kipindi chake cha Uongozi, ameweza kuonyesha njia kwa kuwa msimamizi mzuri, msemaji, mfuatiliaji na mhamasishaji wa shughuli za Maendeleo katika jimbo letu la Hai. Mbali na kuwa Kiongozi wa watu lakini ameweza kujenga ukaribu mkubwa na Wananchi wa Jimbo lake la hai kwa kuwasikiliza, kutatua ama kuwasilisha changamoto zao kwa Mamlaka husika ama kupitia jukwaa la Kibunge.

Mbunge huyu ameweza kusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika muda wake mfupi tu wa Uongozi;

Miradi ya Maji: Ameweza kuibua miradi mbalimbali ya maji kwa kushawishi Mamlaka kutimiza wajibu wake kama ilivyo katika ilani ya Chama cha Mapinduzi. Mbunge wetu ameonekana mara kadhaa bungeni akipigania miradi hii ikamilike kwa uharaka, hivi majuzi amefanikiwa kuwasha kukamilika kwa mradi wa Kikafu na sasa tunapata maji jambo lililokuwa limeshindikana kwa zaidi ya miaka 20 ya watangulizi wake. Hii ni kutoka na ufuatiliaji wake wa mara kwa mara wa Mbunge wetu.

Leo hii katika Jimbo la hai, changamoto ya huduma ya maji safi na salama kwa Wanachi imepungua kwa kiasi kikubwa sana. Zaidi ya Kata zote katika jimbo la Hai huduma hii ya ni ya uhakika, na bado anaendelea kupambana kuhakikisha changamoto hii ya maji inakuwa historia katika Jimbo la Hai. *Hakika ni Kiongozi mwenye kuacha Alama.

Miundo Mbinu ya Barabara: Hali ya miundombinu ya barabara imeimarika katika jimbo la hai. Maeneo mengi ndani ya jimbo na kata zetu kwa sasa yanafikika kiurahisi kutoka na matengenezo ya mara kwa mara ya barabara zetu katika kiwango cha lami na changarawe. Hivi ni nani asiyeona hili katika Jimbo letu?

Huduma za Afya:
Leo hii katika jimbo la hai, kupitia Mbunge wetu, ameweza kusemea, kuhamasisha na hatimaye kufanikiwa katika ujenzi/upanuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Hai, Vituo vya afya na Zahanati. Kwa sasa Wananchi wanapata huduma ya afya bila changamoto yoyote na kwa ukaribu zaidi. Haya yote yasingewezekana bila jitihada za Mbunge. Haya ni matunda ya uongozi makini na ufatiliaji wa kina unaofanywa na Mbunge wetu Mhe. Saashisha Mafuwe.

Elimu: Kila Mwanajimbo wa hai anaweza kuelezea hili, shule nyingi zimejengwa katika ngazi ya kata hivyo kuwezesha watoto wetu kupata elimu karibu na maeneo yao. Idadi kubwa ya watoto wanaojiunga na masomo katika shule zetu za awali na sekondari ni matokeo chanya ya Serikali, Chama Cha Mapinduzi na Jitihada Binafsi za Mheshimiwa Mbunge. Haya yote sio rahisi kufanyika pasipokuwa na Msemaji wala Mfuatiliaji.

Uchumi: Kwa wasiofahamu, sisi wakazi wa hai kwa asilimia kubwa tunaishi kwa kutegemea kilimo na viwanda japokuwa vingi ni vile vidogo vidogo. Kwa kuzingatia umuhimu wa Wananchi kujikwamua kiuchumi, Mbunge wetu ameweza kuvalia njuga hali ya Uchumi ya Wananchi wa Hai kwa kuhakisha shughuli za Kilimo na Viwanda ndizo zinakuwa msingi wa kunyanyua kipato cha Mwananchi mmoja mmoja wa Jimbo la Hai.

Leo hii, sote tunaona Kiwanda cha Machine Tools zaidi ya miaka mingi kilikufa na je hao walio pita Katika nafasi zao hawakuona umuhimu wa uwepo wa kufufuliwa kiwanda hicho??

Ø Mashine Tools: Tayari mashine mpya na vifaa vipya vimefungwa na kuanza kazi rasmi. Kiwanda hiki ni muhimu sana kwa wana Hai katika kuibua ajira na kukuza uchumi wa jimbo letu la hai.

🪞Kiwanda cha kuchakata zao la parachichi kinaenda kujengwa hapa hai.

Ø Mashamba ya Vyama vya Ushirika: Kwenye hili, hakuna mwanajimbo asiyetambua ni kwa kiasi gani kuyumba kwa mashamba haya kulifanya uchumi wa Wanahai kudidimia. Jitihada za Mbunge katika kusimamia ufufuaji wa mashamba ya ushirika, umeleta msukumo mkubwa wa kunyanyua uchumi wa Wanahai.

Ø Kilimo cha Umwagiliaji: Sote tulishuhudia usimamizi hafifu wa ulinzi na usalama wa Mifereji mikuu ya maji hivyo kudumaza shughuli za kilimo katika jimbo letu. Leo hii kupitia jitihada za Mbunge, skimu mbalimbali za umwagiliaji zimeibuliwa kupitia usimamizi madhubuti wa mifereji hii. Mbunge anashinda mitaani kufanya kazi hiyo ili walau kilimo cha umwagiliaji kiendelee na kuleta ukombozi kwenye uchumi wetu. Hivi tunataka nini Wanahai????????

Ø Mazao ya Mkakati: Wote ni mashuhuda mazao tegemezi kama kahawa yalikosa usimamizi kabisa lakini kupitia Mbunge wetu Ndugu Saashisha Mafuwe, tumeanza kuona akiingia vijijini kuhamasisha wakulima warejee shambani huku akisaidia katika utafutaji wa masoko. TaCRI pamoja na Shirika la Red Cross ni mifano hai katika uwekezaji kwenye mashamba ya ukanda wa tambarare wakifanya kilimo cha mazao ya kimkakati.

*Kwa hatua hizi chache na muhimu, Wanahai tunapaswa kukiri na kuamini kuwa Saashisha Mafuwe ni mpambanaji wa kweli na anayejua changamoto za Wanahai. Na bado tutamuhitaji leo, kesho na kesho kutwa kwa matokeo chanya ya Wilaya na Taifa kwa ujumla.

Rai yangu kwetu sisi sote tutambue, tuthamini mazuri haya yanayo fanywa na Serikali yetu katika Jimbo letu kupitia jitihada za Mbunge wetu Mhe. Saashisha Mafuwe. Ni ukweli usiopingika kuwa bila yeye kusema shida za jimbo letu tusinge pata mengi mazuri ndani ya Jimbo hili. Ni wakati sasa wa kuweka kando hisia na mahaba binafsi ya kisiasa ili kupata maendeleo halisi yanayogusa maisha yetu ya kila siku. Tuachane na harakati za makundi ya kisiasa, usengenyaji, wivu na zaidi upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu wasiolitakia mema jimbo letu la hai. Tumpe moyo Mbunge wetu na tumsaidie katika kuhamasisha shughuli za maendeleo katika jimbo letu. Hai ni muhimu zaidi kuliko maslahi ya kisiasa ya baadhi ya watu.

Sisi wananchi wa Hai tunapenda kuona tunapata huduma bora katika tasnia ya Maji, Elimu, Afya, Barabara na shughuli zote za kiuchumi zinazogusa Kilimo, Masoko, Viwanda ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira pamoja na uinuaji wa Uchumi wa mtu mmoja mmoja kwa wakazi wote wa Jimbo la Hai. Hatupendi si kuwa sehemu ya wachache wanaokaa na kuangalia udhaifu wa mtu usiokuwa na maslahi mapana ya Wanajimbo.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Wilaya yetu ya Hai,
Mungu Mbariki Mbunge wetu, tunakuomba uumpe nguvu na moyo thabiti wa kuendelea kulipambania Jimbo letu kwa matokeo chanya ya ustawi wa Wanahai.

Bariki Viongozi wetu wa Wilaya ya HAI wakiongozwa na Mkuu wetu wa Wilaya Ndugu Juma Irando pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya Ndugu Upendo Wela na Viongozi wote wanaohudumia wanahai katika ofisi mbalimbali.Mungu wabariki mno.
andika yooooooooooooooooooooooooooote, penye uchguzi wa haki mbele ya Mbowe /chadema anaondoka. Mwisho .
 
Miradi yote uliyoandika ni miradi ya fedha za Covid na Tozo ipo nchi nzima, sasa wewe mbunge huna ushawishi wowote kuileta jimboni na unajipigia debe tuu
Kama mwanachama mpya labda hujasoma uzi mwingine hapa,unao kutuhumu kutumia fedha zote za Jimbo kwenye kata ya nyumbani kwenu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom