Kwani hawezi kutokea a better person than him? Watu walisema haya haya kwa Mwinyi wakataka aendelee, isingekuwa mwalimu huenda Mwinyi angekuwa rais hadi leo, akaja Mkapa tukasema hayahaya, akaja JK watu wakata akae hadi katiba mpya ipatikane, uzuri JK ni mwanasiasa alijua amani ya Tanzania inasimama kwasababu ya term limit watu wakimchoka rais matumaini yanayobaki ni kusubiri muda wake uishe. Hivi tumeshawahi kujiuliza Mwinyi angeamua kubaki leo tungekuwa na JPM? Who knows what God has in stock for our nation? Huenda ajaye atakuwa bora zaidi ya huyu. Na kiongozi mzuri hufanya yale mazuri katika muda wake wa uongozi na kuwaacha wengine watende mengine mazuri, kiongozi mbovu huamini hakuna binadamu wengine wenye akili ila yeye tu, Na hupenda kung’ang’ania madarakani na mwisho wake huwa sio mzuri. Rais wetu keshatukumbusha mara nyingi tu kuwa hana mpango wa kuendelea muda wake ukiisha, wacha wapiga ramli waendelee ila yeye keshasema. Ikitokea akayageuka maneno yake na msimamo wake basi hatufai. Maana kiongozi mzuri ni yule anayesimamia maneno yake, a man of his words.Wanabodi.
Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu Mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tuu", na kama hiki tunachokiona sasa, sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020, kuna haja kweli ya kufanya tena uchaguzi wa rais?, si tumwache tuu aendelee mpaka pale tutakaapoona tumetosheka?.
1. Pamoja na ukanyagaji wake wa katiba ya nchi, lakini kwa kazi hii nzuri anayoifanya rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kuinyoosha nchi hii iliyopinda kupindukia kwa rushwa, uzembe na ufisadi, hivi kweli Tanzania, tuna haja tena ya kufanya uchaguzi wa rais kwa mwaka 2020?, au tumwache tuu aendelee mpaka 2025? na kama bado anatosha, aendelee tuu?.
2. Jee hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, bila kufanya uchaguzi wa rais, na kumwacha Magufuli kupita bila kupingwa, ili kuokoa muda, pesa na mali?, hivyo Magufuli apewe tuu a walkover ya kuendelea hadi 2025 and beyond?.
3. Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike kwa mujibu wa katiba, hata kama uchaguzi huo ni wastage of time, money and resources?!. Kwani katiba ndio nini hata iheshimiwe hivyo?.
4. Na hiyo 2025 tukimuona Magufuli bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili hiyo katiba yetu ili tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.
5. Kwani katiba ni nini?, si ni kipande tuu cha karatasi?!, ingekuwa katiba ni muhimu kihivyo kama ambavyo watu wanataka kutuaminisha humu, ingekanyagwa kirahisi rahisi na kupuuzwa, huku watu wakiangalia tuu?, nini muhimu zaidi kwa taifa letu Tanzania, kati ya katiba ambayo ni kipande tuu cha karatasi na maamuzi ya rais Magufuli ambaye ni rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu, katika uchaguzi huru na wa haki?.
6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, hivyo kama sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua tunamtaka Magufuli aendelee tuu idefinately, si tunaweza kuiweka tuu pembeni hiyo katiba, na tukaendelea na Magufuli wetu mpaka tutosheke naye?!.
7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana kuliko hata katiba na ndio maana anaweza hata kuikanyaga, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu, na kumwacha aendelee tuu kama Kagame, Museveni na Mugabe?.
8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Kama katiba inakanywa na hakuna kinachofanyika, Jee kuna ubaya kama tutaibadili katiba na Magufuli akapatiwa muda wa kutosha kabisa wa kuinyoosha nchi yetu kama Kagame anainyoosha Rwanda, , Museveni anavyoinyoosha Uganda na Mugabe anavyoinyoosha Zimbabwe?.
9. Na baada ya katiba kukanyagwa, kwa mikutano ya siasa kuzuiwa, jee kuna ubaya wowote kama wapinzani wa Tanzania mkiamua kwa kauli moja msisimamishe tena mgombea urais, haswa kwa kuzingatia the playing field is not level, na badala yake CCM tuu ndio iwe pekee inatoa mgombea urais siku zote kufuatia long eksipirience ya uzoefu wa muda mrefu wa CCM wa kumtoa rais ambaye siku zote huchaguliwa kwa ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huru na wa haki?.
10. Na kufuatia somo la demokrasia ya Kiafrika, na mfano hai wa matokeo ya urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado kweli watahitaji kusimamisha mgombea urais wa kushindana na mgombea wa chama dola, CCM?, yaani by now tumeishajua mgombea wa CCM kwa 2020 ni Magufuli?, kuna chama kiko tayari kumteua mgombea wake kushindana na Magufuli ambaye ni a sitting president, huku kutakuwa ni kugombea au kujifurahisha tuu?!, au hata ikitokea huyo mgombea wa upinzani ameshinda atatangazwa?!.
Hayo ni maswali tuu nimeanza kujiuliza aloud?!.
Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.
Paskali