Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,581
- Thread starter
- #201
Kwa vile taifa letu linatatizo, limepinda vibaya kupindukia, na mtu pekee mwenye uwezo wa kulinyoosha ni yeye, kwa nini tusimuombe Mungu amuimarishe, hata ikibidi kuiweka katiba pembeni, na tuiweke ili kumpatia muda wa kutosha tuinyooshe kwanza nchi. Nimeuliza nini muhimu zaidi kati ya nchi na katiba, au kati ya watu na katiba, hakuna anayejibu. Ninawaeleza watu humu kuwa katiba ni kipande tuu cha karatasi ya mkataba lakini muhimu zaidi kuliko hata katiba ni watu, we the people, ndio tengeneza katiba tunataka nini, tukiona kuna jambo zuri lakini hali po kwenye katiba yetu, tunaibadili katiba na kuliongeza. Ndivyo alivyofanya Nyerere wakati tunaanzisha mfumo wa chama kimoja na ndivyo alivyofanya Mwinyi ile 1992, , hivyo ikitokea we the people tukiona mfumo wa vyama vingi haujawahi kufanya kazi kwenye urais, tunaweza kubadili katiba na kutoa exclusivity ya uurais kwa CCM pekee, na tukaondoa ule ukomo ili kumpa extension of time, kuna ubaya gani?.Kwa maana hiyo ni lazima watanzania tuwe na huruma kwa mwenzetu, 2020 tumsaidie ili apumzike tu asiendelee kujitesa bure maana walio tayari kuongoza bila kulalamika wapo.
PaskaliPaskal