Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,035
- 6,907
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri kwa sauti ya Iron Lady SSH,kiboko ya wanasiasa uchwara.
Moja kwa moja kwenye mada,kuna msemo unasomeka kwamba starehe ya maskini ni ngono,bila shaka unasadifu kwa kasi ya kuzaana inayoendelea kwa mikoa yote ya Kanda ya Ziwa.
Kwa wastani uzazi huko kwenye hiyo mikoa ni wastani wa 4% kwa mikoa yote 7 kitu ambacho ni hatari sana kwa ustawi wa jamii za huko.
Case study ni Mkoa wa Mwanza ambao unakadiriwa kuwa na wakaazi takribani Mil.4 huku growth rate ikiwa 4.1% .Inamaana Sensa ya 2032 huenda Mkoa wa Mwanza utakuwa na Wakaazi karibu Mil.8 huku na ndio utakuwa Mkoa wenye Idadi kubwa zaidi ya Watu Nchini na kutupita Mkoa wa /Jiji la wa Dar es Salaam.Hali hiyo itakuwa hivyo kwa Kanda nzima ya ziwa
Cha kusikitisha sasa ni kwamba ukuaji wa kipato hauendani na ongezeko la watu na matokeo yake itakuwa ni umaskini wa kutisha.Kwa mfano Takwimu za 2020 zinaonesha GDP per Capita ya Mwanza ni 2.6Mil ,ambapo kwa Kanda hiyo nzima ni chini ya hicho kiasi ukilinganisha na Mikoa ya Dar (4.6),Iringa(4.0) na Mbeya(3.7).Tayari kuna umaskini mkubwa sasa huo mwaka 2030 Hali itakuaje?
Ndugu zetu wa Kanda ya Ziwa wanaotakiwa Kusaidiwa hasa kwenye Elimu Ili wapunguze uzazi na wadhibiti Umaskini badala ya kuwajengea madaraja nk . Rasilimali kubwa za Mikoa hiyo ni Migodi ambayo haihusishi watu wengi na ambayo haina uhakika wa sustainability.
Nitoe wito kwa Serikali ilitazame jambo hili kwa jicho la upekee na wasaidiwe kwa maslahi mapana ya Nchi.Takwimu hizo hapo za mwaka 2020 kwa mujibu wa NBS 👇👇