Kwa Kasi hii CCM itaendelea kuwa Mzigo kwa nchi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Kasi hii CCM itaendelea kuwa Mzigo kwa nchi.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Ngandema Bwila, Apr 15, 2011.

 1. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nimefuatilia na kubaini kuwa kasi ya CCM kusikiliza, Kujiuliza, Kujifunza na Kuchukua hatua ni ndogo mno. Mbaya zaidi Wana CCM ni wakaidi sana wanapoambiwa ukweli, huwa wanakuwa wakali na kutoa vitisho kwa wanao wambia ukweli.

  Moja mambo yanayo wafanya wawe goigoi katika kufikia mamamuzi ni Kuabudu na kusujudu watu kutokana na vyeo au pesa zao mfano sasa hivi sasa kila mwana CCM anamsifu Mwenyekiti wao kwa uwamuzi wa kuivunja CC kama vile mwenyekiti huyo ndio amechaguliwa juzi,huku wakijua mwenyekiti ndio amewafikisha hapa.

  CCM imechukua muda mwingi sana kukubali na kuanza kuchukua hatua juu ya mambo mengi kamaifuatavyo-:

  1. Mpasuko wa Zanzibar. CCM wamechukua muda mrefu sana wakikana kuwepo mpasuko huko visiwani hata baada ya kutokea mauwaji na nchi kuzalisha wakimbizi.JK akisema upo wanapongeza.
  2. Kero za Mungano: Mpaka sasa CCM wanadai kero za mungano ni mambo madogo madogo tu. Ladda sasa, baada ya mswaada wa katiba kuchanwa mbele ya Sita, atawapasha kuwa hali ni tete.
  3. UFISADI : CCM wametumia muda na nguvu nyingi na kukana kuwa chama hicho si cha mafidadi huku wakidai ushahidi. Leo kila mtu anakuballi kuwa kuna mafidadi ndani yao na wanawataja kwa majina na idadi. leo tumeambiwa wako 100.
  4. Matumizi ya helikopta : waliiponda CDM kutumia helikopta kuwa ni ghali na ni matumizi mabaya ya rasilimali. Wote ni mashahidi mwakajana walikuwa na helikopta ngapi.
  5. TUME ya uchaguzi na KATIBA: Vyote wanadai havina matatizo mpaka leo.
  kuongozwa na chama goigoi kama hiki kina kana kila kitu na baadaye kinakopi vilevile tena kwa pupa baada ya ubishi wa muda mrefu wakisubili JK aseme wanze kupongeza! Ni hatari na hatutapiga hatua kamwe.
   
Loading...