VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Tangu kuanzishwa kwake,CCM imekuwa ikiunda na kuongoza Serikali za Tanzania. Kwa hilo,CCM haipaswi kutenganishwa na kudumaa kwa uchumi wa Tanzania; kushamiri kwa vitendo vya rushwa na ufisadi na mambo mengineyo
CCM pia,niliyojiunga nayo 1980s,haipaswi kutengwa na mafanikio ya kinchi kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni. CCM ni mmiliki wa mfumo wa kiuongozi katika Tanzania;mfumo wa kiuchumi na mfumo wa kielimu na kitamaduni kwa ujumla.
CCM inabebwa na wanachama wasio na soni. Wanachama wanaoshangilia,bila kuangalia,kila jambo ili mradi tu linapendwa na chama. Bandika-bandua ya kashfa za kitaifa,hasa za kifisadi na kulitia taifa hasara,ni taswira halisi ya CCM na mifumo yake.
CCM na wanachama wake,kwa kashfa zinazoendelea,ilipaswa kujificha kwa soni na si kujibaraguza kama ni mambo mema au ya mbali na mifumo ya kichama. Tumbuatumbua zinazoendelea hazisaidii kukisafisha chama na mifumo yake kwakuwa hata waliobaki ni wafuasi watiifu wa mifumo ile ile
Kwa mfano,ameondolewa Waziri Muhongo Nishati na Madini. Naibu wake Kalemani amebaki vipi ikiwa alikuwa Mkurugenzi wa Sheria Wizara hiyohiyo wakati kashfa ya mchanga wa dhahabu ikimea au ikikua? Au ni kwakuwa wa Chato? Ni mifumo inayosubiri wakati tu
Wanachama wa CCM tungekuwa na soni hata kama chembe ya haradari tungejificha hadi papoe. Hatupaswi kuwa na guts wala integrity ya kusifu kinachofanyika kuuwa wadudu wanaoendelea kuzalishwa na mfumo!
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Songea,Ruvuma)