Kwa kamati hizi za Bunge Sitta na Mwakyembe mikononi mwa midomo ya mamba!!

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Uchaguzi wa Kamati za Kudumu Bungeni umeisha ukiwaacha Mhe. Edward Lowassa na Mhe. Peter Selukamba videdea wa Kamati za Bunge za Mambo ya Nchi za Nje na Miundombinu, respectively. Hii ina maana kuwa Mhe. Lowassa automatically anakuwa bosi wa Mhe. Sitta na vivyo hivyo Mhe. Selukamba anakuwa bosi wa Mhe. Mwakyembe. Nikikumbuka jinsi pande hizo mbili zilivyokwaruzana wakati wa skendo ya Richmond napata hamu ya kujua kitakachojiri kwenye Kamati hizo. Selukamba alijibainisha waziwazi kuwa upande wa Lowassa. Kwa hiyo Sitta na Mwakyembe wamekalia kuti kavu.
 
Kwani kesi iliyofunguliwa kupinga uchaguzi uliompa Selukamba ubunge si bado ipo? Tuombe isikilizwe haraka, maana kuna kila sababu ya kuipoteza kesi hiyo.
 
Back
Top Bottom