sifi leo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 5,014
- 8,364
Uchaguzi wa mwaka huu sioni kama mgombea wa CCM anahitaji au kuonesha nia ya dhati ya kufanya kampeni za kuomba kibarua cha kulisha familia yake kwa miaka mitano tena. Ninachokiona naona mgombea kama kachoka na hataki tena sema analazimishwa utaratibu wa CCM kuwa lazima umalize miaka kumi.
Sioni sura ya bashasha waioneshayo wanafunzi waliotoka chuoni wajapo kufanya interview kuomba ajira.
Naiona sura iliyokunjamana, kiburi na majivuno mengi sishangai pengine ni maumbile yake lakini nadhani kipindi hiki ni kipindi muhimu sanaa kwake kuonesha sura ya Tabasamu kama wafanyavyo wanafunzi wajapo hapo ofisini kwangu Wizarani kuomba kazi.
Ninatambua anaumia sana kutumia Bilioni 300 na zaidi kwa ajili ya Uchaguzi ila hizo ni fedha zetu wote ziache zitafunwe.
Hivi zote za nini kununulia Makopo ya kutumbukiza makaratasi ya watu waliotiwa tiki au kosa?Mimi kama Waziri nasema ni nyingi sana tume itupe mchanganuo wa matumizi ya hizo fedha.
Wagombea tambueni mnaomba ajira habari za kuja mmenuna hatuzitaki.