Kwa jinsi nilivyomuobserve Rais, nakubaliana naye suala la kutohudhuria misiba, tusimlaumu..

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Nimekuwa niki muobserve kwa ukaribu sana mh rais wa jamuhuri yetu ya muunganio, ni mtu mwenye hisia sana, ndiyo we mwangalie kwenye videos akiwa anaongea, ana hisia kali sana, ana hisia ambazo si vyema aende kwenye msiba. maana kwa zile hisia mh anaweza kuangua kilio kikubwa sana.

Kwa jinsi alivyo na huruma kwa watanzania hili anaweza lifanya na nadhani washauri wake wakamwambia "mzee usiwe unaenda maana tunakujua ulivyo na huruma unaweza lia mpaka ukapoteza fahamu"

Watu wanasema eti alipaswa aende kuwaaga wanajeshi waliokufa kule "Congo" (kwanza niulize hili chini chini, hivi ni yeye aliwapeleka? ) kule Bukoba lilitokea tetemo lilitetema watu wakatetemeka na vitu vyao.

Muheshimiwa alijisikia huzuni sana, akajifungia kwanza home akalia kwa siku kadhaa,akalia sana na kuhuzunika mpaka alipohakikisha angalau sasa huzuni imeisha then akaenda Bukoba akiwa sasa kama jemedari. Jemedari hutakiwi kulia mbele za watu utaonesha udhaifu si vizuri kuruhusu hilo. hivyo akaenda bukoba this time akiwa amegangamaa kinyama...akakaza sura na kuongea nao kwa hisia kabisa.wakamwelewa.matatizo yao wakajua namna ya kuyatatua. sasa imagine angelia? ungekuwa msiba wa kitaifa.kila mtanzania ungepishana naye njiani angekuwa analia.anaomboleza. haitakiwi iwe hivyo.

After all lile tetemeko hakulisababisha yeye so sijui kusema "nini na nini" haikuwa sahihi kabisa. Haya mambo tuwe tunapeana tu ukweli yaishe kupakana pakana mafuta hakutusaidii. hivi ndivyo inapaswa kuwa.

Rais anapenda kujumuika na watu lakini hisia zake na huruma zake watu wanaweza kuzichukulia vibaya. Mmewahi mwona Rais analia mpaka anagala gala chini? mnataka itokee hivyo? Mwacheni mheshimiwa ana mambo mengi ya msingi ya kufanya.ni mpenda watu na ndo maana anaongea kwa hisia sometime anafoka akiwafokea mafisadi mpaka wameanza kumwogopa....

kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji. nyie nendeni mwacheni mh achape kazi.hapa kazi tu.
 
watu wana frustrations kama za 'Baba' yao...hata thread hawasomi...mbio Kucomment..

matokeo yake $1000,inakuwa $billion moja,kufumba na kufumbua
 
Back
Top Bottom