Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
- Thread starter
- #201
Mkuu tambua kuwa kuwa hii dawa ilishatengenezwa na ipo na sababu wewe ni mtaalamu na hakika hili unalifahamu. Ni taasisi ya Gilead ya Usa ndio waliitengeneza kwa hiyo ipo. Ndio maana walijaribu hata kuja kuifanyia majribio katika matibabu ya Ebola japokuwa haikuleta ufanisi mkubwa huko Congo na nchi zingine zilizoathirika.Kwa hiyo hii dawa ipo na kwa jina ni Remdesivir. Ila baada ya mlipuko wa Corona virus taasisi ya Gilead ikishirikiana na serikali ya China waliitumia kama majiribio kwenye kliniki mbali mbali huko Wuhan na ikaleta ufanisi. Kwa hiyo kuagiza dawa ambayo imeleta ufanisi japokuwa haujathibitishwa na mamlaka kama WHO n.k sio mpaka ununue. Mnaweza kuagiza hata kwa kuziomba ili ziwasaidie. Na kwa nchi kama China kama zilipelekwa kwenye taasisi kama Wuhan institute of virorogy nafikiri kuna cha ziada walikipata. Hivyo tunaweza kuziagiza iwe Us au China na sisi zitusaidie.Mkuu, duniani kuna taratibu. Ondoa fikra za kujifanyia mambo tu kienyeji tulikozoea sisi kuyafanya.
Fikra hizi ndizo zinazotudidimiza katika nyanja nyingi tu, za kukiuka taratibu na matokeo yake ndiyo haya tunayoona. Ni kama tunarudi kinyumenyume, hata pale tulipokwishaonekana kupiga hatua.
Wachina hawana hiyo dawa ya kuwauzia watu nje ya nchi yao. Hiyo sio mali yao.
Kama walishirikiana na Gilead katika matumizi ya hiyo dawa kiuchunguzi huko kwao, haina maana kwamba dawa sasa ni ya kwao.
Kuna umhimu mkubwa wa kulirudisha taifa letu katika misingi imara. Shule zetu zinatakiwa ziwe na mitaara inayokazia umhimu wa kufuata taratibu katika kila jambo tunalofanya.
Na usije ukadhani sielewi uwepo wa dharura, lakini hata katika hali hiyo ni lazima pawepo na utendaji unaoonekana kutumia akili, sio kukurupuka tu.