Kwa jinsi gani watanzania tulivyo ma hohehahe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa jinsi gani watanzania tulivyo ma hohehahe

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Observer2010, Mar 15, 2011.

 1. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wakati serikali yetu ya Tanzania ikiwa haijiwezi hata kujitosheleza kwa bajeti ya mwaka mmoja, huku mkwere akiwa anachanja anga kila kukicha na mawaziri wake wakiwa kwenye mizunguko isiyoisha inayofilisi kabisa kidogo tulichonacho, benki kuu ya Japan imetoa kiasi cha dola za marekani Bilioni 182 kusaidia katika uchumi wa nchi hiyo baada ya kukumbwa na maafa makubwa ya ya tetemeko la ardhi na Tsunami.


  Ukifanya mahesabu ya haraka haraka, kwa bajeti ya Tanzania ya Mwaka 2010/ 2011 ambayo ni takribani Trilioni 11 za Tanzania almost sawa na dola bilioni 7.3 za kimarekani, hii ikiwa ndiyo bajeti kubwa zaidi katika historia ya nchi yetu, hivyo basi kiasi kilichotolewa na benki kuu ya Japan kutokana na hili janga ni bajeti ya Tanzania miaka takribani 25 !!! Hapo utajua ni jinsi gani Tanzania tulivyo mahohehahe.


  Binafsi sijajua serikali yetu imetoa kiasi gani kukabiliana na janga la mabomu ya Gongo la Mboto. Na pia sijjajua serikali na Benki kuu yetu imewekeza kiasi gani katika kukabiliana na majanga ambayo yanaweza kutokea wakati wowote ambayo yana impact kubwa kwenye uchumi wetu.
   
 2. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  mkwere yupo kwa ajili ya maonyesho si kwa ajili ya kuwatumikia wananchi
   
 3. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,972
  Likes Received: 20,332
  Trophy Points: 280
  Upande wa majanga hapa kwetu huwa ni zimamoto, hakuna mipango inayoeleweka zaidi ya kutegemea michango ya watu na taasisi za binafsi, tumeshuhudia namna ambavyo serikali imechukua muda kuhakikisha wahanga wa g'mboto wanakuwa na mahema yanayofaa nyakati za mvua na jua.
  Tuna mengi ya kujifunza lakini zaidi ni kwa serikali kuwepo kwa ajili ya umma na si watu wachache wanaounda serikali
   
Loading...