Kwa jinsi alivyodhibiti na kuondoa hofu ya Corona, Rais Magufuli aongezewe miaka saba

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Members, Maisha ya Watanzania wengi ni "Hand to Mouth" yaani wanafanya kazi pesa yote inaishia kwenye kula chakula, Watanzania wengi hawana ajira rasmi na ujuzi (unskilled labor) na hawana akiba ya ziada kwa ajili ya dharula(emergency).

Maneno hayo ya kiingereza ndio nguzo ya watu wengi kuhitaji muda wake uongezwe wa kutawala, Maneno hayo ni HAND TO MOUTH, UNSKILLED LABOR na EMERGENCY.

Tishio au hofu yeyote ya kuwafungia Watanzania ndani kisa corona ingetengeneza maisha magumu na njaa kali sana mitaani.

Mwanzoni niliamini katika kufungia watu ndani na hii ilitokana na dhana potofu ya kusoma na kutumia miongozo ya nchi za Ulaya ambazo kufungia watu ndani kumeshindwa vibaya na korona inaendelea kwa kasi.

Ninaunga mkono mabadiliko au hati ya dharula Bungeni kubadilisha kipengele cha katiba kumuwezesha Rais Magufuli aongezewe miaka saba baada ya mwaka 2025.Na hii ni kama shukrani kwa watanzania kuachwa huru waendelee na kazi zao wakati wa mlipuko wa corona.

Ni muhimu Bungeni ipigwe kura ya wazi ya ndio au hapana wakati wa mabadiliko ya kipengele cha muda wa Urais.

Yote haya tutashinda kwa mbinu za kisasa na zilizoboreshwa zaidi, Na hii kura ya kubadili kipengele cha katiba itawaacha wanafiki midomo wazi kwani wabunge tuliowachagua wana imani na Rais Magufuli hakika hii itakuwa landslide Victory au SHiKwaMbi ( Shinda kwa Mbinu) iwe mvua au jua.
 
Wewe ndio kichaa sasa toa hoja zako kumpinga mleta uzi

Hoja hupingwa kwa hoja

Wewe unatoa povu huna point yeyote

Je, Rais Magufuli hajaondoa hofu kwa Watanzania?

Je, Wabunge hawajadili aongezewe muda?

Mkuu kama huna hoja wewe ndie kichaa mwenyewe
 
Ninyi watu tegemezi ni wazi ajira zenu zinategemea Prez Magufuli akiwa madarakani.

Mjifunze kujitegemea, anzisheni miradi, kuna maisha zaidi ya kuajiriwa.

Rais Magufuli kasema hataongeza muda.

Polepole pale bungeni kasema Katiba itaheshimiwa, Magufuli hataingeza.

Tulia Ackson, Naibu Spika naye aliliongelea hili.

Kiherehere chenu ni kuogopa kupigwa chini ndani ya miaka mitano ijayo.
 
Fika pale himo mida ya saa 11 asubuhi uone coster zilivyopangana zikisubiri kuingia moshi kuzika, watu wanazika balaa yakikukuta utakaa kimya
Na hao wanaofanya kiherehere cha kwenda kuzika nao watazikwa wote halafu watakaowazika nao watazikwa wote na kuendelea, yaani ni chain. Na hapo ndipo umuhimu wa serekali kuingilia kati unapoleta maana kwa sababu watu wanazikana kiholela bila ya kujua kwamba wanaambukizana!
 
Hoja hupingwa kwa hoja

Wewe unatoa povu huna point yeyote

Je? Rais Magufuli hajaondoa hofu kwa watanzania

Je? Wabunge hawajadili aongezewe muda
Mkuu kama huna hoja wewe ndie kichaa mwenyewe
Kweli ni rahisi sana kuwatawala Watanzania kwa vile hawajitambui. Hawajitambui kwa kuwa elimu waliopewa kupitia CCM haiwapi maarifa na uwezo wa kuchanganua mambo.

Yaani vifo vyote hivi unavyovisikia bado unampongeza Meko? Kweli ni sahihi kumuamini mtu mmoja aliyesomea kufundisha chemistry chuoni na kuacha kuwaamini mabingwa wa tiba wenye PhD kwenye immunology na virology?
 
Kama wewe ni Sampuli ya Population kubwa ya hii nchi yenye mawazo kama yako basi hata maisha atatawala tu, hata yeye akiondoka atakuja kama huyo, after all inaonekana watu siku hizi mnawakabidhi wengine akili zenu ili wafikiri kwa niaba yenu.
 
Mada zako ni za ajabu sana siku hizi.

Ubaya ni kwamba unapoziandika unaamini kabisa kwamba wasomaji wako wanazielewa kama unavyozielewa wewe.

Basi acha na mimi niweke machache kama nilivyoelewa hoja yako:

1. Tanzania ndio nchi ya kipekee kabisa duniani yenye wananchi wake ni "HAND TO MOUTH" ndio maana ni nchi pekee inayostahili kufanya inavyofanya kuwanusuru wananchi wake.

2. WaTanzania wamejazwa WOGA, ingawa inasemwa madhara ya "woga ni hatari zaidi" kuliko ugonjwa wenyewe.

Kwa hiyo bahati ya waTanzania ni kwamba sasa hivi hawaiogopi corona, ila wanao "woga" mwingine; tena ni woga wa kutisha. Hawa watu wanamwogopa sana kiongozi wao sasa kuliko wanavyouogopa ugonjwa wa corona, kiasi kwamba ikitamkwa tu kwamba aongezewe miaka mingine saba, kwa woga wa watu hawa hakuna atakayehoji lolote.

Kwa hiyo, iktajwa tu "miaka saba" hakuna mwananchi atakayesikika kupinga hilo; kama ambavyo hawakuhoji lolote kuhusu KURA ZAO katika uchaguzi mkuu.

Jambo la kujiuliza ni hili: je corona ikichachamaa na kuwalaza mitaani hawa watu, "woga" wao utaendelea kuwa juu ya kiongozi wao au utageuka na kuwa "waoga" wa corona? Ikifikia huko, je miaka saba itakuwaje?

Lakini ngoja nikutahadharishe juu ya uandishi wa aina hii ulioamua kuufanya ndiyo iwe staili yako ya kuwasilisha maoni yako.
Unavuruga unachokiamini wewe.
 
Mada zako ni za ajabu sana siku hizi.

Ubaya ni kwamba unapoziandika unaamini kabisa kwamba wasomaji wako wanazielewa kama unavyozielewa wewe....
Haya mawazo yako ndio yaliyosababisha wananchi kutoichagua chadema mwaka 2020

Lazima uwe positive
 
Back
Top Bottom