Kwa jina la Liverpool na maajabu ya Instanbul Chelsea bingwa wa UEFA 2020-2021

marcoveratti

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
967
1,693
Chelsea mpoo?

Fainali itapigwa jiji linaloitwa Istanbul, nchini Uturuki.

Kule kwa Sultan Suleiman Khan na Shghazad Mustapha.

Yes! Huko huko kwao Ertugru.

Mkifika pale wanaifahamu timu moja ya England inaitwa Liverpool. Ukisema tu 'The mighty Reds' wanaacha kila kitu na kukusikiliza chochote utakacho waambia kuhusu Liverpool nao wata itikia wakisema "SOYLULAR" yani "watukufu"

Kwa waturuki hasa wakazi wa jiji la Instanbul liverpool sio timu tuu bali ni timu tukufu!

Hawakuamini kitu kilifanywa mwaka 2005 kwenye fainali ya UEFA AC Milan alirudishiwa bao tatu kama amesimama vile.

Nikisema AC Milan namaanisha ile iliyotikisa Ulaya sio hii ya leo waliojazana wavulana wasio jua bolu. AC Milan ambayo kikosini alikuwepo Andrea Pirlo kwenye ubora wake, maestro Ricardo Kaka fundi wa kibrazil na mtu mbaya Gennaro Gattuso mtu wa kazi .

Kwenye Ukuta yupo Paolo Maldini beki bora ya ya muda ote hii ,na pacha wake Allesandro Nesta unamjua Nesta wewe? hawa wakina Van Djik wanapatikana 70 kwa huyo mwanaume mmoja. Juu yupo fundi fulani wa ki-Argentina Hernan Crespo na Andriy Shevchenko achana hii AC Milan.

Ulaya nzima ilisujudu kwao, Ulaya nzima ulipiga goti kwao lakini sio kwa timu inayoitwa Liverpool. Mpaka leo waturuki hawaamini kilichotokea usiku ule wa May 25 2005 nakwambia leo kesho wanataka irudiwe, irudiwe ili waamini!

Hakuna alie amini ile Meza pale jijini Instanbul ilivyo pinduliwa kibabe! na watoto kutoka Mercside chini ya Captain Steven Gelard!
Hao ndio Liverpool watakatifu wa Instanbul Uturuki!

Yes, nimeona niwakumbushe kwasababu binadamu tuna sahau mapema sana!

Kama imani za kidini zinavyo tumia watukufu kuomba wanayo taka yatiimie basi na Chelsea nawakumbusha msi usahau utukufu wa Liverpool jijini Instanbul kuomba jambo lenu litimie.
 
Taarifa zilizonifikia sasa hivi. City wamepata big blow baada ya kiungo mshambuliaji Gundogan(mchine) kupata majeraha alipokuwa akifanya mazoezi kwenye dimba la el dragao. Fernadinho ndio kamsababishia maumivu.

Pamoja na hilo. Chelsea wataadhibiwa kama kawaida. Uwepo wa mahrez, Foden, Silva, sterling, De bruyne wanatosha kabisa kuisambaratisha chelsea.

Game inaisha first half. City 4-1 Chelsea
 
Mkuu goli nying sanaa hizo, wasameee.
 
Mwandish anaish dunia ya peke yake

Fainal n ureno na s uturuk

Ukiwa na jina Kama lako ina takiwa uwe mtu wa kusoma Sana taarifa il kujua mengi
 
Mwandish anaish dunia ya peke yake

Fainal n ureno na s uturuk

Ukiwa na jina Kama lako ina takiwa uwe mtu wa kusoma Sana taarifa il kujua mengi
Hahah shukrani sana nimechelewa kujua huu uamisho wa fainali hii shukrani lwa kunijuza.
 
Back
Top Bottom