Kwa Jina la CCM: Mbunge wa Mtera Lusinde aporomosha matusi Arumeru kumwombea kura Siyoi

Ah.. Nimeisikiliza Na kuiangalia You tube.. Hakika jambo hili lazima liwekwe mezani baada ya Uchaguzi kupita.. Si vijembe vya Kampeni Bali ni zaidi ya Hapo.. Lusinde alikerwa Na Hoja kwamba Mgombea wa Chama chake aliitwa shoga Kwa kutoga maskio.. Of which Sioi ni mwanaume Na mashoga ni wanaume pia, sasa kutumia neno Mimba Kama ni Nuksani Na Kiroja Jukwaani ni kudhalilisha utu Wa mwanamke.. Kwamba Ccm imewatia mimba viongozi Wa CDM, kana kwamba Mtu aliyepachikwa mimba ni Nuksani Na Gundu flan ni kudhalilisha sana utu wa Mwanamke.. Kwanini wasingegombana wanaume wao Kwa wao Na wanawake wao Kwa wao.. Nadhani TAMWA, WAMA Na CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE , lazima jambo Hili liwasilishwe kunakotakiwa.. Mimba ni Udhu, Kudra, Na heri ya mwanamke Na Mtu yeyote hawezi kutumia jukwaa la Uwazi kudhalilisha Jinsia tofauti Na yake mbele ya jamii, si CCM, CHADEMA, CUF Wala Mtu yeyote mwenye mamlaka ya kudhalilisha utu Wa mwingine. .. Maneno Haya yana maana kwamba viongozi wale aliowashutumu Lusinde wote ni Wanawake tu.. So mwanamke ni takataka Flani Isiyo Na maana Wala thamani ndani ya jamii, mwanamke ni Kama katuni .. No no
No malizeni Kampeni zenu ila Kwa hili halivumiliki.. Tutaendeshana mahakamani no mater hata ikicost 50 years..
 
Huyo Lusinde na hadhira yake wanazo timamu? Nadhani wana matatizo. kama siasa ni hizo basi hatuna wanasiasa ila tuna watu wanaojua kutukana ... Mpaka sitamani ...

Hivi watoto wake wakimsikiliza matuzi yote hayo na kesho akikuta watoto wake wanatukana wapita njia atuweza kuwakanya???????

Kuna haja ya watu kuangalia shria za nje zinasemaje juu ya mtu anayetukana hadharani maana tunakoelekea si shwari.
 
Ivi hao watoto wa shule na madaftari yao mgongoni wamejifunza nini kutoka kwa Lusinde? Ndivyo anavyowalea watoto wake?

Siasa za Lusinde zimepiliza utu na ubinadamu ... Ni kama ...
 
jamaa amefanya kweli. audio na video ziko vizuri ila kwa sababu ya net bongo ziko slow its better kama utadownload. nenda kwenye google search for FREE YOUTUBE downloader. ukiipata install halafu ukifungua you tube unacopy URL na kuipeleka kwenye youtube downloader ili uihifadhi kwenye computer ili uziangalie taratibu.
 
Hii ni hasara kwa taifa ....anyway kwakua hata mkuu wa inji nae ni wamipasho anaweza aione kua ni shida ....ila sipati picture nikiifikiria Tanzania ijayo itakua ya aje aisee...
 
Hii ni hasara kwa taifa ....anyway kwakua hata mkuu wa inji nae ni wamipasho anaweza aione kua ni shida ....ila sipati picture nikiifikiria Tanzania ijayo itakua ya aje aisee...

Tunajua kuwa Lusinde na CCM yake wamefilisika kisiasa lakini kinachouma hapa ni hawa watoto wadogo waliojazana ktk mkutano huu kwani hawastahili kusikia matusi kama haya.
 
Taifa lina khali ngumu sana kama ndo viongozi hawa

 
Last edited by a moderator:
Kudadadeki?ooh jamani huyu ni Mbunge wa wapi?

anawakilisha wananchi wa jimbo la Mtera, Dodoma. Aibu, aibu, hizo ndo akili za wabunge wa chama cha magamba! Mbayuwayu watupu. Kweli Mzee Malecela alishindwa na huyu mpuuzi kwa siasa zao za makundi na sio tofauti ya uwezo wa kujenga hoja.
 
Hii ni dalili ya desperation. Nina hakika kuwa kama CDM ndiyo wangekuwa wametoa matusi hayo jukwaani basi either Tume ya uchaguzi au polisi ingeingilia kati.

Kinachonisikitisha mimi ni kuwa huyu anayetukana hivi ni Mbunge wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, anawakilisha wananchi wenye akili zao. Kutukana matusi ya namna hii jukwaani mbele ya watoto ni matusi makubwa sana kwa mtu kuitwa mbunge na mbaya zaidi kuwa mbunge wa CCM au mwanachama wa CCM.
 
Kajinga haka kaLusinde, kalikuwa CDM akapata safari ya kwenda ujerumani kujifunza mambo yahusuyo vijana, kwa kuwa kichwani hamnazo, lugha yenyewe ya kuokota akasingizia tumbo. Lusinde ile sh 720.000/ uliyopewa na cdm ukanunue horn speaker za chama na ukatimkia nayo ccm tunaitaka, pesa ya cdm siyo shamba la bibi.
 
Hata pa kuanzia sina, labda nianze na kazi, ubunge siyo kazi bali ni dhamana tu ambayo wenyewe wakitaka wanakunganya tofauti na kazi kama useremala,uvuvi au udaktari hakuna mtu anaweza kukunyanganya ni kitu ambacho unaweza kuama
nacho saa yoyote na wala hakiitiaji utashi wa watu kuwa nacho. ubunge sio cheo cha kurithi na hata useremala hakuna ambaye anaweza kurithi kutoka kwa baba yake bila ya kujifunza na vilevile ktk issue ya ubunge uwezi kupata ubunge mpaka
watu watake upate na siyo kurithisishana kama miogo. kulingana na maneno yake yale inaonekana lusinde hata kama ni shule
basi itakuwa ni ndefu mno ambayo kwa kweli kwa umri wake anaweza asielewe mpaka kiama.
 
Lusinde siasa kajifunzia chadema si unajua kabla ya kujiunga na CCM alikuwa chadema so anapotray aliyojifunza huko..... Kazi ni kwenu
 
Wewe akili yako haikutoshi.Hajasema Lema kaliwa? hajasema Nyerere kaliwa? Anya ujinga kijana/mzee,CCM Hovyooooooooooooooo

Uko makini wewe! Nilichosemea mwanzo na kukiombea ushahidi ni mada ya mwanzo ambayo imeondolewa hapa. Mada ambayo mletaji alitumia neno 'Lema alifirwa' na sio kaliwa kama ilivyo. Sikuhoji kuhusu matusi mengine. Niliomba mleta mada alete audio yenye neno 'Kafirwa' kama alivyoandika. Naona hukuwepo tangu mwanzo wewe.
 
Back
Top Bottom