Kwa jicho la tatu naliona bunge la 11 kuwa la kihuni sana tena sana

BungelaKatiba2014tz

JF-Expert Member
Feb 18, 2014
1,231
648
Nadiriki kuamini hivyo. Uhuni Wa Bunge la 11 nauona katika sura mbili. Matusi na uzushi.

Uhuru na kinga walionayo ya Bunge nadhani wameitfsiri ndivyo sivyo
Matukio ya kuanzia sakata la RC Wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Sakata la Wema Sepetu Matusi ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na sasa Kinachozungunzwa na Mbunge Wa Nzega, Hussein Bashe na Mbunge Wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe kuhusu tuhuna za Wabunge kutekwa yanadhihirisha sasa Bunge ni la kihuni.

Nakumbuka Sakata la RC Makonda, Mbunge Wa Bunda mjini, Ester Bulaya alisema amepigiwa simu na Makonda akimtishia. Tuhuma hizo hazikuwa ndogo. Makonda amehojiwa na Kamati ya maadili ya Binge na Kwa hakuna dalili zozote zinazoashiria Makonda kuhojiwa juu ya tuhuma za Bulaya. Maana yake zilikuwa ni za kutunga. Uhuni huo.

Sakata la Wema Sepetu kutetewa na Wabunge likazimwa na ujumbe wa sauti wa Mama Wema na Msanii Steve Nyerere Kwa kuwadhihirishia watanzania kuwa ulikuwa ni mpango mkakati kati baadhi ya Wabunge, Mama Wema na Steve Nyerere. Uhuni huo.

Sasa kinachofanywa na Bashe na Zitto Kabwe ni uhuni ule ule Wa kutafuta kick. Eti kuna wameambiwa na Mawaziri kuwa ndani ya Idara ya usalama Wa Taifa kuna kikundi cha kuteka watu na kwamba wao ni walengwa. Hao mawaziri nao ni sehemu ya kikundi hicho cha kuteka watu? Uhuni huo. Katika hili nashauri Serikali ichukue hatua Kali Kwa sababu maana halisi ya Kinga waliyonayo Wabunge ni wazi inatumiwa vibaya.

Bunge limejaa matusi, uzushi uzushi. Limegeuka kuwa sehemu ya kitengo cha propaganda Kwa sababu tu wana kinga Kwa mujibu Wa sheria.

Jicho langu la tatu limeona hivyo.
 
Tena Bashe Leo abanwe aseme ni waziri gani kamwambia kuwa atatekwa!!hili siyo dogo kabisa kwa taifa letu!!waziri/mawaziri huyo /hao wazibitishe madai hayo pasipo na shaka!! Hatuwezi kuendelea kwa kuokota maneno ya mitani !!!
 
Taarifa yako hii imejaa unafiki haina uchunguzi wa kina kujua yanayosemwa ni kweli au sio kweli ,hakuhojiwa ester kwa sababu bunge lina uoga hv wakahoji halafu voda,tigo wanadhibitisha kweli amemtisha then inakuwaje kwa wabunge na kamati zake zenye uongo na unafiki huu
 
Viongozi wengi bungeni wapo "desperate" kuna mambo hayaendi vizuri na sio ubabe wa Dk. Tulia pekee bali mwenendo mzima wa Serikali.

Wabunge wengi ni waoga,wataongea endapo tu wana "interest" na ajenda husika. Tuwasamehe bure maana wengi wetu tunao wakosoa tungefanya vivyo hivyo kama tungekua katika nafasi zao.

Angalizo: Kuna taaluma ya "whistleblowing" na haina mzizi wowote mbali na hulka ya kujitolea,kujiamini na kuishi kwaajili ya wengine. Hatuna "whistleblowers" waliopo wamekosa utashi fulani wa kujua nini mbadala wa kupoteza maneno yao kwa viziwi.
 
Andiko lako limejaa unafiki!
Hii ndio tabia ya ccm kuzuia watu kuzungumza ukweli na kuwaona wanafiki......
Nape sasa hivi anashambuliwa na wanaccm kwasababu akili zimemkaa sawa
Bashe huwa anaonekana mbaya kwasababu huwa anazungumza ukweli....
Ukijua wajumbe wa kamati ya maadili ya bunge ina wajumbe gani huwezi kuandika huo ujinga
 
Nadiriki kuamini hivyo. Uhuni Wa Bunge la 11 nauona katika sura mbili. Matusi na uzushi.

Uhuru na kinga walionayo ya Bunge nadhani wameitfsiri ndivyo sivyo
Matukio ya kuanzia sakata la RC Wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Sakata la Wema Sepetu Matusi ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na sasa Kinachozungunzwa na Mbunge Wa Nzega, Hussein Bashe na Mbunge Wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe kuhusu tuhuna za Wabunge kutekwa yanadhihirisha sasa Bunge ni la kihuni.

Nakumbuka Sakata la RC Makonda, Mbunge Wa Bunda mjini, Ester Bulaya alisema amepigiwa simu na Makonda akimtishia. Tuhuma hizo hazikuwa ndogo. Makonda amehojiwa na Kamati ya maadili ya Binge na Kwa hakuna dalili zozote zinazoashiria Makonda kuhojiwa juu ya tuhuma za Bulaya. Maana yake zilikuwa ni za kutunga. Uhuni huo.

Sakata la Wema Sepetu kutetewa na Wabunge likazimwa na ujumbe wa sauti wa Mama Wema na Msanii Steve Nyerere Kwa kuwadhihirishia watanzania kuwa ulikuwa ni mpango mkakati kati baadhi ya Wabunge, Mama Wema na Steve Nyerere. Uhuni huo.

Sasa kinachofanywa na Bashe na Zitto Kabwe ni uhuni ule ule Wa kutafuta kick. Eti kuna wameambiwa na Mawaziri kuwa ndani ya Idara ya usalama Wa Taifa kuna kikundi cha kuteka watu na kwamba wao ni walengwa. Hao mawaziri nao ni sehemu ya kikundi hicho cha kuteka watu? Uhuni huo. Katika hili nashauri Serikali ichukue hatua Kali Kwa sababu maana halisi ya Kinga waliyonayo Wabunge ni wazi inatumiwa vibaya.

Bunge limejaa matusi, uzushi uzushi. Limegeuka kuwa sehemu ya kitengo cha propaganda Kwa sababu tu wana kinga Kwa mujibu Wa sheria.

Jicho langu la tatu limeona hivyo.

Jicho lako lipi ?? Mwanadamu ana macho 2 tuu ilo la tatu liko wapi??
 
Ila nchi inapita ktk kipindi kigumu sana tunaomba viongozi wenye 'BUSARA NA MAONO' kama vile Mzee Mwinyi, Salim, Warioba, Msuya na Butiku wavunje ukimya kwani tunakoelekea ni giza.
 
Wacha watu watapike nyongo zailizo wajaa....Kwani hujui hii nchi inaendeshwa kwa kiki kuanzia juu..
 
Back
Top Bottom