Kwa jicho la kengeza, naona umoja wa kitaifa haupo tena

mcoloo

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
918
1,401
Kwa yule anayefatilia umoja ulio kuwepo enzi za uongozi wa awamu ya kwanza na akilinganisha na uongozi wa awamu zilizofuata hadi kufikia awamu tuliyo nayo sasa ataona mporomoko mkubwa sana wa umoja wa kitaifa.

Enzi za serikali ya awamu ya kwanza umoja ulikuwa ni nguzo kubwa ya taifa letu, ilifika wakati watanzania wakaitana ndugu kila ulipo pita ulikuwa hukosi kusikia neno ndugu likitamkwa hadi kufikia kuwa kama vile neno hilo kuwa slogan ya taifa letu.

Nakumbuka vita vya kagera vilipotokea umoja na mshikamano wetu kama taifa ulikuwa mkubwa sana, vijana walijitokeza kila pembe ya nchi hii kujiandisha jeshini ili kwenda kulipigania taifa lao kumng'oa nduli na dikteta Iddi Amin Dadaa.

Baada ya hapo yakaja mabadiliko ya mfumo wa kisiasa na tukaingia kwenye mfumo wa vyama vingi, hadi kufikia awamu ya nne ya uongozi katika taifa letu bado tulikuwa na umoja kwa kiasi fulani, kwani mitazamo ya kisiasa kati ya mtanzania mmoja na mwenzake bado haukuleta uhasama Bali ulizaa kitu kama utani mfulani hivi, ukiwa upande wa pili basi unaonekana kama mtani wa yule aliyoko upande wa pili.

Gafla mambo yakabadilika katika awamu hii ya tano , siasa zikatuletea uadui ambao haujapata kutokea, chama kimoja kikaona kuwa kukosolewa kwao nidhambi , tukaanza kuona utekaji wa wanasiasa wa upinzani ukifanyika kwa kasi kubwa, watu wakipotea na wasionekane tena , watu kufunguliwa kesi zenye mrengo wa kisiasa na hadi kufikia kufungwa jela, tumeshuhudia mashambulizi yenye makusudio ya mauwaji yakilenga wana siasa wa upinzani, na hata wananchi wamefikia hali ya kupoteza upendo wa wao kwa wao kisa eti siasa.

Kama tulikubali mfumo wa siasa wa vyama vingi ni lazima ukubali kuwa itafikia muda fulani wananchi watakuchoka na ukiliona hilo tafuta ni kwanini wamekuchoka na sio kuendesha siasa za kibabe kisa tu eti kwa sababu umeshikilia dola.

Usilazimishe wananchi wakupende wakati wanaona huna jipya la kuwafanyia ,toka Uhuru umeshindwa kuondoa kero ya maji wakati nchi imezungukwa na maziwa makubwa pamoja na mito mikubwa takribani kila pembe ya nchi.

Manung'uniko yamejaa nchi nzima ,ufukara unazidi kuongezeka, wafanya biashara wakubwa wameshindwa kuendelea na biashara kwa sababu mfumo wa kodi sio rafiki kwao, kodi imefanywa kama sehemu ya kukomoa na wala sio sehemu ya kukusanya mapato ya serikali kiuhalali.

Wajasiri amali nao usiseme, mama muuza mchicha mwenye mtaji wa shilingi elfu tano unamlazimisha kununua kitambulisho kinacho zidi mtaji wake.
Kuna haja ya kuwakataa wanao tuletea ubaguzi tuwakemee na kuwazomea popote pale walipo.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Wanaishi watu boss shida ni kutobalance kati ya Geita na Chato

Ni wapi Tanzania palipobalansiwa, Hata Arusha na Moshi hazipo sawa, kwani mkoa mmoja ukiwa na sehemu mbili ni vibaya, ni kama Ilala na Kinondoni hapo Dsm
 
Hilo ndo tatizo la makengeza.
 
Tatizo watu wanafikiri kazi ya kujenga umoja wa kitaifa ilimalizwa na Mwalimu Nyerere.

Wakati kazi hiyo inatakiwa kuendelea na kila kizazi.
Ni kazi endelevu; na ajue mwalimu kutufikisha hapo kuna watu walikimbia, waliwekwa kizuizini, waipotezwa, n.k Mkengeza yake yanamuonesha awamu ya Tano. Mpaka mnyooke upumbavu ulikuwa umekithiri.
 
Mimi sitetei uvunjwaji wa haki za kiutu kwa kisingizio cha kujenga umoja wa kitaifa.

Ingawa napenda umoja wa kitaifa, napenda haki za watu pia.

Mawili haya hayana mgogoro usiotatulika kuweza kuwepo kwa wakati mmoja.

Ukifikiri kuna mgogoro huo, na ni lazima haki za watu zivunjwe ili tuwe na umoja wa kitaifa, utakuwa hujafikiri sana tu.

Kwa kweli uvunjwaji wa haki unasababisha watu wanaoonewa kujiona hawana haki katika nchi yao, na manung'uniko yao huvunja umoja wa kitaifa.
 
Ni wapi Tanzania palipobalansiwa, Hata Arusha na Moshi hazipo sawa, kwani mkoa mmoja ukiwa na sehemu mbili ni vibaya, ni kama Ilala na Kinondoni hapo Dsm
Chanzo cha kuendelea kikiwa ni kiongozi basi itafanya watu waanze kuchagua watu wao ili kusogeza maendeleo na wanyama pori hawa Chadema hawajui????
 
Kila Kiongozi apende kwao kuanzia Rais hadi Mtendaji wa kijiji
 
Kwa yule anayefatilia umoja ulio kuwepo enzi za uongozi wa awamu ya kwanza na akilinganisha na uongozi wa awamu zilizofuata hadi kufikia awamu tuliyo nayo sasa ataona mporomoko mkubwa sana wa umoja wa kitaifa.

Enzi za serikali ya awamu ya kwanza umoja ulikuwa ni nguzo kubwa ya taifa letu, ilifika wakati watanzania wakaitana ndugu kila ulipo pita ulikuwa hukosi kusikia neno ndugu likitamkwa hadi kufikia kuwa kama vile neno hilo kuwa slogan ya taifa letu.

Nakumbuka vita vya kagera vilipotokea umoja na mshikamano wetu kama taifa ulikuwa mkubwa sana, vijana walijitokeza kila pembe ya nchi hii kujiandisha jeshini ili kwenda kulipigania taifa lao kumng'oa nduli na dikteta Iddi Amin Dadaa.

Baada ya hapo yakaja mabadiliko ya mfumo wa kisiasa na tukaingia kwenye mfumo wa vyama vingi, hadi kufikia awamu ya nne ya uongozi katika taifa letu bado tulikuwa na umoja kwa kiasi fulani, kwani mitazamo ya kisiasa kati ya mtanzania mmoja na mwenzake bado haukuleta uhasama Bali ulizaa kitu kama utani mfulani hivi, ukiwa upande wa pili basi unaonekana kama mtani wa yule aliyoko upande wa pili.

Gafla mambo yakabadilika katika awamu hii ya tano , siasa zikatuletea uadui ambao haujapata kutokea, chama kimoja kikaona kuwa kukosolewa kwao nidhambi , tukaanza kuona utekaji wa wanasiasa wa upinzani ukifanyika kwa kasi kubwa, watu wakipotea na wasionekane tena , watu kufunguliwa kesi zenye mrengo wa kisiasa na hadi kufikia kufungwa jela, tumeshuhudia mashambulizi yenye makusudio ya mauwaji yakilenga wana siasa wa upinzani, na hata wananchi wamefikia hali ya kupoteza upendo wa wao kwa wao kisa eti siasa.

Kama tulikubali mfumo wa siasa wa vyama vingi ni lazima ukubali kuwa itafikia muda fulani wananchi watakuchoka na ukiliona hilo tafuta ni kwanini wamekuchoka na sio kuendesha siasa za kibabe kisa tu eti kwa sababu umeshikilia dola.

Usilazimishe wananchi wakupende wakati wanaona huna jipya la kuwafanyia ,toka Uhuru umeshindwa kuondoa kero ya maji wakati nchi imezungukwa na maziwa makubwa pamoja na mito mikubwa takribani kila pembe ya nchi.

Manung'uniko yamejaa nchi nzima ,ufukara unazidi kuongezeka, wafanya biashara wakubwa wameshindwa kuendelea na biashara kwa sababu mfumo wa kodi sio rafiki kwao, kodi imefanywa kama sehemu ya kukomoa na wala sio sehemu ya kukusanya mapato ya serikali kiuhalali.

Wajasiri amali nao usiseme, mama muuza mchicha mwenye mtaji wa shilingi elfu tano unamlazimisha kununua kitambulisho kinacho zidi mtaji wake.
Kuna haja ya kuwakataa wanao tuletea ubaguzi tuwakemee na kuwazomea popote pale walipo.

Mungu ibariki Tanzania.
Zipo dalili za Umoja wa kitaifa kufifia/kudidimia.
Niisitushwa na kushangilia kufungwaTaifa Stars, kwa vile tu wanamchukia kiongozi Fulani aliyejitolea kuifuatilia timu Misri.
 
Chadema ndio waliompiga risasi lissu ..Kisha wakampiga risasi Akwilina na baada ya hapo wakatoa report ya uchunguzi Inayosema kwamba risasi ili ruka juu kisha ikakata kona. .......?

Aisee safi sana ' mkuu --- CCM Oyeeeeee
Ni kweli hawa CHADEMA wanaharibu nchi, yaani mali ya umma ufanyia kwao kama yao binafsi hii itasababisha michuano ya uongozi kuwa kikanda mathalani wagombea watasema nani alidhani kuwa Chato itakuwa mji mkubwa kuliko Geita?

Je hii hoja ikitumiwa kwa kila mkoa nchi itayumba sana hawa Chadema
 
Binadamu wanaroho mbaya sana
Screenshot_20190708-181356_TubeMate.jpeg
 
Back
Top Bottom