Kwa Jibu hili la Mzee Butiku nadhani Serikali ya Rais Samia chini ya CCM isione Aibu Kukubali Katiba Mpya kwani kwa sasa haizuiliki kabisa

Swali ( Farhia Middley dakika 45 ITV )

Je, Mzee Butiku Tume za Uchaguzi barani Afrika huwa ziko huru na kutenda Haki katika Chaguzi?

Jibu ( Mzee Joseph Butiku wa MNF )

Ni Akili ya Kawaida tu isiyohitaji Elimu Kubwa kujua ya kwamba Mkuu wa Tume ya Uchaguzi aliyeteuliwa na Rais atathubutu kwenda Kinyume na Yule aliyemteua kuwa hapo.

Kwa Uhondo Kamili wa ' Madini ' ya Mzee wangu huyu ' Genius ' kabisa kutokea ' Uzanakini ' Mkoani Mara ( Musoma ) Joseph Butiku usikose Kutizama Kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV Kesho Jumatatu 31 May, 2021 Saa 3 Kamili Usiku.

Msimamo wangu GENTAMYCINE nami ( japo ni mwana CCM lia lia ) juu ya Katiba Mpya ni ule ule kuwa naitaka tena haraka mno kwani Katiba ya 1977 ina ' Vipengele ' vingi vya Kipuuzi Kipuuzi ambavyo vimepitwa na wakati na haviendani kabisa na Nyakati hii tuliyopo na hata ile ijayo.

Tafadhali wanaotokea Mikoa hii ya Kagera, Singida, Kigoma, Kondoa Dodoma na Ukerewe Mwanza wakichangia Uzi huu wawe na Adabu zote japo itapendeza zaidi kama wakiwa Watazamaji na Wasomaji ili Wasinichoshe ' Kipanga ' wa ukweli kuwahi kutokea Mkoani Mara ( Musoma )

CCM Wenzangu Katiba Mpya muhimu.
Kinachoigharimu tume ya sasa watu kutokuwa na imani ni kuruhusu magoli ya kuotea dhidi ya timu pinzani kwa njia ya mapingamizi.Watazamaji wote bila kujali itikadi au elimu zao,waliamini ilikuwa hujuma.Ndo maana wengi wanapenda tume huru kabisa ili haki iweze kutendeka
 
Suala la katiba mpya mpaka sasa ni kama mwiba, hatuoni kama kuna kiongozi mwenye lengo la kuibadili.
Ukiangalia katiba tuliyonayo ni zaidi ya kuwapa mamlaka viongozi wetu. Ndiposa wanapowaza nikiibadili nitabaki kwenye nyadhifa nilionayo au la.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom