Jumakidogo
R I P
- Jul 16, 2009
- 1,851
- 417
Suala la leseni mpya za kuendeshea magari sasa limekuwa mradi wa watu kwa ajili ya kuwaingizia kipato kutokana na ukweli kuwa haki katika utoaji wa leseni hizo haipo kabisa na kilichopo sasa ni rushwa kwa kwenda mbele.
Pamoja na rushwa hiyo hasa kwa upande wa polisi, lakini pia serikali ingepanga ada ya chini kidogo ili wananchi wengi wanaotegemea udereva kama ajira kwao wapate unafuu wa kuchukua leseni hizo. pamoja na hilo laikini pia kuna mpango wa kuwanyonya wanachi kutokana na muundo wenyewe wa leseni ulivyo na gharama zake.
Katika leseni hiyo kuna vyombo vya barabarani ambvyo vimeainishwa kwa kutofautishwa kutokana na muundo wake yaani kuanzia piki piki hadi magari madogo ya kutembelea.
Kinachosikitisha hapa ni kuwa, kila aina ya chombo linatozwa ada yake. Kwa maana hiyo ukitaka kuondesha aina zote za magari yaliyoainishwa katika leseni hiyo ni lazima ulipe 40000 kwa kila kimoja kisha ujaziwe tiki katika chombo ulichokiombea leseni.
Huo ni uenevu mkubwa ambao unahitaji mtu makini ili kugundua. Haiwezekani dereva wa roli akiwa na gari yake ndogo ya kutembelea alipie leseni ya kuendeshea roli, pia alipie na leseni ya kuendeshea corolla yake ya kutembelea.
Haingii akilini kuwa dereva mwenye uzoefu wa kuendesha roli ashindwe kuendesha gari ndogo ya kutembelea. Au dereva wa basi kubwa la abiria awe na leseni ya kuenseshea basi hilo pia alipie na leseni ya kuendeshea dala dala. Haiwezekani dereva huyo akamudu kuendesha basi hilo kubwa halafu akashindwa kuendesha taxi.
Leseni zilitakiwa kutolewa kulingana na sifa ya deleva mwenyewe katika taaluma hiyo kuanzia ngazi ya chini mpaka ya juu kama ilivyokuwa awali, zaidi kilichokuwa kikitakiwa kubadilika ni muundp wa leseni tu. bila ya kurekebisha suala hili serikali yetu itakuwa imetugeuzi wananchi wake mti wenye matunda...