Kwa jambo hili nitatofautiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Masinki

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
695
461
Yapo mengi sana anayofanya bwana mkubwa Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Christian Makonda. Ni moja ya viongozi mahiri kwenye suala zima la kiungozi ikizingatiwa yupo mkoa ambao unahitaji akili kubwa kwa sababu ni Jiji lenye Kila aina ya vitu na watu.

Jana wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika moja ya agenda alizotoa, ni pamoja na kuonesha yupo mstari wa mbele kutetea haki na usawa kwa wanawake kwa kueleza bayana kuwa atakabiliana vikali na mwanaume yeyote atakayempiga mke wake, na alienda mbali zaidi kwa kutoa namba zake za simu ili kurahisisha jukumu hilo. Hapa sina tatizo naye.

Kilicho nishtua sana na kuniweka kujiuliza bila majibu ni suala hili la kutaka kupeleka muswada bungeni wanawake wapate asilimia 40% kutoka kwa waume zao kwa kila mwezi!

Najaribu kujiuliza itakuwaje kwa rafiki zangu wakulima? Itakuwa vipi kwa vibarua? Je, kwa wenzangu wa ulinzi wanaopokea 80k per month?

Sipati picha wewe Mwalimu rafiki yangu mwenye mshahara wa 350k ulivyoduwaa bila majibu, achilia mbali makato mfanyakazi anayovunjwa kwa mwezi alafu plus no increment kwa maana hiyo tunajiandaa kuwa na payslip tu bila mshahara.

Mkuu wa Mkoa lengo lako ni zuri sana lakini kabla ya kulifikisha huko jaribu kuheshimu wanaume wenzako. Haiwezakani mwanaume utoe huduma zote za ndani kisha ugawe fedha kwa ajili ya mwanamke, wewe unadhani hiyo 40% ukitoa ndio sululuhisho? Tafuta namna nyingine ya kuwasaidia, wapeni mitaji na sisi tutawapa fursa za kufanya kazi.

Acha kuingilia mambo yetu ya ndani maana punde utasikia wake zetu wanadai mishahara yao na hapo ndio ndoa nyingi zitakuwa ndoano. Tutawafanya kama Platnumz tu hakuna namna.

Serikali yetu ni sikivu sana. Hope haitapokea huu muswada. Miaka yote watu wanaishi vizuri, msituletee figisu na habari zenu za siasa.
 
Mleta mada hivi kwani 80k hsina 40%?

Ishu sio wenye mishahara kidogo ishu ni je kwann wanataka kura za wanawake kwa kuwahonga 40% ya mishahara ya waume zao?
 
Huo mshahara wa kugawa 40% ni huu ambao siku ya kulipwa mtu unaona aibu kuuchukulia counter kwa bank teller badala yake inabidi uingine ATM ukauchkue huku ukiangalia nyuma yako kama kuna mtu anachungulia?
 
Hivi huwa kuna cha mwanamke na mwanaume? Mimi najua familia inamiliki kila kitu kwa pamoja. Haya mambo yana lengo la kufarakanisha familia. Kuna wanawake wasio na akili kweli watademand hii.
 
Huo mshahara wa kugawa 40% ni huu ambao siku ya kulipwa mtu unaona aibu kuuchukulia counter kwa bank teller badala yake inabidi uingine ATM ukauchkue huku ukiangalia nyuma yako kama kuna mtu anachungulia?
Kusudio la Bashite ni dhihirisho tosha kwamba alifoji vyeti. Tumhurumie tu. Kihwani hakuna kitu!
 
Back
Top Bottom