Kwa interview hii, bado robo ROMA atausema ukweli juu ya watesi wake!


___________
Ukisikiliza vizuri hii interview, utagundua kuwa, ROMA amebakiza robo kuusema ukweli juu ya tukio la kutekwa kwake.

Kwamba, maswali yalihusiana na nini? Anadai, maswali yalihusu maisja ya kawaida, siasa na muziki. Walimhoji vitu ambavyo anaamini havifanyi. Hivi vitu ambavyo ROMA anaamini havifanyi ni vitu gani? Aidha;

(a) kuuza madawa ya kulevya?
(b) usalama wa taifa aliyeasi?
(c) kutumiwa na upinzani kutukana wakubwa? Au
(d) kushirikiana na upinzani kuikosoa serikali?

Tuviachie vyombo vya dola.

Lakini pia, wakati wanamteka, walisema asijali kuhusu vitu vyake, kuna polisi watakuja kuvichukua.

Je, hawa watesi wana uhusiano wowote na polisi? Je, yawezekana kulikuwa na uratibu baina ya polisi na watesi?

Huyu aliyetaka kumpa deal la tangazo, anamjua. Je, ni kweli ROMA hajamsema huyo mtu kituoni ili kuisaidia polisi?

Yote tisa, kumi ni je, vyombo vya dola vinahusianishaje utabiri wa nabii Kaso na kupatikana kwa ROMA kabla ya jumapili? Wakati Sirro mwenyewe mwenye uzoefu na kazi alisema hana uhakika huo?

Mimi nadhani hapa kuna kitu kikubwa sana. Ningekuwa ROMA, ningeingia makubaliano rasmi na vyombo vya dola kuwa, ifikapo muda fulani, basi upelelezi uweze kuisha ili kama ni kesi basi iende mahakaman. Hii ingeenda saambamba na kuujulisha umma kisa cha kutekwa.

Uncle Kaso

Kama ulimboka na Kibanda hawakudiriki kuwasema waliowateka sidhani kama Roma atasema chochote.....haya mambo ni mazito sana
 
Hawatabiriki hao wasanii,hata maisha yao yakisanii sanii tu. UNAEZA SHANGAA BADALA YA KUWATAJA AKAJA SEMA ANAHAMIA CCM.. Tuwaacheni tu na matumbo yao bhana
 
Back
Top Bottom