Kwa interview hii, bado robo ROMA atausema ukweli juu ya watesi wake!

Hussein J Mahenga

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
745
633

___________
Ukisikiliza vizuri hii interview, utagundua kuwa, ROMA amebakiza robo kuusema ukweli juu ya tukio la kutekwa kwake.

Kwamba, maswali yalihusiana na nini? Anadai, maswali yalihusu maisja ya kawaida, siasa na muziki. Walimhoji vitu ambavyo anaamini havifanyi. Hivi vitu ambavyo ROMA anaamini havifanyi ni vitu gani? Aidha;

(a) kuuza madawa ya kulevya?
(b) usalama wa taifa aliyeasi?
(c) kutumiwa na upinzani kutukana wakubwa? Au
(d) kushirikiana na upinzani kuikosoa serikali?

Tuviachie vyombo vya dola.

Lakini pia, wakati wanamteka, walisema asijali kuhusu vitu vyake, kuna polisi watakuja kuvichukua.

Je, hawa watesi wana uhusiano wowote na polisi? Je, yawezekana kulikuwa na uratibu baina ya polisi na watesi?

Huyu aliyetaka kumpa deal la tangazo, anamjua. Je, ni kweli ROMA hajamsema huyo mtu kituoni ili kuisaidia polisi?

Yote tisa, kumi ni je, vyombo vya dola vinahusianishaje utabiri wa nabii Kaso na kupatikana kwa ROMA kabla ya jumapili? Wakati Sirro mwenyewe mwenye uzoefu na kazi alisema hana uhakika huo?

Mimi nadhani hapa kuna kitu kikubwa sana. Ningekuwa ROMA, ningeingia makubaliano rasmi na vyombo vya dola kuwa, ifikapo muda fulani, basi upelelezi uweze kuisha ili kama ni kesi basi iende mahakaman. Hii ingeenda saambamba na kuujulisha umma kisa cha kutekwa.

Uncle Kaso
 
Amekaa akapima akaona machozi na mayowe ya Raia juu yake kipindi hapatikani yamekuwa mazito sana na hayabebeki tena kama alivyotaka kuyabeba mwanzo kwa kivuli cha Bashite na Mwakyembe via Pombe. Time and Karma is what killing him now.

"PAMBANA NA HALI YAKO"
 
Kamwe hatoweza kusema sema nyie mnapata kiherehere cha bure tuu...wewe ungetekwa ungesema?
Msipende kuyazungumzia msiyoyafahamu,maana mna mlazimisha aseme as if nyie ndio mnajua ukweli kuliko yeye...
Watanzania makelele mengi kuliko vitendo....
 
Kwa alipofikia kwa sasa na ujasiri aloonesha hakuna tena wa kumteka cha msingi nachoona ataombwa asiendelee kutoa siri zaidi. Uzuri wa kusema wazi ndo huo
 
Kamwe hatoweza kusema sema nyie mnapata kiherehere cha bure tuu...wewe ungetekwa ungesema?
Msipende kuyazungumzia msiyoyafahamu,maana mna mlazimisha aseme as if nyie ndio mnajua ukweli kuliko yeye...
Watanzania makelele mengi kuliko vitendo....

Huwa hueleweki aisee, unasemaga haya kwa malipo au tu ndivyo ulivyoumbwa tukuache ulivyo
 
Kamwe hatoweza kusema sema nyie mnapata kiherehere cha bure tuu...wewe ungetekwa ungesema?
Msipende kuyazungumzia msiyoyafahamu,maana mna mlazimisha aseme as if nyie ndio mnajua ukweli kuliko yeye...
Watanzania makelele mengi kuliko vitendo....
Kwani mpaka hapo hujamwelewa? Kuna kilichobaki?
 
Back
Top Bottom