Kwa Imani yangu naamini kila mwezi kuna mtu kutoka Kundi la waloitwa WASIOJULIKANA anaaga Dunia

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Wasiojulikana walifanya ukatili mkubwa sana juu ya binadamu; ghafla mtandao wao ukakosa wakuwaunga mkono na may be hata ahadi walizopewa zikayeyuka. Mwenyenzi Mungu aliumba mwanadamu lakini akumkabidhi mwanadamu Haki na mamlaka ya kuuwa wengine.

Mamlaka ya kisiasa iliyokosa baraka za Mungu umkosoa Mungu nakuhoji uwepo wake; wasiojulikana walimhoji Mungu kama yupo au la. Kutokana na kumhoji Mungu nimekuwa nikitafakari wapo wapi wasiojulikana; sikupata jibu sahihi na naamini sitopata.

Ila ninachoamini ni kwamba hakuna mtesaji na muuaji anayeishi Kwa amani, na ukikosa amani unapata maradhi ikiwemo kisukari na presha au stroke na ukipata magonjwa unayojua Wazi yametokana na ukatili wako hakuna madaktari watakuponya utakufa tu .

Naamini Kila mwezi tunampoteza asiyejulikana, kama ndivyo naamini pia wanakaribia kumalizika. Endapo watamalizika naamini pia mabosi wao watapata hofu na wataugua Baada ya kusikia taarifa za waajiriwa wao wakipotea Duniani.

Hivyo natabiri genge la wasiojulikana awatakula pensheni, maana kitendo Cha kumkosoa muumba sio Cha kuruhusu wapumue Kwa amani. Tuishi Kwa Imani huku tukichunguza viumbe wakatili kwenye maeneo yetu wanavyopukutika .

Karma
 
Kwa imani?! Sote tunajua huwa zipo na imani potofu, yako inaweza pia kuangukia kwenye hilo kundi, unless ulete ushahidi wa kuthibitisha hicho unachokiamini
 
Back
Top Bottom