Kwa idadi hii ya wanachama, CCM Kuondolewa madarakani ni rahisi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa idadi hii ya wanachama, CCM Kuondolewa madarakani ni rahisi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MchunguZI, Aug 9, 2010.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kwa miaka mingi CCM kimejivuna kwamba ni chama kikubwa na chenye wanachama wengi zaidi ya vyama vingine, lakini ktk chaguzi hizi zilizopita, Ktk majimbo yote hakuna hata jimbo moja lililokuwa na wanachama wapiga kura wanaofikia 20,000! Baadhi ya majimbo idadi iliishia 7,000 tu! Hii inanipa ishara kwamba idadi kubwa ya wapiga kura wako nje ya CCM.

  Naelewa pia kwamba idadi hiyo ilifikiwa baada ya kadi mpya kutolewa kwa kasi sana, ina maana hapo nyuma idadi ya wana-CCM wenye kadi ilikuwa ndogo sana.

  Hakuna haja ya kuwashawishi wajiulize ni kwa nini Wananchi wengi hawavutiwi kujiunga na chama hicho lakini Kama CCM haitabadili mtindo wa kuomba kura kwa kutumia chama, kumbe wale ambao siyo wanachama wake wana nguvu ya kukiondoa madarakani.

  Tuombe uchaguzi wa haki usiokuwa na kura za bandia.
   
 2. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Bwana Muchunguzi, kuna wanachama wengi sana zaidi ya milioni 10 Tanzania nzima ambao hawakupiga kura kutokana na sababu kadha wa kadha.
  Kwa hivyo basi hili lisikupe uhakika wa kuiondoa CCM madarakani.

  CCM Hoyeee eeeeeeeeeeeeeeee !
   
 3. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Millioni 10!!
  Naona unakumbuka wale waliolazimika kutafuta kadi miaka ile ya maduka ya ushirika. Kuna wakati pia kadi ya CCM ilikuwa ni kibali cha kujiunga na chuo kikuu. Wanachama wa aina hiyo hawapo tena! Ndo maana waheshimiwa wamegawa kadi mpya.

  Kama wapo na hawakupiga kura kwa wingi kiasi hicho, wewe kama katibu wa chama hiki lazima uelewe ni ishara ya kitu gani.
   
 4. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Takwimu zako naona zina kasoro Makamba anasema wanachama wa CCM nchi nzima ni 4m,tena idadi hiyo inawezekana kuhusisha hata waliokufa na walihamia vyama vya upinzani, sasa wewe hiyo ya kumi unaitoa wapi?
   
Loading...