Kwa huu uzushi Serikali ipige marufuku mahindi kwenda Kenya, badala yake mahindi ya ziada yatumike kuzalisha vyakula vya mifugo

Hili swala ni dogo wala halipaswi kukuzwa hivi.
Suluhu ni wataalzmu kutoka Kenya na Tanzania wangepima sample chache na waseme walichoona.
Pili wafanye uchunguzi kuhusu ununuzi, uhifadhi na usafirishaji na muda.
Wakulima na wafanya biashara wanaumia huku wakubwa wanalumbana. Haisaidii zaidi ya kuzidisha bifu.
Apo umenena
 
Hivi karibuni kumetolewa madai na kenya kuhusu mahindi yetu kuwa na sumu kuvu. Swala la milipuko ya watu kuugua na kufa kwa kula mahindi yenye viwango vya juu vya aflatoxin limekuwepo nchini kenya tangu mwaka 1981. Mfano, mwaka 2004 wakenya 317 waliugua na 125 walifariki kutokana na kutumia mahindi yenye viwango vya juu vya sumu kuvu aina ya aflatoxin.

Chanzo cha tatizo yalikuwa ni mahindi yaliyokuwa yamezalishwa na wakulima wenyewe na kuhifadhiwa katika mazingira mabovu. Kwa hiyo utaona hayo mahindi hayakutoka Tanzania.

Nchini kenya kumekuwa na kawaida ya Wafanyabiashara wakubwa kuagiza na kuhodhi mahindi kwa muda mrefu hali inayopelekea sumu kuvu kuendelea kuzalishwa yakiwa yamehifadhiwa, na baadaye kutolewa kwa bei chee kwa watu maskini ambao wanakuwa wamekumbwa na uhaba mkubwa wa chakula, na hivyo kutokea milipuko ya aflatoxin.

Haiwezekani uagize na kuhifadi mahindi, miaka mitano baadaye useme hayo mahindi yenye aflatoxin yametoka Tanzania. Utafiti umeonyesha mahindi yaliyovunwa maeneo mbalimbali nchini Tanzania yana viwango vya chini sana vya aflatoxin ambavyo ni chini ya viwango vya wastani vinavyopendekezwa na mamlaka za usalama wa chakula nchini Tanzania.

Kenya wanapokuja na tuhuma zisizokuwa na mashiko maana yake wana ajenda nyingine ambazo wanakuwa wamebeba na hii si mara ya kwanza. Kwa hiyo ili kuweka mazingira ya kuheshimiana ni bora serikali ichukue hatua mathubuti dhidi ya hizi sarakasi za kila mara kutokea Kenya.
Jibu tuhuma acha kuandika utopolo,mahindi yenu yamejaa sumu mle wenyewe mataga kwanza
 
Serikali ipi? kwani kila mwaka si huwa wananunua kwa kumkopa mkulima? kwa shilingi 500@kilo!? Mwaka juzi nilikuwa mkoa wa katavi, NFRA, hawapati watu wa kupeleka mahindi, yaani mkulima aache kuuza kwa cash, apeleke akakopwe tena kwa bei iliyochini ya bei ya soko? Tusidanganyane serikali haina uwezo wa kununua mahindi yote yalimwayo nchini!!
Ukweli mtupu, hayo mahindi ya kulisha mifugo, serikali ilime mashamba yake, ni mara mia mkulima auze 30,000 gunia cash mkononi, kuliko kukopwa kwa sh50,000 gunia na serikali ambayo kila siku mtaambiwa inahakiki madeni.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Mawazo finyu kabisa, lakini hey watu kama nyinyi ndio mnaopewa uongozi maana badala ya kutumia akili na diplomasia na kuangalia kila jambo kwa upeo mkubwa mnakurupuka tu na kutoa amri za ajabu ajabu.
 
Mmelazimishwa kuwauzia wakenya?
Hujawahi kumwona hapa waziri wa kilimo wa kenya akija kuomba mahindi? naona kwa sasa wamefanikiwa kudhibiti njaa huko kwao, muda utaongea.....natarajia serikali ianze mapema kuchukua hatua madhubuti..
 
Hujawahi kumwona hapa waziri wa kilimo wa kenya akija kuomba mahindi? naona kwa sasa wamefanikiwa kudhibiti njaa huko kwao, muda utaongea.....natarajia serikali ianze mapema kuchukua hatua madhubuti..
Unaombea wapate matatizo lakini nyie hamtaki wa kwenu apate matatizo
 
Ukweli mtupu, hayo mahindi ya kulisha mifugo, serikali ilime mashamba yake, ni mara mia mkulima auze 30,000 gunia cash mkononi, kuliko kukopwa kwa sh50,000 gunia na serikali ambayo kila siku mtaambiwa inahakiki madeni.

Everyday is Saturday............................... :cool:
Hili ni genge la wanya'nganyi
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom