Kwa huu uchakachuaji sijui muundo wa wizara utakuwaje

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
2,000
Hivi ndg zangu watanzania, kama CCM inadiriki hata kuchakachua majina ya wanaowania uspika kwa staili hii, itakuwaje kwa muundo wa wizara?

Wakati wanatangaza kwa wenye sifa ya kugombania uspika hawakueleza kuwa anayetakiwa ni mwanamke. Lakini ili wakamilishe malengo yao ya kumwondoa Sitta, wakaamua kusema eti wanataka mwanamke.

Sitashangaa kusikia kuwa hata kwenye wizara hawatakuwepo wapiganaji kama akina Magufuli, Mwandosya.
 

Anko Sam

JF-Expert Member
Jun 30, 2010
3,203
1,195
Kuchakachua huko ndiko kunako ipeleka CCM kuparaganyika. We subiri utaona!
 

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
0
JK anaamini hana cha kupoteza (anajidanganya) kwa kuwa ni kipindi chake cha mwisho - hivyo anaweza kumalizia kulipa fadhila kwa washikaji kwenye baraza jipya la mawaziri. Tusubiri tuone! Ni kweli hakuna mantiki ya kuchezea akili za watu kwa kusema yeyote anaweza kugombea wakati mnajua mlengwa ni mwanamama. Kwa nini usiseme safari hii wagombea wawe kina mama tu? Hii Makambaism_Jakayaism itatupeleka pabaya!
 

rmb

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
223
195
Wanamlipa fadhila mzee six kwa alichowafanyia alipokuwa kakalia kiti
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
2,000
Form za kugombea uspika hazikuwa zinatolewa bure, ilikuwa inauzwa laki5. Nadhani walikuwa na shida ya kama m3 ndiyo maana hawakutangaza mapema kuwa spika anayetakiwa ni kilaza. Sijui akina Makamba watachezea akili za watu mpaka lini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom