Kwa huu mfumuko wa bei ya bidhaa karibu zote nchini Serikali inapaswa kujiuzulu haraka sana

Kila kitu holela, bidhaa aina zote bei juu na ni ndani ya muda mchache sana, serikali imeshindwa kazi, ijiuzulu.

Mwaka jana pamoja na kovidi kutisha kwa kiwango cha hali ya juu hatukuwa na mfumuko wa bei kiwango cha sasa.

Inaonekana Serikali tayari mikononi mwa walanguzi
CCM wanaandaa maandamo kumpongeza Mhe Rais kwa kudhibiti mfumoko wa bei
 
Nilimsikia madelu anasema pesa zitamwagwa mtaani, kwa walioshuhudia huko zilikomwaga watushtue.....maana wengine tunaambulia za uso tu, tunaenda mwaka wa kumi mshahara ule ule kiduchu.
 
T

Siasa ni mchezo wa zamani sanaa yaaani unawasha moto uchome jengo unazunguka kwa nyuma unaenda kupiga mayowe nyumba inaungua halafu unajumuika kuzima tena uleule moto uliouwasha.Sahizi hatuwezi dangaywa tena.
Mtafanya nini sasa? katiba mbovu sn hii
 
Na mkate umepunguzwa uzito, ila ujazo ni ule ule (sponji kavu), kwa buku ile ile. Vibaraka wanachekelea, kama vile watakalia hayo mamlaka milele.
Turudi kwenye mihogo tuwaachie sponji zao. Haya madawa ya kufanya sponj yatatuua
 
Na mkate umepunguzwa uzito, ila ujazo ni ule ule (sponji kavu), kwa buku ile ile. Vibaraka wanachekelea, kama vile watakalia hayo mamlaka milele.
Ila mkate standard unatakiwa uwe gram 500 yaani nusu kilo.
Wiki moja tu unga kg 25 umepanda kutoka 19,000 hsdi 25,000 leo
 
Ni kitu gani kimechangia mfumuko wa bei. Ni Mzunguko wa pesa umeongezeka au bei ya mafuta?
Bei za vyakula ni sababu ya kuwepo kwa ukame na ongezeko la bei ya mafuta.
Pamoja na mafuta kupanda duniani kodi za mafuta ni nyingi na ni tatizo.
 
Mimi najiunga rasmi na Sukuma Gang. Siwezi kuvumilia kuona msimamo wa Magufuli kuhusu bei za bidhaa zinazotumiwa na wanyonge ukipuuzwa.
 
Hii ni serikali ya WALANGUZI na wameuonesha UMMA wa WATANGANYIKA waziwazi kwamba wao ni walanguzi maana hawazungimzii chochote juu ya gharama za maisha kupanda kwa kasi kubwa.LEO KWENYE HUU UHURU WAO WANAZUNGUMZIA SANA AMANI NA INAONESHA HAWATAKI KUSIKIA NENO LINAITWA HAKI AMBALO NDIO BABA WA AMANI.Kuendelea kusheherekea sherehe kama hizi huku maisha wa watanzania yakiendelea kuwa magumu ni upumbavu mtupu tena uliopitiliza.
 
Kila kitu holela, bidhaa aina zote bei juu na ni ndani ya muda mchache sana, serikali imeshindwa kazi, ijiuzulu.

Mwaka jana pamoja na kovidi kutisha kwa kiwango cha hali ya juu hatukuwa na mfumuko wa bei kiwango cha sasa.

Inaonekana Serikali tayari mikononi mwa walanguzi
Kila tatizo ni fursa, tunapaswa tuzitumie fursa zinazotokana na "mfumuko wa bei" kuzifanya mafanikio.

"Necessity is the mother of invention" Uhitaji (umuhimu) ni mama wa uvumbuzi.

Kupanda (mfumuko wa bei) kwa bei za bidhaa inatubidi wadau wa ujenzi tubuni mbinu mpya za kupunguza gharama za ujenzi bila kuathiri ubora (quality and standards). Hapa darasa la ujenzi la waja wema, tumebuni aina ya ujenzi wa ngazi za kipekee, zenye kukidi viwango na kupitiliza viwango na zenye ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu. Bofya link ujionee: Darasa la ujenzi la Madrassatul Abraar latunukiwa Tuzo ya ubunifu wa ujenzi kutoka Shirika la Uingereza.
 
Kila kitu holela, bidhaa aina zote bei juu na ni ndani ya muda mchache sana, serikali imeshindwa kazi, ijiuzulu.

Mwaka jana pamoja na kovidi kutisha kwa kiwango cha hali ya juu hatukuwa na mfumuko wa bei kiwango cha sasa.

Inaonekana Serikali tayari mikononi mwa walanguzi
Sahivi wanajificha kwenye vita ya Ukraine
 
Back
Top Bottom